Wajasiriliamali wa Tanzania tuna lipi la kujifunza kutokana na makosa ya kiufundi / kitaalam ya Mr. Kuku?

Yes shida ni mitaji, Ila sasa lwenye kutafuta mitaji ndo hapo tunakuja na Idea ambazo mwisho wake sio.

NAMINGO wale niliwahi kuwaambia live kwamba Idea ni nzuri ila the way walivyo kuwa wanaitekeleza isingefika kokote kule.

Sasa vitu kama NAMINGO au Mr Kuku vinakuka kufanya Model zingine zisifaulu kwa sababu watu wanafanya comparison.

Idea inaweza kuwa nzuri ila implementation yake ikaleta matatizo makubwa sana Idea ya Mr Kuku ilikuwa ni nzuri sana ila the way alivyo chagua kuifanya ndo shida
Sawa mkuu ila andiko langu vipi lipo sahihi ??
 
Waulize aliowatapeli TMT ndio wanajua ,kwamimi ambaye ni TAPELI mstaafu siwezi kudanganywa na utapeli wa miaka ya 1970s aje kuniletea mtoto wa 1994 leo.
TMT ni kina nani Mkuu.
 
SIMPLE....

Ponzi Scheme; a form of fraud in which belief in the success of a non-existent enterprise is fostered by the payment of quick returns to the first investors from money invested by later investors.

Shareholders / Stakeholders: A shareholder owns part of a public company through shares of stock, while a stakeholder has an interest in the performance of a company for reasons other than stock performance or appreciation

KWAHIO...
Ponzi Scheme na aina za Biashara za hivyo, hakuna product pesa za member A na B zinamlipa member C na kiasi kingine kinaliwa na Mr Ponzi...., huwezi ukatoa guarantee ya returns za ajabu ajabu bila kuwa na uwezekano wa kudanganya watu..., kwenye shareholders / stakeholders kuna uwezekano wa kwamba hao kuku wakaugua ukapata sifuri au demand ikaongezeka ukapata maradufu... (In business and mathematically there is no guarantee of such returns as promised by Mr KUKU) and demand and supply is not infinity there comes the time when the market is saturated..
 
TMT ni kina nani Mkuu.
Mkuu kuna vitu kama huvijui usiwe mwepesi wa kubisha bisha uwe unauliza kama hivi upate jibu.

Ukitaka ushuhuda tafta nyuzi zimo humuhumu zikilalamika kuhusu huyo ontario na TMT yake
 
Mkuu kuna vitu kama huvijui usiwe mwepesi wa kubisha bisha uwe unauliza kama hivi upate jibu.

Ukitaka ushuhuda tafta nyuzi zimo humuhumu zikilalamika kuhusu huyo ontario na TMT yake
Nimebisha nini Mkuu Wangu.
 
I

Ikiwa limetokea hili sawa, maana mimi nilisikia wame block kwa uchunguzi tu.


Na ndicho nilichokisikia kutoka kwake akitolea maelezo kwamba vyombo vya serikali vimeamua kujiridhisha na utendaji wao kisha wangetoa maelekezo ya kuboresha au kuruhusu, matokeo yake ndio imekua kakutwa na hatia.

Sina uelewa sana lakini alichokua anakifanya kilikua kinaonekana, na kwa kuzidiwa na soko, ilifika mahali akawa ananunua kuku kwa wafugaji wengine ili kukidhi mahitaji ya wateja wake.

Sijajua dhuluma ingetokeaje lakini uhakika wa soko alikua nao na bidhaa ( kuku) unawaona.
Shida yangu ilikua kiwango kikubwa cha faida anayogawia wawekezaji. Asilimia kubwa sana, hapo ingeweza kuleta shida mbeleni kwamba watu wengi wangewekeza na kutakiwa kurejesha pesa zao kwa wakati ingeleta shida.

Nilitegemea ifike mahali awe na ukomo kwamba hapokei pesa kwa muda flani au anstafuta ikifika kiwango flsni cha pesa anasitisha kupokea kwa wawekezaji wapya.

Mbona interchick nao kuna muda wanalemewa na soko wanashirikisha watu binafsi kuzalisha kuku kwa msaada na uangalizi wao?
 
Leseni baba leseni..

Namna hiyo ni hatari maana mtoa mchango atalindwa na nini iwapo mjasiriamali akila tu hiyo hela?

Wewe unajiangalia wewe kama mjasiriamali watu wakuamini wakupe hela zao ukila?

Lazima kuwe na check and balances kwamba mwanya wa kuzila au kufanya chochote kinyume usiwepo

Usituambia mambo ya kipumbavu kama "niamini" tu,fvck that,no one anaamini upumbavu,kwenye biashara kila mtu anajiamini yeye tu,infact mimi sometimes siamini myself what myself convinces me!

Sheria nzuri sana kudhibiti embellzement!
 
Yes

Wewe ndio design ya wana JF tunaowahitaji sio kizazi hiki cha kondoo fata mkumbo.

Mwishoni ilikuwa wanasema hawatapokea tena wateja wa kuwekeza wataanza kujiendesha wenyewe that what i know...kuhusu watu kutaperiwa sikuwao kumshuhudia mtu sijawa tayari kuwa kondoo wa mkumbo huo ila nikiona evidence nitakubali nasimamia sehemu sahihi sio walipo wengi.
 
Unavosema watu walete ushahidi wa malalamiko dhidi ya mr kuku. Huu ni ubishi namba 1

Huyo jamaa nimeanza kusikia malalamiko dhidi yake mwaka 2018 November
Nivyema ukaweka shahidi za malalamiko unadhani kilamtu anamfuatilia MR humu, hivyo wasiofuatilie waunge juhudi kikondoo ausio.
 
Nivyema ukaweka shahidi za malalamiko unadhani kilamtu anamfuatilia MR humu, hivyo wasiofuatilie waunge juhudi kikondoo ausio.
Hivi unadhani mimi mtu alinifuata kuja kuniambia jamaa kawatapeli?

Hilo no jukumu lako wewe kufuatilia mambo sio uletewe hapo ulipo
 
Hata Kama Mr kuku alikuwa Ana Nia mbaya ya kuwabamiza watu,lakini kwa kijana wa miaka 29,kuweza kuanzisha kitu,na kukusanya bilioni 17!hiyo ni akili kubwa!
Kuna watu wapo serikalini,bungeni kwa miaka 40,hawana hata kakampuni ka kufunga maji.
Vijana kawa ilibidi wakusanywe,wapewe msaada,watumike vzr,ujuzi wao utumike vzr kuanzisha mambo makubwa,
Bahati mbaya,hii nchi Haina thinkers wanaoweza kuwatumia vijana Kama Hawa,ni hakika huyu kijana,akili inachaji kweli kweli!
Sasa atakutana na system ilyojaa,mizee mivimba macho,atahukumiwa,atapigwa faini,atafilisiwa,Kwisha habari,
Serikali yenyewe,ilishindwa kwenye Ishu ya korosho,ikawapa hasara wakulima,
Huyu ilibidi awekwe sehemu,apewe mwongozo,kwa kutumia bichwa lake,alete vitu ,mipango,business plans,ambazo zitainufaisha nchi.
China,kila kijana anafundishwa,lengo lake liwe kuifanya China iwe superpower,achangie anavyoweza,ndio maana wafanyakazi wote wa kichina,waliopo USA,ulaya,lengo lao ni moja tu,iba Siri za kila kitu,uchumi,kilimo,sayansi,pereka nyumbani,China.
Hebu fikiria Kama kila MTZ,popote alipo duniani atakuwa anafanya udukuzi kwa ajiri ya nchi!
Tutakuwa na maspy kibao,na vyanzo kibao vya taarifa/Intel.
 

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba kushikiliwa kwa account zake, sababu haikua malalamiko ya utapeli. Yule jamaa kafanya hiyo kazi kwa zaidi ya miaka mitatu na hakukuwahi kutokea malalamiko ( vinginevyo niseme sijawahi kusikia malalamiko binafsi).

Tukirudi kwa serikali, kwa mtu aliyefanya kazi namna ile huku akijitangaza anavyoendesha kazi zake walimwacha tu kipindi chote hicho kwanini? Ikiwa kuna mapungufu na hakuna dhuluma imejitokeza, kwanini wasitoe maelekezo ya utaratibu gani utumike? Vinginevyo itakua ni chuki na nia ovu serikali kukwamisha juhudi za wajasiriamali.

Ikiwa amekutwa na hatia ya kudhulumu watu au makosa mengine, sheria ichukue mkondo wake. Lakini kutumia mifumo kama DECI au Forex kumtuhumu Mr. Kuku sio sawa.
 

Serikali yeti haitaki kuwa na uhusiano au urafiki wa aina hiyo na raia wake. Huyu kijana alitakiwa aelekezwe alipokosea au sheria zilizokiukwa.

Kwa kumfungulia kesi na kushikilia akaunti zake itasababisha madhara kwa wawekezaji wengi sana waliokua wanatarajia wapate faida.

Lakini mbaya zaidi, itaua na kudidimiza mawazo ya kibunifu kwa kuleta hofu na woga.
 
Hivi unadhani mimi mtu alinifuata kuja kuniambia jamaa kawatapeli?

Hilo no jukumu lako wewe kufuatilia mambo sio uletewe hapo ulipo
Huna evidence bana kubali kuwa wewe fata upepo mada yoyote ikiletwa jamvini ukiona upepo uko wapi unaungana nao bila kuhoji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…