Wajasiriliamali wa Tanzania tuna lipi la kujifunza kutokana na makosa ya kiufundi / kitaalam ya Mr. Kuku?

Wajasiriliamali wa Tanzania tuna lipi la kujifunza kutokana na makosa ya kiufundi / kitaalam ya Mr. Kuku?

Yes shida ni mitaji, Ila sasa lwenye kutafuta mitaji ndo hapo tunakuja na Idea ambazo mwisho wake sio.

NAMINGO wale niliwahi kuwaambia live kwamba Idea ni nzuri ila the way walivyo kuwa wanaitekeleza isingefika kokote kule.

Sasa vitu kama NAMINGO au Mr Kuku vinakuka kufanya Model zingine zisifaulu kwa sababu watu wanafanya comparison.

Idea inaweza kuwa nzuri ila implementation yake ikaleta matatizo makubwa sana Idea ya Mr Kuku ilikuwa ni nzuri sana ila the way alivyo chagua kuifanya ndo shida
Sawa mkuu ila andiko langu vipi lipo sahihi ??
 
Waulize aliowatapeli TMT ndio wanajua ,kwamimi ambaye ni TAPELI mstaafu siwezi kudanganywa na utapeli wa miaka ya 1970s aje kuniletea mtoto wa 1994 leo.
TMT ni kina nani Mkuu.
 
SIMPLE....

Ponzi Scheme; a form of fraud in which belief in the success of a non-existent enterprise is fostered by the payment of quick returns to the first investors from money invested by later investors.

Shareholders / Stakeholders: A shareholder owns part of a public company through shares of stock, while a stakeholder has an interest in the performance of a company for reasons other than stock performance or appreciation

KWAHIO...
Ponzi Scheme na aina za Biashara za hivyo, hakuna product pesa za member A na B zinamlipa member C na kiasi kingine kinaliwa na Mr Ponzi...., huwezi ukatoa guarantee ya returns za ajabu ajabu bila kuwa na uwezekano wa kudanganya watu..., kwenye shareholders / stakeholders kuna uwezekano wa kwamba hao kuku wakaugua ukapata sifuri au demand ikaongezeka ukapata maradufu... (In business and mathematically there is no guarantee of such returns as promised by Mr KUKU) and demand and supply is not infinity there comes the time when the market is saturated..
 
TMT ni kina nani Mkuu.
Mkuu kuna vitu kama huvijui usiwe mwepesi wa kubisha bisha uwe unauliza kama hivi upate jibu.

Ukitaka ushuhuda tafta nyuzi zimo humuhumu zikilalamika kuhusu huyo ontario na TMT yake
 
Mkuu kuna vitu kama huvijui usiwe mwepesi wa kubisha bisha uwe unauliza kama hivi upate jibu.

Ukitaka ushuhuda tafta nyuzi zimo humuhumu zikilalamika kuhusu huyo ontario na TMT yake
Nimebisha nini Mkuu Wangu.
 
I

Ikiwa limetokea hili sawa, maana mimi nilisikia wame block kwa uchunguzi tu.

Na ndicho nilichokisikia kutoka kwake akitolea maelezo kwamba vyombo vya serikali vimeamua kujiridhisha na utendaji wao kisha wangetoa maelekezo ya kuboresha au kuruhusu, matokeo yake ndio imekua kakutwa na hatia.

Sina uelewa sana lakini alichokua anakifanya kilikua kinaonekana, na kwa kuzidiwa na soko, ilifika mahali akawa ananunua kuku kwa wafugaji wengine ili kukidhi mahitaji ya wateja wake.

Sijajua dhuluma ingetokeaje lakini uhakika wa soko alikua nao na bidhaa ( kuku) unawaona.
Shida yangu ilikua kiwango kikubwa cha faida anayogawia wawekezaji. Asilimia kubwa sana, hapo ingeweza kuleta shida mbeleni kwamba watu wengi wangewekeza na kutakiwa kurejesha pesa zao kwa wakati ingeleta shida.

Nilitegemea ifike mahali awe na ukomo kwamba hapokei pesa kwa muda flani au anstafuta ikifika kiwango flsni cha pesa anasitisha kupokea kwa wawekezaji wapya.

Mbona interchick nao kuna muda wanalemewa na soko wanashirikisha watu binafsi kuzalisha kuku kwa msaada na uangalizi wao?
 
Watu ambao wana comment negatively ni kwa sababu ya kutokua na uelewewa na concept mpya ya crowd farming.

Crowd farming
ni kuanzisha kilimo aidha cha matunda au ufugaji wa kuku au ngombe nk. lakini kwa kushirikisha wadau wa kawaida kama Mimi na wewe ambao hatuna muda wa kusimamia ufugaji na pia uwezo binafsi wa kipesa ni mdogo kuanzisha biashara ya ufugaji.

According to google: Crowd farming is a model where a number of investors share risks and own shares in a farming venture.
The origins of the "crowd" concept can be traced to crowd sourcing where a large number of people are invited to participate in a project.

Aina hii ya kilimo imeshika kasi sana Nigeria.

Huku Nigeria inaitwa crowd farming au online farming (najua hili neno watu hawapendi kulisikia kilimo cha mtandao) Lakini ukijifunza kufatilia vitu kwa undani sidhani kama utakuwa ni mtu wa kupelekwa na mawambi ya watu.

Kuna makampuni mengi sana ambayo yanatumia huu mfumo huko Nigeria na south Africa, Na pia hii concept bado ni ngeni sana kwa hiyo watu wanakuwa negative kisa tu ni kitu kigeni.

Nimefatilia makampuni Mengi ambayo yanatumia mfumo huu na faida kwa wawekezaji ni kuanzia 10%-50%.

Baadhi ya makampuni ni yafutayo (Nigeria):

1. thriveagric.com
2. farmcrowdy.com
3. farmkart.ng
4. porkmoney.com
5. efarms.com.ng/end
6. payfarmer.com
7. agropartnerships.co
8. tradersofafrica.com
9. farmfunded.com
10. ez-farming.com
11. menorahfarms.com
12. farmagric.com
13. farmbuddy.ng
14. groupfarma.com.ng
15. greenfoldfarmprojects.com
16. smartfarm.com.ng

Investment cycles kwa nyingi naona ni kuanzia miezi 4 hadi 12.

Anyway nirudi kwa Mr Kuku anatumia the same mode of operation yaani crowd farming, investment cycle yake ni miezi 4 hadi 6. Na pia soko la uhakika analo, (contract farming)unaingia mikataba awali ya kusupply kuku constantly kwa muda maalum ili mwishoni mwa huu muda ndo ulipwe malipo. (Hii Ina maana unahitaji capital kubwa sana ya kuweza kuendesha mradi bila kuaffect supply ya kuku. Meaning investors au crowd farmers that's where they come in)

Simple facts mt kuku farms
Ana kuku 90,000+
Ana chinja 3000+ every week

Kuhusu masoko ngoja nikupe scenario.

Acacia/Barrick wanaotumia 2500-3000 chickens per week
American Embassy/washirika 1000+ chickens per month
Geita Gold Mine wanahitaji 3000 chickens per week
Bado hizi hotel kubwa na masupplier wadogo wanaopelekea masokoni etc.

Advantages ziko hivi:
Mfano Mimi nimeajiriwa natoka kazini saa mbili usiku nafanya kazi hadi Jumapili. Muda wa kuanzisha na kusimamia mradi sina Na hata ulisema mkopeshe mtu pesa mtaishia kugombana.

Kwa hiyo pesa zangu ambazo nimesave naziwekeza huku kama investor nakuwa kama vile nimenunua shares ambazo zitamature ndani ya muda Fulani.Kwahiyo nakuwa ufugaji unafanywa wa kuku unafanywa kwa niaba yangu.

Ni kama kununua shares kwenye kampuni la Coca Cola au Vodacom, wakutumia pesa yako kuendesha biashara mwishoni mwa muda Fulani aidha mwaka miezi sita au Tisa ukalipwa profits in form of dividends.

Mimi binafsi nakusanya pesa zangu naenda kuziweka huko.

By the way kama kuna mtu amesikia kuna crowd farming nyingine mbali na Mr kuku, please anijulishe.

Risks
Ofcoz just like any other business, kuna risks za kuconsider kabla hujaweka pesa yako huku kwenye hii miradi. It's your job to determine whether you can accept the risks or not. Kitalaam inaitwa Risk appetite. Is your risk appetite high or low; mfano Mimi am willing to risk 5 million, mwingine na risk 7million etc.

Mr kuku farms hii concept yeye ndo kaintroduce Tanzania kwa sasa hivi bado hajapata competition yoyote, naona kuna huyu jamaa mwingine anaitwa Weku enterprises.

Mwaka juzi kama sikosei kuna Tender mmoja ilitangazwa na US Embassy au International school of Tanganyika walikua wanataka supplier mkubwa wa kuku at least 1000 per month na hawataki excuses, sio unaanza mwezi huu mara mwezi ujao unaanza kuleta sababu mara sijui mtaji umekata nk.

Kwa kutumia crowd farming Mr kuku anaweza supply US embassy.

Pia kuna huyu jamaa wa South Africa anasema unanunua ngombe na kumuhudumia mpaka anakua hadi kummuuza for a profit...livestock wealth.com

Kwa hiyo jamani ndugu zangu tusipende kuhukumu vitu bila kufanya research. Tusipende kujibu kwa mihemko kwa sababu tu uliwahi poteza fedha zako sijui ukaliwa pesa zako.

TUJIFUNZE KUSOMA NA KUFATILIA VITU KIUNDANI KABLA HATUJA KATISHA TAMAA WATU. TUKIENDELEA HIVI KILA SIKU TUTABAKI NYUMA SIKU ZOTE.
Leseni baba leseni..

Namna hiyo ni hatari maana mtoa mchango atalindwa na nini iwapo mjasiriamali akila tu hiyo hela?

Wewe unajiangalia wewe kama mjasiriamali watu wakuamini wakupe hela zao ukila?

Lazima kuwe na check and balances kwamba mwanya wa kuzila au kufanya chochote kinyume usiwepo

Usituambia mambo ya kipumbavu kama "niamini" tu,fvck that,no one anaamini upumbavu,kwenye biashara kila mtu anajiamini yeye tu,infact mimi sometimes siamini myself what myself convinces me!

Sheria nzuri sana kudhibiti embellzement!
 
Na ndicho nilichokisikia kutoka kwake akitolea maelezo kwamba vyombo vya serikali vimeamua kujiridhisha na utendaji wao kisha wangetoa maelekezo ya kuboresha au kuruhusu, matokeo yake ndio imekua kakutwa na hatia.

Sina uelewa sana lakini alichokua anakifanya kilikua kinaonekana, na kwa kuzidiwa na soko, ilifika mahali akawa ananunua kuku kwa wafugaji wengine ili kukidhi mahitaji ya wateja wake.

Sijajua dhuluma ingetokeaje lakini uhakika wa soko alikua nao na bidhaa ( kuku) unawaona.
Shida yangu ilikua kiwango kikubwa cha faida anayogawia wawekezaji. Asilimia kubwa sana, hapo ingeweza kuleta shida mbeleni kwamba watu wengi wangewekeza na kutakiwa kurejesha pesa zao kwa wakati ingeleta shida.

Nilitegemea ifike mahali awe na ukomo kwamba hapokei pesa kwa muda flani au anstafuta ikifika kiwango flsni cha pesa anasitisha kupokea kwa wawekezaji wapya.

Mbona interchick nao kuna muda wanalemewa na soko wanashirikisha watu binafsi kuzalisha kuku kwa msaada na uangalizi wao?
Yes

Wewe ndio design ya wana JF tunaowahitaji sio kizazi hiki cha kondoo fata mkumbo.

Mwishoni ilikuwa wanasema hawatapokea tena wateja wa kuwekeza wataanza kujiendesha wenyewe that what i know...kuhusu watu kutaperiwa sikuwao kumshuhudia mtu sijawa tayari kuwa kondoo wa mkumbo huo ila nikiona evidence nitakubali nasimamia sehemu sahihi sio walipo wengi.
 
Unavosema watu walete ushahidi wa malalamiko dhidi ya mr kuku. Huu ni ubishi namba 1

Huyo jamaa nimeanza kusikia malalamiko dhidi yake mwaka 2018 November
Nivyema ukaweka shahidi za malalamiko unadhani kilamtu anamfuatilia MR humu, hivyo wasiofuatilie waunge juhudi kikondoo ausio.
 
Nivyema ukaweka shahidi za malalamiko unadhani kilamtu anamfuatilia MR humu, hivyo wasiofuatilie waunge juhudi kikondoo ausio.
Hivi unadhani mimi mtu alinifuata kuja kuniambia jamaa kawatapeli?

Hilo no jukumu lako wewe kufuatilia mambo sio uletewe hapo ulipo
 
Hata Kama Mr kuku alikuwa Ana Nia mbaya ya kuwabamiza watu,lakini kwa kijana wa miaka 29,kuweza kuanzisha kitu,na kukusanya bilioni 17!hiyo ni akili kubwa!
Kuna watu wapo serikalini,bungeni kwa miaka 40,hawana hata kakampuni ka kufunga maji.
Vijana kawa ilibidi wakusanywe,wapewe msaada,watumike vzr,ujuzi wao utumike vzr kuanzisha mambo makubwa,
Bahati mbaya,hii nchi Haina thinkers wanaoweza kuwatumia vijana Kama Hawa,ni hakika huyu kijana,akili inachaji kweli kweli!
Sasa atakutana na system ilyojaa,mizee mivimba macho,atahukumiwa,atapigwa faini,atafilisiwa,Kwisha habari,
Serikali yenyewe,ilishindwa kwenye Ishu ya korosho,ikawapa hasara wakulima,
Huyu ilibidi awekwe sehemu,apewe mwongozo,kwa kutumia bichwa lake,alete vitu ,mipango,business plans,ambazo zitainufaisha nchi.
China,kila kijana anafundishwa,lengo lake liwe kuifanya China iwe superpower,achangie anavyoweza,ndio maana wafanyakazi wote wa kichina,waliopo USA,ulaya,lengo lao ni moja tu,iba Siri za kila kitu,uchumi,kilimo,sayansi,pereka nyumbani,China.
Hebu fikiria Kama kila MTZ,popote alipo duniani atakuwa anafanya udukuzi kwa ajiri ya nchi!
Tutakuwa na maspy kibao,na vyanzo kibao vya taarifa/Intel.
 
Yes

Wewe ndio design ya wana JF tunaowahitaji sio kizazi hiki cha kondoo fata mkumbo.

Mwishoni ilikuwa wanasema hawatapokea tena wateja wa kuwekeza wataanza kujiendesha wenyewe that what i know...kuhusu watu kutaperiwa sikuwao kumshuhudia mtu sijawa tayari kuwa kondoo wa mkumbo huo ila nikiona evidence nitakubali nasimamia sehemu sahihi sio walipo wengi.

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba kushikiliwa kwa account zake, sababu haikua malalamiko ya utapeli. Yule jamaa kafanya hiyo kazi kwa zaidi ya miaka mitatu na hakukuwahi kutokea malalamiko ( vinginevyo niseme sijawahi kusikia malalamiko binafsi).

Tukirudi kwa serikali, kwa mtu aliyefanya kazi namna ile huku akijitangaza anavyoendesha kazi zake walimwacha tu kipindi chote hicho kwanini? Ikiwa kuna mapungufu na hakuna dhuluma imejitokeza, kwanini wasitoe maelekezo ya utaratibu gani utumike? Vinginevyo itakua ni chuki na nia ovu serikali kukwamisha juhudi za wajasiriamali.

Ikiwa amekutwa na hatia ya kudhulumu watu au makosa mengine, sheria ichukue mkondo wake. Lakini kutumia mifumo kama DECI au Forex kumtuhumu Mr. Kuku sio sawa.
 
Nivyema ukaweka shahidi za malalamiko unadhani kilamtu anamfuatilia MR humu, hivyo wasiofuatilie waunge juhudi kikondoo ausio.
Hivi tuhuma juu yake?
Screenshot_20200813-102831.jpg
View attachment 1535755
 
Hata Kama Mr kuku alikuwa Ana Nia mbaya ya kuwabamiza watu,lakini kwa kijana wa miaka 29,kuweza kuanzisha kitu,na kukusanya bilioni 17!hiyo ni akili kubwa!
Kuna watu wapo serikalini,bungeni kwa miaka 40,hawana hata kakampuni ka kufunga maji.
Vijana kawa ilibidi wakusanywe,wapewe msaada,watumike vzr,ujuzi wao utumike vzr kuanzisha mambo makubwa,
Bahati mbaya,hii nchi Haina thinkers wanaoweza kuwatumia vijana Kama Hawa,ni hakika huyu kijana,akili inachaji kweli kweli!
Sasa atakutana na system ilyojaa,mizee mivimba macho,atahukumiwa,atapigwa faini,atafilisiwa,Kwisha habari,
Serikali yenyewe,ilishindwa kwenye Ishu ya korosho,ikawapa hasara wakulima,
Huyu ilibidi awekwe sehemu,apewe mwongozo,kwa kutumia bichwa lake,alete vitu ,mipango,business plans,ambazo zitainufaisha nchi.
China,kila kijana anafundishwa,lengo lake liwe kuifanya China iwe superpower,achangie anavyoweza,ndio maana wafanyakazi wote wa kichina,waliopo USA,ulaya,lengo lao ni moja tu,iba Siri za kila kitu,uchumi,kilimo,sayansi,pereka nyumbani,China.
Hebu fikiria Kama kila MTZ,popote alipo duniani atakuwa anafanya udukuzi kwa ajiri ya nchi!
Tutakuwa na maspy kibao,na vyanzo kibao vya taarifa/Intel.

Serikali yeti haitaki kuwa na uhusiano au urafiki wa aina hiyo na raia wake. Huyu kijana alitakiwa aelekezwe alipokosea au sheria zilizokiukwa.

Kwa kumfungulia kesi na kushikilia akaunti zake itasababisha madhara kwa wawekezaji wengi sana waliokua wanatarajia wapate faida.

Lakini mbaya zaidi, itaua na kudidimiza mawazo ya kibunifu kwa kuleta hofu na woga.
 
Hivi unadhani mimi mtu alinifuata kuja kuniambia jamaa kawatapeli?

Hilo no jukumu lako wewe kufuatilia mambo sio uletewe hapo ulipo
Huna evidence bana kubali kuwa wewe fata upepo mada yoyote ikiletwa jamvini ukiona upepo uko wapi unaungana nao bila kuhoji.
 
Back
Top Bottom