Wajasiriliamali wa Tanzania tuna lipi la kujifunza kutokana na makosa ya kiufundi / kitaalam ya Mr. Kuku?

Exactly, investment and wealth management zina taratibu zake. Huwezi tu kukusanya hela za watu na kuanza kuwekeza
 
Sawa kabisa mkuu
 
Wapi nimemtetea hivi nyie GT munatatizo kwenye ombwe au.
 
Ponzi scheme ina cha ukomo wa kuwekeza? Endeleeni kujiliwaza..
 
Ubunifu au utapeli? Wapigeni lecture feki zenu waliolala.
 
Wapi nimemtetea hivi nyie GT munatatizo kwenye ombwe au.
Wewe unaelezea na kutolea mawazo jambo usilolijua. Nashangaa sana watanzania wengi wanadhani fedha zinapatikana kwa urahisi namna hii. Mtu anakusanya mamilioni ya fedha eti kufanya mradi wa kufuga kuku wakati hakuwahi hata kufuga kuku 1000! Bongo za kuamini vitu vya Alinacha kama hivi utazipata Bongo tu...
 
Ponzi scheme ina cha ukomo wa kuwekeza? Endeleeni kujiliwaza..

Umesoma vizuri nilichokiandika?

Hapo ndipo shida yangu. Uwekezaji wowote amba usiodhibitiwa na usiokua na kikomo cha uwekezaji kwa kuahidi faida ile ile mwisho hauwezi kuwa mwema.
 
Umesoma vizuri nilichokiandika?

Hapo ndipo shida yangu. Uwekezaji wowote amba usiodhibitiwa na usiokua na kikomo cha uwekezaji kwa kuahidi faida ile ile mwisho hauwezi kuwa mwema.
Huu wa Mr Kuku siyo uwekezaji. Ni Ponzi Scheme. Kuna tofauti kubwa kati ya uwekezaji na Ponzi Scheme. Wewe unaita huu ni uwekezaji.
 
Huu wa Mr Kuku siyo uwekezaji. Ni Ponzi Scheme. Kuna tofauti kubwa kati ya uwekezaji na Ponzi Scheme. Wewe unaita huu ni uwekezaji.

Eleza hapa hizo tofauti. Nimeona mahali unaandika jamaa hajawahi kufuga hata kuku 1000, una uhakika na hiyo habari uliyoiandika?

Unajua kwamba walikua na duka la kuku na mayai Namanga? Hilo ni moja nnalolifaham mimi.

Unajua kwamba wameshafanya hiyo biashara kwa zaidi ya miaka mitatu?

Na unajua kwamba walikua na wateja soko kubwa zikiwemo shule, makampuni ya mawasiliano na ya migodi?
 
Ubishi wa wa kibongo bongo hauna mantiki yoyote. Hii ni Ponzi na usifanye watu wengine ni wajinga! Narudia tena. Hakuwa mfugaji na alitumia kizingizio cha kuku kukusanya fedha. Ni ponzi.
 
Lecture fake ndio wewe ueleze unachokijua ili hii isiwe fake sasa.
Bujibuji kaleta uzi tujadili mambo ya kujifunza kwa kilichomkuta Mr. Kuku. Kila mtu anaandika kadri alivyoifaham Mr. Kuku.
Utajifunza nini kwenye Ponzi Scheme? Tujifunze namna ya kuibia watu? Kama ni kujifunza miradi ya ufugaji au kilimo hii thread haifundishi chochote. Mnakuja na ufugaji au kilimo cha kwenye Internet mnakuja ''kufundisha'' watu walio site? Mambo yangekuwa rahisi namna hiyo hii dunia ingekuwa na watu mafukara. Au unadhani kufuga kuku wengi ni jambo geni watu wasiolijua. Najua kabisa Ponzi huwa inakusanya fedha nyingi na kunakuwa na wanufaika wachache ambao wako tayari kufanya lolote ili watu wasiwashtukie utapeli wao.
 
Jibu swali moja tu. Mr. Kuku alikua anafuga kuku au hakua nao?

Naona kuelezea Ponzi na Uwekezaji imezua mengine.
 
Kiongozi kampuni ya mr kuku ilikuwa ya aina gani? Public limited au private limited?
 
Ubishi wa wa kibongo bongo hauna mantiki yoyote. Hii ni Ponzi na usifanye watu wengine ni wajinga! Narudia tena. Hakuwa mfugaji na alitumia kizingizio cha kuku kukusanya fedha. Ni ponzi.

Sipo hapa kufanya mtu/ watu wajinga nikiwa na uwezo huo ntakua sio mtu wa kawaida.

Kwanini unasema nafanya ubishi? Unalifaham duka la Mr. Kuku la Namanga? Umeshawahi kufika kwenye mashamba yao Kigamboni?

Jibu hayo maswali
 
Kila nchi Ina utaratibu na sheria zake.. Kukusanya AMANA Au kukusanya MTAJI kutoka kwa wanachi kuna sheria zake...
Ndio maana TBL etc wakitaka mitaji wanaenda soko LA mitaji na dhamana. Msitake kuhalalisha shortcut wakati pesa za watu zinakuwa rehani INCASE anything happen..
 
Sipo hapa kufanya mtu/ watu wajinga nikiwa na uwezo huo ntakua sio mtu wa kawaida.

Kwanini unasema nafanya ubishi? Unalifaham duka la Mr. Kuku la Namanga? Umeshawahi kufika kwenye mashamba yao Kigamboni?

Jibu hayo maswali
Hayo ni magumashi na aliweka kuvutia watu ili awapige vizuri. Ni ponzi hii. Ni utapeli.
 
Kwanini unaita Ponzi Scheme??
 
Ipi sheria ya Tanzania ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…