Wajasiriliamali wa Tanzania tuna lipi la kujifunza kutokana na makosa ya kiufundi / kitaalam ya Mr. Kuku?

Mpaka kaingia kwenye matatizo alishaanza kushindwa kulipa watu faida. Mradi ulishaanza kusua sua. Msg hajibu alitegemea watu wakae kimya kuhusu hela zao. Watu washawekeza wanategemea baada ya mieizi sita kulipwa utawaambia nini wakati hukuwaeleza uhalisia wa mradi na risk iliyopo. Challenge gani zikitokea mtu hataweza kulipwa mpaka hapo faida itakapopatikana ambayo inaweza kupitiliza ile miezi sita aliyoahidi. Kwasababu hata hayo makampuni kama hayajatengeneza faida, mwekezaji hutalipwa sasa yeye hakuwaambia the other side of the story alikua anapeleka mambo kienyeji enyeji.
Exactly, investment and wealth management zina taratibu zake. Huwezi tu kukusanya hela za watu na kuanza kuwekeza
 
Sawa kabisa mkuu
SIMPLE....

Ponzi Scheme; a form of fraud in which belief in the success of a non-existent enterprise is fostered by the payment of quick returns to the first investors from money invested by later investors.

Shareholders / Stakeholders: A shareholder owns part of a public company through shares of stock, while a stakeholder has an interest in the performance of a company for reasons other than stock performance or appreciation

KWAHIO...
Ponzi Scheme na aina za Biashara za hivyo, hakuna product pesa za member A na B zinamlipa member C na kiasi kingine kinaliwa na Mr Ponzi...., huwezi ukatoa guarantee ya returns za ajabu ajabu bila kuwa na uwezekano wa kudanganya watu..., kwenye shareholders / stakeholders kuna uwezekano wa kwamba hao kuku wakaugua ukapata sifuri au demand ikaongezeka ukapata maradufu... (In business and mathematically there is no guarantee of such returns as promised by Mr KUKU) and demand and supply is not infinity there comes the time when the market is saturated..
 
una jaribu sana kumtetea uyu jamaa lakin moshi ulikwisha anza kufoka kuanzia kweny groups zake za whatsapp watu wakiwa hawajui hatma yao
pia kupitia page zake za instagram ambapo pia malalamiko ya wawekezaji yake walianza kupeleka malalamiko jamaa ali amua kuzuia comments ambao hata sasa uki ingia kweny hzo pages comments zime blockiwa huoni ni tatizo hili?
kwann uzuie uhuru wa watu kuchangia kuutaka kuujua ukweli kuhusu fedha zao walizo ziwekeza kwako?
Wapi nimemtetea hivi nyie GT munatatizo kwenye ombwe au.
 
Na ndicho nilichokisikia kutoka kwake akitolea maelezo kwamba vyombo vya serikali vimeamua kujiridhisha na utendaji wao kisha wangetoa maelekezo ya kuboresha au kuruhusu, matokeo yake ndio imekua kakutwa na hatia.

Sina uelewa sana lakini alichokua anakifanya kilikua kinaonekana, na kwa kuzidiwa na soko, ilifika mahali akawa ananunua kuku kwa wafugaji wengine ili kukidhi mahitaji ya wateja wake.

Sijajua dhuluma ingetokeaje lakini uhakika wa soko alikua nao na bidhaa ( kuku) unawaona.
Shida yangu ilikua kiwango kikubwa cha faida anayogawia wawekezaji. Asilimia kubwa sana, hapo ingeweza kuleta shida mbeleni kwamba watu wengi wangewekeza na kutakiwa kurejesha pesa zao kwa wakati ingeleta shida.

Nilitegemea ifike mahali awe na ukomo kwamba hapokei pesa kwa muda flani au anstafuta ikifika kiwango flsni cha pesa anasitisha kupokea kwa wawekezaji wapya.

Mbona interchick nao kuna muda wanalemewa na soko wanashirikisha watu binafsi kuzalisha kuku kwa msaada na uangalizi wao?
Ponzi scheme ina cha ukomo wa kuwekeza? Endeleeni kujiliwaza..
 
Serikali yeti haitaki kuwa na uhusiano au urafiki wa aina hiyo na raia wake. Huyu kijana alitakiwa aelekezwe alipokosea au sheria zilizokiukwa.

Kwa kumfungulia kesi na kushikilia akaunti zake itasababisha madhara kwa wawekezaji wengi sana waliokua wanatarajia wapate faida.

Lakini mbaya zaidi, itaua na kudidimiza mawazo ya kibunifu kwa kuleta hofu na woga.
Ubunifu au utapeli? Wapigeni lecture feki zenu waliolala.
 
Wapi nimemtetea hivi nyie GT munatatizo kwenye ombwe au.
Wewe unaelezea na kutolea mawazo jambo usilolijua. Nashangaa sana watanzania wengi wanadhani fedha zinapatikana kwa urahisi namna hii. Mtu anakusanya mamilioni ya fedha eti kufanya mradi wa kufuga kuku wakati hakuwahi hata kufuga kuku 1000! Bongo za kuamini vitu vya Alinacha kama hivi utazipata Bongo tu...
 
Ponzi scheme ina cha ukomo wa kuwekeza? Endeleeni kujiliwaza..

Umesoma vizuri nilichokiandika?

Hapo ndipo shida yangu. Uwekezaji wowote amba usiodhibitiwa na usiokua na kikomo cha uwekezaji kwa kuahidi faida ile ile mwisho hauwezi kuwa mwema.
 
Huu wa Mr Kuku siyo uwekezaji. Ni Ponzi Scheme. Kuna tofauti kubwa kati ya uwekezaji na Ponzi Scheme. Wewe unaita huu ni uwekezaji.
 
Eleza hapa hizo tofauti. Nimeona mahali unaandika jamaa hajawahi kufuga hata kuku 1000, una uhakika na hiyo habari uliyoiandika?

Unajua kwamba walikua na duka la kuku na mayai Namanga? Hilo ni moja nnalolifaham mimi.

Unajua kwamba wameshafanya hiyo biashara kwa zaidi ya miaka mitatu?

Na unajua kwamba walikua na wateja soko kubwa zikiwemo shule, makampuni ya mawasiliano na ya migodi?
 
Ubishi wa wa kibongo bongo hauna mantiki yoyote. Hii ni Ponzi na usifanye watu wengine ni wajinga! Narudia tena. Hakuwa mfugaji na alitumia kizingizio cha kuku kukusanya fedha. Ni ponzi.
 
Lecture fake ndio wewe ueleze unachokijua ili hii isiwe fake sasa.
Bujibuji kaleta uzi tujadili mambo ya kujifunza kwa kilichomkuta Mr. Kuku. Kila mtu anaandika kadri alivyoifaham Mr. Kuku.
Utajifunza nini kwenye Ponzi Scheme? Tujifunze namna ya kuibia watu? Kama ni kujifunza miradi ya ufugaji au kilimo hii thread haifundishi chochote. Mnakuja na ufugaji au kilimo cha kwenye Internet mnakuja ''kufundisha'' watu walio site? Mambo yangekuwa rahisi namna hiyo hii dunia ingekuwa na watu mafukara. Au unadhani kufuga kuku wengi ni jambo geni watu wasiolijua. Najua kabisa Ponzi huwa inakusanya fedha nyingi na kunakuwa na wanufaika wachache ambao wako tayari kufanya lolote ili watu wasiwashtukie utapeli wao.
 
Jibu swali moja tu. Mr. Kuku alikua anafuga kuku au hakua nao?

Naona kuelezea Ponzi na Uwekezaji imezua mengine.
 
Eleza hapa hizo tofauti. Nimeona mahali unaandika jamaa hajawahi kufuga hata kuku 1000, una uhakika na hiyo habari uliyoiandika?

Unajua kwamba walikua na duka la kuku na mayai Namanga? Hilo ni moja nnalolifaham mimi.

Unajua kwamba wameshafanya hiyo biashara kwa zaidi ya miaka mitatu?

Na unajua kwamba walikua na wateja soko kubwa zikiwemo shule, makampuni ya mawasiliano na ya migodi?
Kiongozi kampuni ya mr kuku ilikuwa ya aina gani? Public limited au private limited?
 
Ubishi wa wa kibongo bongo hauna mantiki yoyote. Hii ni Ponzi na usifanye watu wengine ni wajinga! Narudia tena. Hakuwa mfugaji na alitumia kizingizio cha kuku kukusanya fedha. Ni ponzi.

Sipo hapa kufanya mtu/ watu wajinga nikiwa na uwezo huo ntakua sio mtu wa kawaida.

Kwanini unasema nafanya ubishi? Unalifaham duka la Mr. Kuku la Namanga? Umeshawahi kufika kwenye mashamba yao Kigamboni?

Jibu hayo maswali
 
Kila nchi Ina utaratibu na sheria zake.. Kukusanya AMANA Au kukusanya MTAJI kutoka kwa wanachi kuna sheria zake...
Ndio maana TBL etc wakitaka mitaji wanaenda soko LA mitaji na dhamana. Msitake kuhalalisha shortcut wakati pesa za watu zinakuwa rehani INCASE anything happen..
 
Hayo ni magumashi na aliweka kuvutia watu ili awapige vizuri. Ni ponzi hii. Ni utapeli.
 
Utajifunza nini kwenye Ponzi Scheme? Tujifunze namna ya kuibia watu? Kama ni kujifunza miradi ya ufugaji au kilimo hii thread haifundishi chochote. Mnakuja na ufugaji au kilimo cha kwenye Internet mnakuja ''kufundisha'' watu walio site? Mambo yangekuwa rahisi namna hiyo hii dunia ingekuwa na watu mafukara. Au unadhani kufuga kuku wengi ni jambo geni watu wasiolijua. Najua kabisa Ponzi huwa inakusanya fedha nyingi na kunakuwa na wanufaika wachache ambao wako tayari kufanya lolote ili watu wasiwashtukie utapeli wao.
Kwanini unaita Ponzi Scheme??
 
Kila nchi Ina utaratibu na sheria zake.. Kukusanya AMANA Au kukusanya MTAJI kutoka kwa wanachi kuna sheria zake...
Ndio maana TBL etc wakitaka mitaji wanaenda soko LA mitaji na dhamana. Msitake kuhalalisha shortcut wakati pesa za watu zinakuwa rehani INCASE anything happen..
Ipi sheria ya Tanzania ??
 
Back
Top Bottom