A
Anonymous
Guest
Kama kinavyoonekana hiki ndicho Kituo cha Afya Nyangoto, kinapatikana Mkoa wa Mara, Wilaya ya Tarime Vijijini, Kata ya Matongo (eneo kwa ujumla linafahamika kama Nyamongo).
Changamoto yake
Ni Wamama Wajawazito kutozwa 3000/=tshs kila anapohudhuria kliniki na wa wale wanaoanza wanalipia 10,000/=tshs.
Hawatoi risiti bali anayepima damu maabara wanaweka mfukoni bila kutoa 3,000tshs hawapewi huduma.
Kibaya zaidi mama mjamzito anaweza kukaa kuanzia saa mbili asubuhi hadi hata saa kumi na moja akifika kwa mhudumu anambadilishia tarehe na kumwambia tarehe ulioandikiwa siyo sahihi, hivyo anabadilishiwa tarehe bila kupewa huduma na pesa tayari wameshachukua, siku akirudi tena anatoa hela tena upya.
Pia wakati mwingine mama anayeanza kliniki anatozwa 10,000/= lakini hata kadi anayopewa ni ya kuchapisha yaani copy na siyo kadi original.
Ufafanuzi ~ DC wa Tarime, Meja Gowele: Mwananchi anayepata changamoto Kituo cha Afya Nyangoto atoe taarifa mapema
Pia soma ~ Naibu Waziri wa Afya- Dkt. Florence: Wajawazito wapate huduma za afya bila kikwazo cha fedha