Wajerumani wananufaika na Mjusi wetu

Wajerumani wananufaika na Mjusi wetu

Gordian Anduru

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2021
Posts
369
Reaction score
747
MJUSI WETU

Mwaka 1909 hadi 1913 watu 500 hukoTendaguru Lindi walihusika kufukua mabaki ya mifupa ya kiumbe mkubwa sana. Mifupa hiyo ilikuwa na uzito wa kilo 250,000 ilichukuliwa na kusafirishwa kwenda nchini Ujerumani ambapo iliunganishwa na kupatikana kiumbe kamili ambacho kilikuwa na urefu wa kwenda juu mita 13 kiasi cha watu sita na urefu wa ardhini mita 22 (kiasi cha urefu wa watu kumi)

wajerumani wanaendelea kummiliki mjusi wetu na kupata pesa nyingi kutoka kwa watalii.

Mifupa halisi imehifadhiwa Berlin Museum of Natural History huko Ujerumani

Pichani ni mfano wa mjusi mkubwa aitwae Dinasour akiwa ametengenezwa kwa mabaki ya chuma Makumbusho Jijini Dar es Salaam na Mabaki ya Dinasour wetu huko Ujerumani

mjusi3.jpg

mjusi1.jpg
 
Wakati huo watu wanalalia ngozi na kukimbizana na sungura maporini. Nani angejali kuhusu mifupa ya mnyama na kuitunza mpaka leo? Marangapi nyangumi anakutwa ufukweni amekufa raia wanawahi mifupa kwa ajili ya imani za kishirikina?
 
Watu Hadi wamemuunganisha kabisa na mifupa ikasimama kabisa...vivutio vyenyewe nyumbani vimetushinda tayar, tuboreshe tulivyonavyo Kwanza...
 
Shida ni akiletwa huku gharama za kumtunza ni kubwa mno, waache wanufaike tu.
Sawa bro, lakini na sisi tulimhifadhi (japokuwa tulikuwa hatujui) kwa namna moja au nyingine na watu wetu 500 kwa miaka 4 walitoa jasho lao/walichangia nguvu kazi kufukua mjusi/dude huyo na pia Inawezekana malipo kwa wachimbaji husika hayakuwa halali.
Basi walao kama kifuta jasho, watugawie ka% fulani hv. kati ya kile kinachopatikana kwa utalii huo kuliko tukose kabisa. Au unasemaje Bro.? Tufungue kesi?
 
ULITAKAJE?NYIE NA WATALAAM WENU
MNGEWEZA KUUMUNGANISHA HILO JUSI

ova
 
Bora ilae hukohuko ikija huku ikija huku kuna wapumbavu watasema mjusi wa ccm
 
Kwa nini tusigawane hizo tozo
Wananchi tupumue na tozo za miamala
 
Sawa bro, lakini na sisi tulimhifadhi (japokuwa tulikuwa hatujui) kwa namna moja au nyingine na watu wetu 500 kwa miaka 4 walitoa jasho lao/walichangia nguvu kazi kufukua mjusi/dude huyo na pia Inawezekana malipo kwa wachimbaji husika hayakuwa halali.
Basi walao kama kifuta jasho, watugawie ka% fulani hv. kati ya kile kinachopatikana kwa utalii huo kuliko tukose kabisa. Au unasemaje Bro.? Tufungue kesi?
Hapo mwisho ndo umefiria vizuri
 
Ni kweli! Nadhani Serikali yetu izungumze na Serikali ya Ujeruman kuona kama angalau wanaweza kutupa 30% ya faida wanayopata!
 
Back
Top Bottom