Wajerumani wapiga kura leo kuanza mchakato wa kumtafuta mrithi wa Angela Merkel

Wajerumani wapiga kura leo kuanza mchakato wa kumtafuta mrithi wa Angela Merkel

Kasomi TV

New Member
Joined
Apr 22, 2021
Posts
1
Reaction score
7
Kinyang'anyiro cha kuamua ni nani atakayemrithi Kansela wa Ujerumani, maarufu na ambaye amehudumu kwa muda mrefu zaidi Angela Merkel kinaweza kuwa kikali huku Wajerumani wakianza uchaguzi wa wabunge hii leo.

Mitaa ya Mji mkuu Berlin inakaribisha mashindano yam bio za marathoni za mwaka , lakini mpambano mkuu wa uchaguzi unafanyika kote nchini Ujerumani.

Katika hatua za mwisho za kuwashawishi watu kupiga kura, Kansela anayeondoka madarakani alijiunga na mgombea kutoka chama cha conservative Armin Laschet katika mkutano wa kisasa Jumamosi katika mji wa kwao wa Aachen.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi Jumapili, na vituo hivyo vinatarajiwa kufungwa sa kumi na mbili jioni.

Uchaguzi haukutabirika hadi pale Bi Merke alipoingia katika cheo cha juu kabisa cha kisiasa cha Ujerumani ambapo muda wake unafikia ukingoni.

"Suala la nani yuko mamlakani muhimu kusema ukweli," aliwaonya wapiga kura mara mbili katika kipindi cha saa 48 kabla ya uchaguzi kuanza. Ujumbe wake ulikuwa kwamba Ujerumani inahitaji utulivu na hali yake ya baadaye inawahijtaji vijana - na ni Armin Laschet ndiye mtu atakayewapatia hilo.

Ubashiri wote haukuwa sahihi

Kuna mambo mengi ambayo sio ya uhakika kuhusu uchaguzi huu. Katika awamu ya kwanza zaidi ya robo tatu ya wapigakura hawakuw ana uhakika ni nani wa kumpigia kura, ingawa tayari idadi kubwa ya wapiga kura wamepiga kura zao.

Kwa miezi kadhaa kura za maoni zimekuwa zikitoa matokeo tfauti, Chama cha Wahafidhina cha CDU na washirika wake wa chama cha Bavaria awali viliongoza kwa kura za maoni na wakati mmoja kile cha kijani- Green, kiliongoza, lakini baadaye kile cha Social Democrats cha Olaf Scholz kikaongoza.

Chanzo: BBC
 
Hivi sisi huku tunafanya uchaguzi wa nini, tungekuwa na akili hata kidogo tu tungewaomba hawa jamaa warudi watutawale, tusingekuwa hivi tulivyo. Heri mkoloni mweupe kuliko mweusi.
 
Hawa wakoloni wetu weusi ni tabu sana dhuluma kwa kwenda mbele tena ni wakatili kuliko hata wakoloni weupe.
Kweli sisi watu wenye rangi kama yangu hua hatupo timamo kwenye mambo mengine.
 
Chaguzi za ulaya nyingi ni kama unaendesha gari automatic kwenye barabara nzuri huhitaji nguvu kubwa kama huku twetu utafikiri unaendesha Fiat tena kwenye rafu road
 
Chaguzi za ulaya nyingi ni kama unaendesha gari automatic kwenye barabara nzuri huhitaji nguvu kubwa kama huku twetu utafikiri unaendesha Fiat tena kwenye rafu road
Naona mpaka wivu hakuna bongo fleva majukwaani wala ngonjera unatoa hoja na akishindwa mtu kimyaa wala hakuna kelele hawa jamaa wako miaka 200 mbele yetu mpaka matokeo hakuna mtu kajimilikisha lazima utaungana na wenzako kuongoza maana hakuna wa kukubaliwa na wote tofauti ya viti ndogo sana kikubwa amani anayeshinda na kushindwa. ehh Mungu tumekukosea nini sisi hata kuchaguana hatujui fujo tu na matusi...
 
Ila haka kabibi kamekaa Yan tokea nikiwa primary nasikiliza DW mpaka Leo democracy n somo pana Sana
 
Ila haka kabibi kamekaa Yan tokea nikiwa primary nasikiliza DW mpaka Leo democracy n somo pana Sana
Mimi hata Kabula sijazaliwa nakasikia hadi leo nina mke na watoto.
Mwanzo nilifikiri nchi hiyo ni yake
 
Back
Top Bottom