cheusimangala_
Senior Member
- Dec 1, 2018
- 114
- 177
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalinda Haki za Binadamu za kila mtu katika nchi hii. Hii inajumuisha haki ya kupiga kura, uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika.
Chaguzi ni moja ya misingi muhimu ya demokrasia. Wananchi wote bila ubaguzi wana haki ya kuamua na kuchagua viongozi na wawakilishi wao katika vyombo mbalimbali vya serikali. Hii hufanyika kupitia kampeni za uchaguzi ambapo vyama vya siasa hunadi mipango na ajenda zao kwa wapiga kura. Kwa kupiga kura wananchi wanachagua miongoni mwa vyama vinavyoshindana viongozi kulingana na mipango na ajenda zao. Katika uchaguzi ulio huru na haki matokeo ya uchaguzi huakisi dhamira ya wapiga kura kama walivyotekeleza kupitia haki yao ya kupiga kura bila ya ubaguzi, vitisho, matusi, fujo au unyanyasaji wa kingono au kijinsia.
Maafisa wa polisi wana wajibu muhimu sana wakati wa uchaguzi. Wana jukumu muhimu la kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa huru na haki na bila vurugu wala vitisho na kuzingatia demokrasia.
Kwa kuongezea:-
Wajibu wa jumla wa polisi ni kama ifuatavyo:-
➣ Kudumisha utulivu na kuhakikisha utii wa sheria katika mchakato wote wa uchaguzi.
➣ Kuhakikisha usalama wa watu na mali zao katika kipindi cha kampeni na uchaguzi.
➣ Kuhakikisha usalama wa wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wao kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
➣ Kutoa ulinzi kwa wagombea wakati wa kampeni na uchaguzi.
➣ Kuhakikiisha kwamba kampeni zinafanyika kwa amani.
➣ Kuhakikisha mazingira wezeshi kwa uchaguzi ulio huru na haki, utii wa sheria na kanuni bila ubaguzi wa aina yoyote.
➣ Kuhakikisha usalama wa vituo vya kupigia kura.
➣ Kuhakikisha ulinzi na usalama wa vifaa vya kupigia kura katika vituo vya kupigia kura, wakati wa kupiga kura, wakati wa kuhesabu kura na usafirishaji wa masanduku ya kura.
➣ Kuhakikisha kwamba wapiga kura hawatishwi au kusumbuliwa katika vituo vya kupigia kura.
➣ Kuhakikisha kuwa hakuna mtu mwingine anayeruhusiwa kuwa katika eneo la kupigia kura isipokuwa wapiga kura tu. Mtu mwingine hataruhusiwa kuwepo isipokuwa kwa idhini ya Tume ya Uchaguzi.
➣ Kuhakikisha amani na usalama kabla, kipindi cha ucahguzi na baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
Kumbuka:-
Polisi wanapotekeleza majukumu haya wanatakiwa kuzingatia maadili, kuheshimu haki za binadamu na kuepuka matumizi makubwa ya nguvu yasiyokuwa ya lazima.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakataza polisi kuwa wanachama wa vyama vya siasa.
Haki za binadamu katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zillingizwa mwaka 1984 na zinatoa haki za kidemokrasia kama vile:
➣ Uhuru wa kujieleza,
➣ Uhuru wa kuabudu na fikra,
➣ Uhuru wa kujumuika,
➣ Uhuru dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote, n.k