Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Kanisa lililoanzishwa na Mungu msingi wake ni kuomba ili kutawala maamuzi yote katika ulimwengu wa roho kabla hayajatokea kama majibu katika ulimwengu wa mwili.
Mwakasege (2013,uk.88) katika kitabu cha Ujue Ulimwengu wa Roho Ili Kufanikiwa Katika Maombi Yako alisema "Dalili ya Kanisa lisiloomba ni kulalamika na kunungu'nika, aliongezea kusema Kanisa linaloomba huwa halilalamiki. Ukiona mtu anaulalamikia uongozi uliopo juu yake ujue hauombei".
Unapookoka hauishii kupata uhalali wa kuitwa mtoto wa Mungu tu ila unapata uhalali wa kutawala kwa njia ya maombi mahali ulipo.
Kanisa linapaswa kutawala maamuzi kwa njia ya maombi bila kujali hali ilivyo.
Mwakasege (2013, uk.89) alifafanua zaidi kuwa "haijalishi uongozi uliopo juu yako, unaupenda au huupendi unachotakiwa kufanya ni kuuombea.
Yeremia 29:7 kama alivyoinukuu (Mwakasege, 2013, UK.89)."Kautakieni amani mji ule ambao nimewafanya mchukuliwe mateka mkauombee kwa Bwana; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani".