Wajibu wa kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu

Wajibu wa kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
234
Reaction score
376
Ni takwa la kisheria kwamba kila mwajiri katika sekta binafsi au sekta za umma kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu pale ambapo mtu huyo mwenye ulemavu ameomba nafasi hiyo na ana vigezo vinavyohitajika katika kazi husika sawa na watu wengine wasio na ulemavu.

Kila Mwajiri mwenye uwezo wa kuajiri watu ishirini au zaidi anatakiwa kuajiri na watu wenye ulemavu. Asilimia tatu ya wafanyakazi hao ni lazima ijumuishe watu wenye ulemavu.

Mwajiri anatakiwa kuhakikisha kwamba anaajiri na watu wenye ulemavu isipokuwa tu kama atathibitisha mambo yafuatayo;
(a) Baada ya kufanya jitihada zinazostahili ameshindwa kupata mtu mwenye ulemavu mwenye vigezo vya kufanya kazi hiyo.

(b) Kulingana na aina ya kazi hiyo, hakupata mtu mwenye ulemavu mwenye ujuzi au uzoefu unaohitajika kwa kazi hiyo.

(c) Kulingana na aina ya kazi au mazingira ya kazi isingekuwa rahisi kumwajiri mtu huyo mwenye ulemavu aliyeomba nafasi hiyo.

(d) kwa kuzingatia hali ya mtu mwenye ulemavu aliyeomba nafasi hiyo hasingeweza kufanya kazi hiyo vizuri kama inavyohitajika.

Kila mwajiri ni lazima azingatie usalama na ustawi bora kwa watu wenye ulemavu wawapo kazini kwani mwisho wa siku anatakiwa kupeleka ripoti ya kila mwaka kwa Kamishna kuhusiana na hali ya kazi ya watu wenye ulemavu katika ofisi au taasisi yake.

Mwajiri anatakiwa kutambua kwamba haki ya kufanya kazi ni haki ya msingi ya kila mtu, pasipo kujali ulemavu wa mtu huyo.

Ubaguzi wa aina yoyote hauruhusiwi. Hivyo, ajira zitolewe kulingana na uwezo wa mtu wa kufanya kazi na kila mtu anatakiwa kupata ujira kulingana na kiasi na sifa ya kazi wanayoifanya.

NB:
Itamburike kwamba, watu wote ni sawa mbele ya sheria na watu wote wana haki ya kufanya kazi, hivyo ulemavu usiwe sababu ya kumnyima mtu kazi au kumpa malipo kidogo tofauti na wafanyakazi wengine.

(rejea kusoma - kifungu cha 31 na 32 cha sheria ya Watu wenye ulemavu, kifungu cha 7 cha sheria ya Ajira na Mahusiano kazini pamoja na ibara ya 22 na 23 ya Katiba ya Tanzania.)

Imeandaliwa na:
Mr. George Francis
0713736006

Join us
Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓

Facebook: TANZANIA LAWYERS FORUM | Facebook
 
Back
Top Bottom