Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Kuwajibika ni wajibu wa kila mtu na siyo watu fulani tu kama wengi tunavyodhani. Hakuna anayepaswa kuacha kuwajibika kwa sababu kila mmoja wetu anao wajibu huo.
Suala la kuwajibika si la viongozi tu ila baki na wanaoongozwa pia. Jamii au mtu mmojammoja anaweza kufikia malengo yake ikiwa itazingatia uwajibikaji.
Kuwajibika kunamfanya mtu kujiona anajambo la kufanya katika Umma unaomzunguka hovyo, kumfanya mtu kujiona mwenye kusudi analopaswa kulisimamia kikamilifu kwa sababu linamhudu.
Uwajibikaji unabeba dhana nzima ya ushirikishwaji na kuthaminiana. Mahali popote penye uwajibikaji duni pana ushirikishwaji dhaifu kwa sababu ushiriki unaambatana na uwajibikaji. Tunashiriki ili kuwajibika katika nafasi mbalimbali na tunawajibika kuonesha ushiriki wetu.