Li ngunda ngali
JF-Expert Member
- Jun 22, 2023
- 707
- 2,572
Kijana, shtuka!
Apaswayo kuyafanya mzazi wako anapokuzaa ni mambo mawili pekee, nayo ni; kukulea ( ki-maadili), kuhakikisha unapata chakula ( kwa umri komo) na kuhakikisha unapata elimu ( kama una akili hiyo).
Vinginevyo, mali za baba yako siyo zako. Na, anaweza kutokukupa urithi akiamua na huwezi kumfanya chochote! Jamaa anaweza kuamua ampe urithi mbwa, nyau, chura na hata Taasisi kama, Vituo vya Afya, Magereza ama CHADEMA na msimfanye kitu. Hata akiamua kubomoa nyumba aliyoijenga mwenyewe, anaweza.
Funzo;
Vijana, acheni kujikunyata kwenye mapaja ya mama zenu jikoni huko, huku mkibembeleza 5k ya kwenda kutesea mtaani kila jioni. Tambueni, wajibu pekee wa mzazi wako ni huo hapo juu.