Wajibu wa ndugu kutoa msaada wa kijamii kwa watu wenye ulemavu

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
234
Reaction score
376
Ndugu wana wajibu wa kutoa msaada wa kijamii kwa watu wenye ulemavu.

Kama kuna ndugu zaidi ya mmoja wa mtu mwenye ulemavu, ndugu hao kwa kushirikiana pamoja wanatakiwa kutoa msaada wa kijamii kwa mtu huyo mwenye ulemavu. Mfano: makazi, chakula, elimu, afya, maji au mavazi nk. kama miongoni mwa mahitaji muhimu ya kijamii ambayo kila mtu kwenye jamii anapaswa kuyapata.

Kushindwa kutoa msaada wa kijamii unaostahili kwa mtu mwenye ulemavu, Mahakama kwa maombi ya mtu mwenye ulemavu au mwakilishi wake itamwamuru ndugu huyo kutoa malipo ya kila mwezi kwa kiwango cha fedha ambacho Mahakama itaona inafaa.

Mahakama, wakati wowote inaweza kubaditilisha au kuondoa amri hiyo ya malipo ya kila mwezi kutokana na sababu zikazoifanya mahakama kufikia maamuzi hayo.

Mtu mwenye ulemavu au mwakikishi anaweza kupeleka maombi Mahakamani ili kuwataka ndugu watoe msaada wa kijamii kwake na hii ni kwa mujibu wa sheria.

(rejea kusoma vifungu vya 16 na 17 vya sheria ya Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2010)

NB:
Katika zama hizi tulizonazo, tunaamini watu wenye ulemavu ni watu wenye uwezo mkubwa na hawana tofauti na watu ambao hawana ulemavu.

Hivyo kulingana na mada hii, ndugu wa watu wenye ulemavu tunapaswa kutengeneza mazingira mazuri ili watu wenye ulemavu waweze kupata mahitaji yao muhimu pasipo kutegemea misaada kutoka kwa watu wengine kila wakati.

Imeandaliwa na:
Mr. George Francis
0713736006

Join us

Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓

Facebook: TANZANIA LAWYERS FORUM | Facebook
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…