Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 376
WAJIBU WA SERIKALI ZA MITAA KUWALINDA WATU WENYE ULEMAVU.
Leo napenda kuelezea wajibu wa serikali za mitaa katika kuwalinda watu wenye ulemavu.
Mamlaka ya serikali za mitaa ina wajibu wa kulinda na kukuza haki na ustawi wa watu wenye ulemavu katika eneo lake.
Jukumu hili linatekelezwa na maafisa ustawi wa jamii katika eneo hilo la kimamlaka. Afisa utawi wa jamii katika kutekeleza majukumu yake anatakiwa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao pamoja na kulinda ustawi wao.
Maafisa ustawi wa jamii wanaweza kutekeleza jukumu la kulinda haki na ustawi wa watu wenye ulemavu kwa kusaidiwa na maafisa wengine wa serikali za mitaa, kama vile wenyeviti wa mitaa, watendaji na wafanyakazi wengine wa mamlaka husika za serikali za mtaa.
Facebook: TANZANIA LAWYERS FORUM | Facebook
Miongoni mwa majukumu ya afisa ustawi wa jamii katika mamlaka ya serikali za mitaa ni kutoa ushauri kwa wazazi, walezi, ndugu, jamii na watu wenye ulemavu kwa lengo la kupunguza au kuondoa ubaguzi na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu katika jamii.
Mamlaka ya serikali za mitaa inatakiwa kuwawezesha watu wenye ulemavu ili waweze kukuza uwezo wao na waweze kujitegemea wenyewe.
Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓
Hivyo, ni jukumu la serikali za mitaa kuandaa mazingira wezeshi au mazingira rafiki ili watu wenye ulemavu waweze kufanya kazi zao au kuzifikia huduma za msingi bila kikwazo chochote cha kimazingira.
Mfano; kuhakikisha maeneo ya masoko yanafikika kirahisi ili kuwezesha watu wenye ulemavu kufanya biashara au kununua bidhaa bila shida yoyote.
Mamlaka ya serikali za mitaa ina wajibu wa kuhakikisha katika eneo lake la kimamlaka kuna mazingira rafiki kwa watu wote kupata huduma zao bila tatizo.
Mfano; kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa uhakika katika mabomba ya karibu ili kuwaondolea usumbufu watu kufuata huduma hiyo maeneo ya mbali jambo ambalo linaweza kuleta shida zaidi kwa watu wenye ulemavu.
Mamlaka ya serikali za mitaa inatakiwa kufuatilia na kutambua idadi ya watu wenye ulemavu katika eneo lake la kimamlaka.
Mamlaka hiyo inapaswa sio tu kufahamu idadi bali pia na aina ya ulemavu na changamoto zinazowakabili kisha kutunza taarifa hizo na kuzipeleka kwa Kamishna wa ustawi wa jamii ili kupanga namna nzuri ya kuwawezesha watu hao wenye ulemavu.
NB: Mamlaka ya serikali za mitaa, Maafisa ustawi wa jamii na viongozi wengine wa selikali za mitaa ni muhimu kutambua majukumu yao katika kulinda na kukuza haki na ustawi kwa watu wenye ulemavu. Mtu yoyote hasinyimwe haki zake kwa kigezo cha ulemavu wake.
(rejea kusoma kifungu cha 20 cha Sheria ya Watu wenye Ulemavu ya mwaka 2010).
Imeandaliwa na:
Mr. George Francis
0713736006
LIKE, COMMENT & SHARE
__________________
TUZIKUMBUSHE MAMLAKA ZA SERIKALI ZETU ZA MITAA KUTEKELEZA MAJUKUMU HAYA MUHIMU.