Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,628
- 6,411
Ualimu ni taaluma yenye mawanda na matao mapana sana huenda kuliko taaluma nyingine nyingi zilizopo.
Mwalimu licha ya kuwajibika kwa taaluma yake, wateja wake (wanafunzi), mwajiri wake, bado anao wajibu pia kwa jamii inayomzunguka na kwa Taifa lake kwa ujumla.
Mwalimu anapaswa kuwa mtoa maarifa na mpokea maarifa mpya kila wakati ili kusaidia jamii pana juu ya masuala mbalimbali.
Likizo hii ya kusimama kwa vipindi kwa muda haimaanishi Mwalimu abweteke ila inamtaka kuwajibika kuisaidia jamii yake kwa kujifunza maarifa mapya hususani juu ya kujiunga na kujihami na ugonjwa wa COVID-19 na kuisaidia jamii yake kwa kuielewesha kwa namna ya karibu zaidi.
Walimu katika Taifa hili tunapaswa kushirikiana na Serikali bega kwa began katika kuelimisha jamii zetu zinazotuzunguka hasahasa vijijini.
Licha ya uwepo wa wataalamu wa afya ambao nao wanatoa elimu hii pia lakini kama kila Mwalimu aliyepo kijijini akielimisha kinaganaga watu wanaomzunguka nina uhakika vijiji vyetu havitaathirika sana.
Vijijini licha ya vyombo vya habari kutoa elimu nzuri, lucha ya Serikali za mitaa kuchukua hatua za tahadhari bado elimu ya kuiamsha jamii ili kujihami inahitaji ushirikiano mkubwa wa wadau wengi zaidi ya tunavyofikiri.
Mwalimu usijifiche ndani na familia yako kijijini taaluma ya ualimu inayotaka kuwajibika moja kwa moja kuisaidia jamii. Itapendeza sana tukielimisha familia zetu na pia tukaelimisha wanaotuzunguka.
...........................