John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Wajibu wa Waumini Kuhudumia na Kuwategemeza Watumishi wa Mungu
Utumishi wa Mungu ni Nini
Utumishi ni hali ya kutii na kuitumikia mamlaka au mtu mwenye mamlaka fulani na ambaye unamwamini na kumtegemea. Katika muktadha huu tunakuta kuna watumishi wa aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na utumishi wa umma, utumishi binafsi na utumishi wa mashirika. Hapa tunazungumzia utumishi wa Mungu. Yaani, msaada uliotolewa au kazi iliyofanywa kwa manufaa ya Mungu na wengine. Tunapowatumikia wengine, tunamtumikia pia Mungu. Chagueni hivi leo mtakayemtumikia (Yoshua 24:15). Utumishi wa Mungu huelezea uhusiano kati ya watu na Mungu.
Neno la Mungu linasema; “Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu. Kila mtu anayempenda mzazi, humpenda pia mtoto wa huyo mzazi. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda Watoto wa Mungu; Kwa kumpenda Mungu na kuzitii amri zake; maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na amri zake si ngumu, maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu” (1Yoh 5:1-3).
Somo hili litasaidia kukabiliana na wimbi wa habari ya utumishi wa Mungu na sadaka na matoleo, na kuona sababu ya upotofu mwingi uliopo miongoni mwa waaminio, kuwa ni kutokana na kiwango cha ufahamu wa KiMungu katika kulielewa suala hili.
Huduma muhimu zinazotolewa na watumishi wa Mungu
Neno la Mungu linasema; “Mavuno ni mengi lakini watenda kazi (mimi na wewe) ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake”. (Luk. 10:2). Katika kila hali uliyo nayo, unapaswa kumtumikia Mungu. Kama, yumkini unao udhaifu, Mungu anaujua. Utumishi wetu siyo kwamba wote tuwe wachungaji, au wainjilisti bali sisi tunao mchango katika sehemu yetu kuhakikisha agizo la Mungu linatimia.
Kuhusu karama za rohoni. Mwingine AMEPEWA neno la hekima, mwingine neno la maarifa, mwingine imani, mwingine karama za kuponya, mwingine matendo ya miujiza, mwingine unabii, mwingine kupambanua roho na mwingine aina za lugha, na mwingine tafsiri ya lugha. Lakini Roho ni yule yule (1Kor 12:4-11). Ndiyo maana utakuta wengine ni mitume na wengine manabii na wengine wainjilisti, wengine wachungaji na wengine pia ni walimu. (Waefeso 4:11). Wengine wanaweza kuwa waimbaji wazuri, wengine watoaji wazuri, wengine wanamaombi, wahudumu kanisani, mashemasi, wafanya usafi makanisani na nyumba za makuhani wetu. Yote hayo ni ili kila mmoja apate sehemu ya kumtumikia Mungu.
Katika utoaji wa huduma za kiroho, kabla ya Kristo kuja duniani, mifano ya VITU vilivyotumika ni kama ifuatavyo: maji ya mto Yordani yalijitenga pande mbili baada ya Musa kuinua FIMBO (Kutoka14:21), Musa aliponya maji kwa kutupia KIJITI (Kutoka 15:25), Elisha alitupa CHUMVI kwenye maji kuponya mapooza (2Wafalme 2:19-25), Elisha alimponya ukoma Naaman kwa kutumia MAJI ya mto Yordani (2Wafalme 5:1-19), Elisha alitupa KIJITI kwenye mto Yordani na shoka lililokuwa limetumbukia likaelea na kuokotwa na wakata miti (2Wafalme 6:6). Nguvu ya MAJI inaonekana pia katika Yohana 5:2-8, Ufunuo 11: 6 na Ezekiel 36:25. Nguvu ya MAFUTA inaonekana kwenye Waamuzi 9:8-9 na nguvu ya CHUMVI kwenye Waamuzi 9:45.
Maandiko katika biblia, yanataja VITU mbalimbali vilivyotumiwa na Yesu katika uponyaji. Njia hizo ni pamoja na MATE (Marko 7:33-35, Marko 8:22-26, Yohana 9:6-7), NGUO (Luka 8:43-48, Marko 6:56), UDONGO/TOPE (Yohana 9:6-7) na MAJI (Yohana 9:7).
VITU walivyotumia mitume wake kwa kuponya na kutoa mapepo ni pamoja na NGUO (Mitume 19:11-12) na MAFUTA (Marko 6:13, Yakobo 5:14-15, 2Wakorintho 1:21, 1Yohana 2:20, 27).
Katika kipindi cha sasa pia, njia mbalimbali zimeendelea kutumiwa na watumishi wa Mungu katika utoaji wa huduma mbalimbali za kiroho. Katika kutekeleza agizo la Yesu (Mathayo 10:1-10), kwenye biblia, kuna ushuhuda mwingi wa kuponya kwa njia ya VITU. Ni muhimu kwa watu KUPITIA BIBLIA YOTE, na kutambua vitabu na aya zake, zinazotamka matumizi ya vifaa mbalimbali vya kiroho katika utoaji wa huduma za kiroho, ili kuinua uelewa wa maandiko katika jambo hili.
Mungu Yehova ni tajiri wa mbinu. Hakuna njia moja pekee inayotumika katika uponyaji na utoaji wa mapepo, na mambo mengine. Njia sahihi ni ile inayoangaziwa na Roho Mtakatifu, kwa mtumishi wa Mungu. Yote yanafanyika KWA IMANI katika Mungu.
Kuhudumia na kuwategemeza watumishi wa Mungu
Andiko linawakumbusha na kuwaagiza waumini kuwashirikisha watumishi wa Mungu wanaowahudumia katika kuwahutubu na kuwafundisha katika mema yote.
Katika 1Timotheo 5:17-18:
17 “Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. 18 Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi anastahili ujira wake”. Hawa wazee ni viongozi wa makanisa na wanakuwa kwenye mojawapo ya zile huduma tano za Mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji na Walimu.
Katika Mathayo 10:1-10:
Katika Mathayo 10:1, imeandikwa Mungu aliwapa mitume wake mamlaka ya kuponya magonjwa yote. Hakusema niombeni nije kuponya. Hii ina maana kuwa yeye amewapa watumishi wa Mungu uponyaji ili wao wawaponye watu.
5 Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. 6 Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. 8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure. 9 Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu; 10 wala mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo; maana mtenda kazi astahili posho lake.
Katika Luka 8:1-3:
Tunamwona hata Yesu alihudumiwa na wale ambao huduma yake iliwagusa
1 Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye, 2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, 3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana mke wa Yoakimu, na wengine wengi, waliokuwa_wakimhudumia kwa mali zao.
Ni wazi kabisa Mungu anatuwajibisha waumini katika kuwategemeza kifedha hata na mali, watumishi wake, hasa wale wajitaabishao katika kuhutubu na kufundisha.
Wapo watumishi wa Mungu wameweka kambi katika nchi za hatari sana, wengine wanakamatwa wanafungwa; wengine wananyongwa, wanachomwa, wanapigwa mawe hadi kifo, sisi tupo salama na tunaishi vyema sana. Tunasoma kwa habari ya Petro Simon mwanafunzi kindakindaki wa Yesu Kristo alipofungwa na Herode ili kuuawa, ni maombi ya watakatifu ndiyo yalimtoa katika kile kifungo, hata wakati wangalipo kukesha wanaomba, ndipo Petro akajidhihirisha kwao kwamba ametoka salama (Matendo ya Mitume 12:1-17).
Siyo kitu rahisi sana watumishi kumtumikia Mungu kwa uaminifu na hawalipwi mshahara wowote wala ujira wowote. Wanaishi maisha ya imani ya kumwamini Mungu. Wanajitoa kwa ajili ya watu na kuleta mguso wa KiMungu maishani mwao na kuwapandia vya rohoni. Watu wa Mungu wasipofundishwa vitu kama hivi, wanaweza tu wakaamini kuwa kuna malaika wanatoka mbinguni na kuwaletea yale wanayohitaji kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku na familia zao.
Heshima kwa watumishi wa Mungu
Tunapaswa kuugua pamoja nao, ni wajibu wetu kuwaombea kwa kufunga na kukesha ili kazi wanayoifanya iwe na ushirika wetu kiroho; waifanye kwa ushindi, tunapaswa kuwategemeza katika maombi. Neno la Mungu linasema; “kwa sala zote na maombi, mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha katika jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi, kwa kufumbua kinywa change, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya injili” (Waefeso 6:18-19).
Biblia katika 1Wathesalonike 5:12-14, inasema; “Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na Amani ninyi kwa ninyi. Ndugu, tunawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote”.
Tuelewe kwamba heshima anayopatiwa mtumishi wa Mungu ndiyo sababu maneno yake, ujumbe wake na baraka anazotoa, hubakia kwako wewe. Yesu alisema katika Mathayo 10:40, “Awapokeaye ninyi, anipokea mimi, naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma”. Hivyo, kuwa mwepesi kujua kwamba pale unapomuheshimu mtumishi wa Mungu, haumfanyii mwanadamu, bali unamfanyia Bwana.
1Yohana 5:1 inasema, “Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto w Mungu. Kila mtu anayempenda mzazi, humpenda pia mtoto wa huyo mzazi”. Kama unampenda Yesu, utawapenda wao anaowatuma. Usiungane na wenye kebehi na mizaha kuwateta na kuwachukia wale Mungu aliowatuma kukubariki na kukukuza katika Neno.
Waebrania 13:17 inasema, “Watiini wale wanaoongoza kati yenu na kuwanyenyekea, maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi”.
Maneno ya watumishi wa Mungu, ujumbe wao na baraka wanazotoa, hubakia kwako wewe. Hivyo, ni vizuri kuwaheshimu, kuwatia moyo. Pia, ni vizuri kuwahudumia na kuwategemeza watumishi wa Mungu kulingana na taratibu zilizowekwa na kanisa.