Wajua japo Rais ni sehemu ya Bunge, bado hana mamlaka ya kuliingilia Bunge? Ili kufuta IGA ya DPW, Rais anapaswa kulivunja Bunge?

Kuna kuzungumza vile tunahisi na kuna kuzungumza vile ilivyo....umeandika hisia sana. Hilo ni Bunge la JMT tuombe Bunge liamue kufuta azimio lake lenyewe.
 
Mkuu nashukuru kwa uchambuzi wako! Na mimi nimegundua ni miongoni mwa wasioijua Katiba!
Nataka kuwaza kwa kuwa Bunge lilivunja Katiba wakati wa kuupitisha Mswaada wa Mkataba huo,na Rais tena akausaini kinyume na Katiba,basi kama hakutakuwa na athari nadhani Rais anaweza kuuvunja Kinyume na Katiba! Harafu tuanze upya.
 
Kwani si tuliambiwa IGA ni non-binding ila HGA ndio binding? Na kwamba hatuwezi kushtakiwa kwa kuvunja IGA bali HGA? Sasa haya ya kuvunja bunge yanakujaje wandugu zangu, kama bado hatuna kesi na Waarabu?
 
Paskali wewe unafiki hautakuisha Kamwe ktk maandiko yako kwani unatanguliza kusaka fursa kuliko ukweli halisi.

1. Unasema TEC haikukusanya maoni ya Wananchi, je twambie ni ushirikishwaji gani uliofanywa na serikali hadi kusaini mkataba kwa siri hata kabla ya muda. Na kasoro hii imethibitishwa ktk hukumu iliyotolewa Mbeya. Je hili ulilipigia kelele kama unavyotaka kutuhadaa?

2. Hapa umekubali kuwa Pr Shivji ni Mwl mzuri aliyekufundisha sheria lakini huyohuyo aliishauri serikali hii kurekebisha kasoro kabla ya azimio la bunge wewe ukashabikia ukiwa upande wa serikali na leo unasema haitawezekana kwa kuwa tayari azimio limepitishwa. Huu ni unafiki wa kiwango cha juu.

3. Unakubali kuwa pale hakuna bunge kwa maana ya mambumbu wengi kutojua kanuni, sheria na katiba kwamba sasa mambo mengi yamekuwa yakisigina taratibu za kikanuni na hata katiba, kama ndivyo unashangaa nini kusema kwamba TEC wameshauri kisichowezekana. Huu ni unafiki na undumulakuwili.

4. Unahoji kuwa TEC wanachanganya siasa na dini ni lini uliwahi kukemea Rais, makamu wa Rais, waziri mkuu au kiongozi pale ambapo mara nyingi hutumia majukwaa ya makanisa na misikiti kuomba kuungwa mkono ktk mambo yao? Kama ndivyo kwa nini wasiache kupanda ktk majukwaa ya makanisa na misikiti kupeleka jumbe zao ila watumie majukwaa yao ya kisiasa tu. Wakipongeza mnaona Safi wakikosoa wasichotaka ni kuchanganya dini na suasa. Hii ni hadaa.

Mwisho tafuta fursa kwa haki na siyo unaaa.
 
Hapo walikosea sana wameonesha interest yao mapema....wangeanza na Huduma za kijamii kama hospital,shule nk
 
Din na siasa Nini,,si vyote vinaongozaa watu,,watu na watu ndio walio chaguana kuongozana ukichaguliwa na watu hutakuwi kuwapingaa inatakiwaa uwaskizee walicho kutumaa ,,Mimi naona Bora tutawaliwe Tena akili zitukae sawaa Hadi Burundi wanatushinda kufikiri binafsi sijaona msomi tanzania hii wa kumsikizaa hawasaidii taifaa walevi ndio wanapambania nchi Yao ili watawaliwe na wasomii shame
 
Rubbish
 
Hivi ndg msomi wa katiba Kuna tofauti gani kati ya mkataba uliopitishwa na Bunge na miswada inayopelekwa bungeni baada ya kupitisha na Bunge Rais anapelekewa kuisani?
Muswada wa sheria unapopelekwa Bungeni na Bunge kutunga kuwa sheria, baada ya Bunge kuitunga sheria hiyo haiwezi kuwa sheria mpaka kwanza rais aridhie kwa kuisaini. Rais anaweza kusaini ama asisaini. Asipo saini, anarudisha Bungeni na marekebisho rais anayoyataka, Bunge linarekebisha, rais anasaini. Bunge likigoma kurekebisha, linamrudishia rais, rais analivunja Bunge.

Azimio la Bunge ni amri ya kibunge, rais hana mamlaka na Azimio la Bunge, ni amri tuu. Bunge likiishapitisha Azimio la Bunge, ni rais has no room ni kutekeleza tuu!. Ile IGA ni makubaliano tuu, mkataba ni HGA, hivyo there is an ample room ya kupata HGA nzuri japo IGA ni IGA mbovu.
P
 
Kusitisha wasilisho la azimio la Bunge ni sawa na kufuta azimio la Bunge?
Azimio la Bunge halina kusitisha, unless ni Bunge lenyewe likae na kupindua Azimio lake. Rais Samia hana mamlaka kusitisha Azimio la Bunge!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…