Wajua japo Rais ni sehemu ya Bunge, bado hana mamlaka ya kuliingilia Bunge? Ili kufuta IGA ya DPW, Rais anapaswa kulivunja Bunge?

Dini na siasa unazitenga vipi? Lingine, Rostam aliposema mahakama zinapigiwa simu tu zinatoa maamuzi alidanganya? Lingine Bunge lililopo limewekwa na Wananchi? Waliomo bungeni wapo kwa kupita bila kupingwa, kwa maagizo ya utawala. Maaskofu wametimiza wajibu wao.
 
Kama aliweza kumtoa Spika wa Bunge na maisha yakaendelea, akamuongezea Jaji mkuu mda kinyume ba katiba na maisha yapo yanaendelea. Hayo makaratasi ndiyo yamshinde. We mzee nawe unazeeka vibaya ujue!
Huyu jamaa namshangaa, hivi hajui Rais hapa Tanzania ni nusu Mungu? Ndiye anayeamua bunge gani awe nalo, la vyama vingi au Chama KIMOJA, ndiye anayeamua nani awekwe ndani na atoke lini ( Reje Mbowe). Eti katiba, kwa Sasa katiba ni karatasi tu.
 
Huyu jamaa haeleweki, dini na siasa unazitenga vipi? Hebu atupe mfano wa viongozi walioleta dini ni yupi alijitenga na siasa? Kwa Waislamu, Mtume Muhammad alipigana vita vingi, 1. Badri, 2.Uhud, Khandak na Hunayn, je, alichanganya dini na siasa? Yesu alikemea mauvu ya watawala mpaka akasulubiwa, je, alichanganya dini na siasa? Kwa kifupi dini na siasa unazitenga vipi?
 
Kwani kuvunja hilo bunge rubber stamp kuna athari gani, hiki nacho umeona kitu cha maana kukitolea angalizo?
 
Natumaini ulisoma theory za ARISTOTLE ulipokua unapata elimu yako ya sheria na utakumbuka vizuri na unaelewa ya HUMAN BEING IS POLITICAL ANIMAL... naomba majibu ya maswali haya

Ni wakati gani maisha ya mwanadamu hayahusishi/anaishi nje ya siasa

Azimio lililopitishwa na bunge limevunja katiba.. kitendo hiki akihalalishi bunge kuvunjwa?

Mwalimu wa katiba ni wapi katiba yetu imemzuia askofu/mtumishi wa Mungu asijihusishe na siasa

TEC inasimamia masilahi ya waumini wakatoliki wa tanzania hawana haki kutetea haki zao?
 
ukisema maaskofu hawaijui katiba huwatendei haki, wale watu wana weledi wa hali ya juu sana na wanajua jinsi mabo nchi hii yanavyoendeshwa (Ref. kauli ya R A juu ya mahakama zetu!)
 
Pasco huzeeki?
Wakati unaongoza kipindi cha kitimoto nilikuwa mdogo
Leo nimekuwa mtu mzima...upo
Lea wajukuu bana acha uchawa
 
Ulicho andika ni kweli ila unajisahaulisha kuhusu aina ya Bunge tulilo nalo kuwa ni Bunge butu hawajui chochote Raisi ana nguvu ya kimamlaka ya kufanya chochote na hakuna wa kumhoji.
Wanasheria , Majaji wa Serikali hawawezi kushauri chochote masikio na midomo Yao wanaimba pambio za kumtukuza malkia.
Kanisa Catholic TEC wanafahamu muhimili wa Bunge ni nguzo ya manyoya, ndio maana wanahangaika na mhimili wa chuma.
Hakuna mtu anaweza kuhangaika na hili Bunge letu ni kupoteza mda.
 
Mkuu nikupongeze sana kwa elimu kubwa pana nayandani sana uliyoitoa hapa Leo nimekuunga mkono 100% kiukweli kabisa uandishi wako wa Leo umeepuka Kila aina ya "Prejudice " katika kutafsiri Waraka wa TEC kwa kuonyesha Katiba inasemaje katk Tamko lile la Maaskofu

Hivyo basi atakaye kupinga katk bandiko hili huyo atakuwa Yuko "Biased " imma kwa kusukumwa na Imani yake ya dini au Itikadi yake ya kisiasa mkuu Leo umekuwa "Neutral " kitu ambacho waandisho wengi wanashindwa kukizingatia katk uandishi
 
Umeeleza vizuri na umeeleweka japo na wewe umechagua upande.

Huko mwisho hata wewe umekiri hayo makubaliano yana mapungufu lakini umeyabariki yaendelee.

Hii nchi janja janja ni nyingi sana. Serikali huitumiq dini kwenye mambo yao ikiwemo kufikisha huduma za kijamii kwa raia, kwani Pascal Mayalla hayo mambo ya hosp, shule nk si wajibu wa serikali lakini hushirikiana na taasisi za kidini. Pia taarifa za kiserikali mfano ulinzi na usalama pia hutumia madhabahu ya dini kufikisha ujumbe kwa wananchi.

Sasa leo hii ndo kisa hao wanadini wanatoa ushauri basi wasitumie madhabah yao kisa itakua wanachanganya dini na siasa?? Kama serikali inavyowatuma wafikishe habari kwa jamii na wao wametumia njia hiyo hiyo kufikisha habari kwa jamii.

Kwa mimi naamini TEC nao wana yao binafsi, ila hapo kwenye hayo yao binafsi pia nao wana hoja wasikilizwe na wajibiwe hoja zao kukata kiu zao na sio kukimbilia kuwashutumu kwa kigezo cha udini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…