Wakati ndo sasa, hatuwezi kujua kama kamwambia au hakumwambia, mtoa mada kaleta tu kero yake anayoishuhudia, hakuna sababu ya kutake it personal,
nikirudi kwenye mada, upande wangu nimeiangalia kwa macho 2;-
a. Kweli mpiga mizinga ana shida,
kama ulivyosema maisha ni kupanda na kushuka, leo unacho kesho huna, mtu wa namna hii hata akikupiga mzinga unatoa kwa moyo mkunjufu maana unajua mpaka kaniomba kweli kakwama...
Saa nyingine kama mtu hana ajira kwa nini asipige mzinga fedha za biashara? Hata mtaji wa kuuza maji.....
B. Aina ya pili ni wale wapiga mizinga naturare, yaani hata awe na hela mfukoni lazima akupige mzing, hawa ndo wanaokera, hata ukiomwambia haisaidii sana..... Nikupe mfano mmoja kuna mtu akiniona mimi au yoyote katika marafiki lazima akupige mzinga, mpe sasa hiyo hela bila aibu atakwambia naenda saluni.... Yaani mpigwa mizinga yeye hataki kwenda saluni? Na mtu wa namna hii ambaye unatoa ulichonacho yeye anatapanya inauma........
Kwa hiyo kwa upande wangu inategemea na aina ya mpiga mizinga kwa kweli, mwingine ana shida, hana kipato au kipato kimeshuka n.k hapo kumsaidia haina shaka.....
Ila siungi mkono mtu akupige mzinga halafu aende baa, au akalipe gest.....
BADILI TABIA ninachosema mimi kwa nin usimwambie direct?alafu kumbuka shida hazina tabia unaweza ukapiga mzinga hata mti chezeya shida wewe,alafu kuna emegency kama za kukutana mahala,kwanza ujue mpaka mtu anakuja kukulia shida ujue amekuthamin na kukuheshimu,haifai kutuponda tusiokuanavyo.