Wajua, kuna 2 Types of Leaders. Born Leaders na Manmade Leaders? Je, Wajua tutamfaidi zaidi Rais Samia kipindi cha 2025-2030 kuliko sasa If Only?

...bila Nyerere, Mkapa asingekua rais,kudai hakuwa na 'wa kumlipa fadhila' si kweli,alikalia kitu...
Si kwamba Nakubaliana na Kila kitu alichowasilisha mleta mada, lakini, hapa nilipoopa maneno kutoka bandiko lako ninaomba ufafanuzi.

Unadhani, Nyerere (Baba wa Taifa) alikuwa anahitaji fadhila gani kutoka kwa Mkapa(R.I.P) ambazo unadhani wakati huo alikuwa anazikosa kutoka sehemu nyingine ama kwa watu wengine ??

Na uwe specific kwenye majibu yako, sihitaji majibu ya jumla jumla!!!
 
Mimi binafsi sijaona chochote kwa Samia, miaka miwili Serikali hakuna Barabara Mpya, Sasa tutamfaidi kivipi ikiwa mpaka Sasa hatuoni chochote ?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kwa mujibu wa mleta mada, inasemekana anamalizia shughuli fulani hivi ambayo sina hakika Hata kidogo kama kweli hiyo ndiyo shughuli yake hasa.
 
Kwako Pascal, I can only say "A little knowledge is a dangerous thing"!

I think you just don't get it, most of it, and I guess this would be okay, IF you weren't spreading the rot to wide.
I hope I am wrong about you.
 
Hukuzingatia mabano, Nyerere hakutaka kuwa mwanasiasa Bali kiongozi wa kidini,askofu akamkataza na Mara akaibukia kwenye siasa,akawa kiongozi wa nchi,kitabu Cha van Bergen kinamnukuu akisema atalipa kanisa lake a better chance,wakati wa mwinyi kanisa lilikua vocal Sana kwamba nchi inakua islamized,misikiti inaongezeka,duru zinadai waliapa hatitawala Tena muislam,alipoingia mkapa kanisa lilikua kimya tu huku kampeni za uchaguzi zikifanyika kanisani,waumini wakuoneshwa picha ya mgombea wanayetakiwa kumchagua..na kutoa waraka uliosema watamchagua Ben... Nyerere wa wakati wake
 
Machawa mnatuchosha na ngonjera zenu. Hali ya maisha inazidi kuwa ngumu tangu aingie madarakani. Kila kitu kimepanda bei zaidi ya mara mbili, wizi, ufisadi maradufu. Acheni ujinga wenu bana.
Rais wetu mama Samia amefanya kazi njema Sana Tangia ameingia madarakani,Ameshughulika na mfumuko wa Bei kijasiri Sana kwa kutoa mabillioni ya Ruzuku,mfano katika mbolea alitoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu, hata katika Nishati ya mafuta serikali ilikuwa inatoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi na kupelekea kushuka kwa Bei ya mafuta ukilinganisha na majirani zetu.

Ameboresha huduma za kijamii na kuzisogeza karibu ya mwananchi, serikali Yake kwa Sasa inatoa Elimu bure Hadi kidato Cha sita,mikopo Elimu ya juu imeongezeka kufikia billioni Mia sita na pointi na kupelekea wanafunzi wote wenye sifa kupata mikopo na hivyo kutimiza Ndoto zao za kielimu.

Ajira kila mwaka anamwaga mitaani ,huku secta binafsi nayo ikiendelea kutoa ajira kila Siku kutokana na mazingira mazuri ya kiuwekezaji na kibiashara yaliyopo hapa nchini, watalii na wawekezaji wanaendelea kumimknika hapa nchini na kupelekea mapato kuongezeka mpaka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi pasipo kukimbizana Wala kufungiana biashara mitaani.

Uchumi wa Tanzania na mzunguko wa fedha mitaani unaendelea kuwa wenye Afya kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi mitaani,Sasa kufungua biashara Ni bure pasipo kusumbuliwa habari za mapato mpaka baada ya mwaka mmoja ili kuchochea ongezeko la biashara mitaani na kutoa fursa ya kukua kimtaji
 
Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Mabandiko yako haya ndio yanafanya tushindwe kukutofautisha na kina zembwela.
 
Mabandiko yako haya ndio yanafanya tushindwe kukutofautisha na kina zembwela.
Mkuu Gagi, Gagnija , mimi zaidi ya kuwa ni mwandishi wa habari wa kujitegemea na mtangazaji wa kujitegemea, pia ni mwanafasihi zote mbili, fasihi simulizi na fasihi andishi, baadhi ya mabandiko yangu ni mabandiko ya fasihi, hivyo ni only wale wenye uwezo to read in between the lines ndio wananielewa vizuri, mimi sio chawa, sijawahi kuwa chawa na kamwe sitakuja kuwa chawa!.

Kwa wale ambao mtakuwa mnapata muda kila Jumapili saa 3:00 usiku, nina kipindi cha KMT on Channel Ten, karibuni.
P.
 
Duh!.

Unamaanisha tuna Rais anayemridhisha yule aliyemfanya awe badala ya kuwaridhisha wananchi, hii ni dharau kwa watanzania japo ndio ukweli wenyewe.

Sijui kuna ubaya gani nikiandika; "hatuna Rais"
Mkuu denooJ , hii inaitwa kuwa mtu wa shukrani, awamu hii ya kwanza, Rais Samia hakuupata urais kupitia kwa wananchi, ameupata kwa kudra tuu za Mwenyeezi Mungu baada ya kushikwa mkono akawa VP ndipo na Mungu akatia mkono wake kivile, ndipo Rais Samia akawa rais.

Rais akiishakuwa ni rais, ni rais, huwezi kusema hatuna rais, tuna rais wa kudra za Mwenyeezi Mungu, mwaka 2025 sasa ndio tumchague rasmi kwa kura zetu, hivyo kutowajibiki kwa yeyote mwingine zaidi yetu sisi wananchi.
P
 
Leadership code
(1) Be self-confident
(2) Be decisive
(3) Take responsibility for anything happening under your watch.

Kuongoza ni kuonyesha njia na kuhakikisha wafuasi wanakufuata kwenye njia hiyo. Ili uweze kuonyesha njia kati ya nyingi zinazowezekana ni lazima ukubali codes hizo tatu hapo juu.

Ukishakuwa na leader ambaye hana confidence katika kufanya maamuzi na hata akifanya maamuzi anaweza kwenda mbele na nyuma hadi kutetemeka, na iwapo lolote linalotokea kwenye utawala wake likiwa baya basi atalaumu ama viongozi waliomtangulia au wafanyakazi wa chini yake na kusahahbu code (3) basi huna kiongozi bali una mwajiriwa. Rais trumann wa Marekani alisema "The buck stops here." Siku za hivi kjaribuni kumekuwa na lawama nyingi kutupiwa Magufuli na kusahahu kuwa "Swala hawezi kuruka deski la Rais"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…