Wajua, kuna 2 Types of Leaders. Born Leaders na Manmade Leaders? Je, Wajua tutamfaidi zaidi Rais Samia kipindi cha 2025-2030 kuliko sasa If Only?

Mkuu Pascal, ili kulinda heshima na taaluma yako hachana kabisa kutuletea makala za aina hii. Moja ya sifa ya mwandishi wa habari, ni kuhabarisha umma matukio kwa usahihi. Na pale anapotoa maoni binafsi basi hayo maoni yanapaswa kuaksi ukweli wa jambo lenyewe.

Uchaguzi mkuu uliopelekea Samia kuwa Rais wa nchi baada ya JPM kufariki ulikuwa ni batili. Ni uhani uliofanyika kwa kupoka matakwa ya umma wa Tanzania na kujitangazia ushindi batili na baadae kuunda serikali. Urais wa Samia ni zao la kihalifu. Hii inathibitishwa mbali na jinsi tulivyo ona kipindi cha uchaguzi pia matamko ya viongozi waandamizi ndani ya chama na serikali yanathibitisha hili. Mfano, Kinana na Makamba wameliweka wazi hili la uchaguzi wa 2020 siku chache zilizopita, ukiachia mbali matamko ya Rais Samia mwenyewe hasa kipindi anatangaza zile 4Rs zake.

Haramu siku zote haiwezi kuhalalishwa na jambo lolote lile. CCM chama nilichokipenda kwasasa kimegeuka kuwa genge la Viongozi mafisadi, wezi wa mapato na rasilimali za nchi. Wanalindana ktk wizi. Kimekuwa chama cha kurithishana madaraka kwa watoto na ndugu zao kidogo na kwa chawa wanaojikomba. Sifa ya kuwa kiongozi sasa hivi ni konekshini na uchawa. Ndiyo huu mwendo unaousifia? Mwanasheria na mwandishi wa habari nilidhani utakuwa na akili pembuzi zaidi yetu tusiokuwa wataaluma. Kwa kiwango chako inasikitisha sana, ingawa sishangai kwasababu ndiyo zao la mfumo hasa kuanzia kipindi cha JPM. Sifiasifia na kutukana wapinzani kesho unakula uteuzi. Alifanya hivyo Jerry Muro na wenzake wakafanikiwa sasa ni zamu yako!!!
 

Nyerere alihitaji kanisa katoliki liendelee kushika hatamu Tz basi
 

Pascal , CCM ni CCM tu hata awe vipi , zaidi ya miaka 60 wako madarakani hamna kitu chochote cha maana walichokifanyia nchi zaidi ya mipasho na majisifu na kuirudisha nyuma nchi kimaendeleo.

Leo humjui aliyesoma wala asiyesoma . watu wako mbioni kila mmoja analia njaa , labda wewe unayetupiwa mafupa labda unaona unafaidi na kupata ujasiri wa kuja kuwasifu humu JF.

Wapo hapo madarakani kwa sababu ya nguvu ya dola tu lakini vyenginevyo kungekuwa na uchaguzi huru na wa haki wangelishaondoka zamani sana tokea enzi zile za Nyerere alipopinduliwa na majeshi miaka ya 60s.

wawashukuru sana , jeshi, polisi, usalama na vyombo vyengine vya usalama kwa uharamia wanaoufanya wakati wa uchaguzi.

watu walishawachoka miaka mingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…