Wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu? Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji? Wajua ubakaji unaweza kuwa alali? IGA batili yaweza kuzaa HGA halali?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hili ni bandiko la kitu kinachoitwa critical thinking, kama wewe sio critical thinker, nakushauri pita mbali na bandiko hili.

Angalizo la Uzalendo
Haya ni maswali critical, yanayotokana na critical thinking na critical analysis kwa lengo la kuwaelimisha Watanzania some complex issues kwa kutumia mifano rahisi ya vitu vya everday in our life.

Maswali yenyewe ni

Je, wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu?. Vivyo hivyo kuna mikataba halali, batili na batilifu.​

IGA ya serikali yetu na DPW iliyoridhiwa na Bunge letu tukufu ni IGA halali, Batili au Batilifu?​

IGA hiyo inakwenda kuzaa ndoa ya TPA na DPW, jee ndoa hii ni halali, batili, batilifu au ni Ubakaji tuu?​

Je, wajua japo ubakaji ni kosa la jinai, lakini ubakaji unaweza kuzaa ndoa halali?.​

Jee Wajua IGA batili Inaweza kabisa kuzaa HGA halali?​


Nimekuwa nikitumia mifano hii ya ndoa kwa hoja nyingi humu baadhi yake ni hizi Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu!

Andamana nami...

1. Je, wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu?​

2. Vivyo hivyo kuna mikataba halali, batili na batilifu​

Kama ulivyo mkataba wa ndoa, vivyo hivyo kwenye mikataba ya Kitaifa na Kimataifa.

Kwa mujibu kifungu cha 2(1) (h) cha Sheria ya mikataba Sura ya 345 (2002) kinasema, “Mkataba ni makubaliano yanayofanyika kati ya mtu mmoja na mwingine ambayo yana lengo la kuwa na nguvu ya kisheria.” Kifungu hicho pia kinasema “mkataba ni makubaliano ya kisheria kati ya pande mbili au zaidi yanayoeleza haki na wajibu wa kila upande. Mgawanyo wa aina za mikataba unategemea na muktadha wa kimazingira. Kama tunataka tutumie maandishi kuigawanya; itaitwa mikataba ya maandishi (written) na mikataba ya maneno (oral).
Kama mtu anataka kutumia uhalali; ataita mikataba halali (legal), mikataba batili (void) na mikataba batilifu (voidable). Kama kigezo ni utekelezaji itaitwa mikataba iliyokwisha tekelezwa (executed) na mkataba utakaotekelezwa baadaye (executory), mikataba ambayo upande mmoja umeshatimiza wajibu wake (unilateral) na mikataba ambayo pande zote zinapaswa kutimiza wajibu wake baada ya kusainiwa (bilateral)

3. IGA ya serikali yetu na DPW iliyoridhiwa na Bunge letu tukufu ni IGA halali, Batili au Batilifu?​

4. IGA hiyo inakwenda kuzaa ndoa ya TPA na DPW, kupitia HGA. jee ndoa hii ndoa halali, batili, batilifu au ni Ubakaji tuu?.​

Kwa vile kwa hoja zangu za kisheria, hii IGA ni null and void, hivyo HGA, inayokwenda kuzaliwa kati ya TPA na DPW ni ubakaji!.

5 Je, wajua japo ubakaji ni kosa la jinai, lakini ubakaji unaweza kuzaa ndoa halali?​

6. Wajua IGA batili Inaweza kabisa kuzaa HGA halali?.​

Hitimisho
Kwa vile katika kuileta DPW, Rais Samia ana nia njema ya dhati kuisaidia nchi yetu, na hakuna mtu yoyote anayepinga uwekezaji kwenye Bandari zetu, wasaidizi wa rais na sisi Watanzania wengine wote tuna wajibu wa kumsaidia rais wetu, kuisaidia serikali yetu na kulisaidia taifa letu to do the right thing and do them right!. Huu ndio uzalendo wa kweli. Hivyo ile IGA ni IGA batili, void ab initio, lakini itazaa HGA halali kabisa!. Kitu muhimu ambacho serikali yetu itapaswa kukifanya ni kuwa very transparent ili kuwaonyesha Watanzania jinsi batili inavyoweza kugeuka halali.

Paskali
 
Wanabodi
Hili ni bandiko la kitu kinachoitwa critical thinking, kama wewe sio critical thinker, nakushauri pita mbali na bandiko hili.

Naomba usichangie kwanza hoja zinafuata....
Paskali
Pascal uzi tayari au?


Maana heading inashawishi mtu kufungua uzi asome ila uzi wenyewe ni vitisho kwa non critical thinkers.

Uzi tayari.
 
Wanabodi
Hili ni bandiko la kitu kinachoitwa critical thinking, kama wewe sio critical thinker, nakushauri pita mbali na bandiko hili.

Naomba usichangie kwanza hoja zinafuata....
Paskali
Kaka Paskali,
Fedha zilizopatikana kwa njia ISIYO halali, zikiingizwa kwenye shughuri halali, au zikatumika kuanzisha shughuri halali, tunaita utakatishaji wa fedha. Hii ina maana kuwa ili kitu kiwe halali, the entire process inatakiwa iwe halali. Kwa muktadha huu, IGA Batili HAIWEZI kuzaa HGA Halali.
 
Jee wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu?. Vivyo hivyo kuna mikataba halali, batili na batilifu.
Ndoa ambazo zimeonekana kuwa batili zinaweza kuhitaji kubatilishwa badala ya talaka! Vivyo hivyo, Mkataba unaonekana ni batili unaweza kubatilishwa.

Sasa Ndoa batili ni ipi?
Wajuvi wa Sheria za ndoa wanasema Ndoa batili ni, mpangilio wa ndoa ambao hautambuliwi kama halali na sheria....
Ndoa yetu ina Uhalali? Na uhalali huo tumeupata wapi? Na tumepata kwa kwa Sheria ipi?
Mpaka hapa tulipo Ndoa yetu(Tanzania na DPW) imepata uhalali na IGA na baada ya Bunge letu kujadili na kuridhia mkataba wa ndoa yetu?, yaani Bunge limekubali kuwa , Wazazi wetu Tanzania na DPW wamekidhi yote yanayotakikana kabla ya ndoa i.e Umri wetu,
makazi yetu, mamlaka yetu, wajibu wetu, wapi na lini tunaweza peana talaka kwenye ndoa n.k n.k Je, masuala ya uhalali wa ndoa yetu walioridhia yamewekwa bayana? Na kama hayako bayana wamehalalisha ndoa iliyo batili?

Kwa hayo tunaweza kusema Uhalali wa Ndoa ya Nchi zetu mbili una mashaka. na kukiwa kuna mashaka tunaweza peana talaka sasa Tunapeana vipi talaka ndoa ambayo tayari inaonekana ni batili?

Ubatili wa Ndoa yetu Ubatilishaji wake:


Again, wajuvi wanasema

"Ubatilishaji (wa ndoa)ni mchakato wa kisheria wa kubatilisha ndoa"
Ni nani mpaka hapa tulipofikia anaye mamlaka ya kubatilisha ndoa yetu?

Maswali ya Pascal yapo loaded kweli kweli!


Sasa kwaavile mimi sio mwanasheria nitagota hapo.
 
Mtajirudi mdogo mdogo tu kikubwa uzima!!
 
Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu rais kuongoza mihula miwili (2) mfululizo ya urais kwa maana ya miaka 10.. ila ikiwapendeza wabunge wetu wanaweza wakafanya namna kurekebisha hicho kifungu ili kukidhi mahitaji yetu kwa sasa.. Mama Samia aongoze hadi 2040.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…