Wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu? Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji? Wajua ubakaji unaweza kuwa alali? IGA batili yaweza kuzaa HGA halali?

Sijui wanasheria wetu walipumbazwa na nini hadi wakaridhia huu mkataba wa hovyo kupindukia!
Kama ni Rushwa basi walipewa fedha nyingi sana hadi wakawa vipofu!
Na kama ni "maelekezo" basi yalitoka juu sana kiasi kwamba hawakuthubutu kuugusa
Mungu ibariki Tanzania, tuepushe na udhalimu wa watu hawa wachache na ukawe MWAMUZI wetu. Amen
 
Hivi technicalities ndizo zinazowapa loopholes watu kutupiga...

Kibaya ni Kibaya tu hata ukifanye nini (If you put lipstick on a Pig its still a Pig)

A Rose by any other Name Smells just as Sweet....

Kwahio ili turahisishe mambo tufanye jambo Moja.... tuondoe usiri wa mikataba / makubaliano ili wanaoingia au wanaotaka kufanya yao wajue kabisa yatakuwa wazi.... Hayo mengine yote ni kuchanganyana akili...
 
Asante Kwa andiko zuri na Kwa mara ya Kwanza umeitendea haki taaluma ya sheria.
Kwa Leo nisichangie mengi kwenye andiko lako lakini Nataka wavivu wa kusoma kama Mimi watoke na neno moja la ajabu kwenye mkataba huu kwamba DPW iligeuzwa kuwa nchi (UAE/DUBAI) wakati wa kusaini IGA na ikifika wakati wa kusaini HGA DPW watarudi kuwa Kampuni kama kawaida. Utapeli huu bado wanasheria wa Tanzania hawauoni wametia pamba masikioni.
 
Kama ndio hivyo fungeni huu mjadala.
 
Ni Rahisi tu kusema,

Pasingekuwa na kelele za wananchi kupinga mkataba huu fake na BATILI,

Wewe ulikuwa umeshaubariki tayari.

Bendera nakusihi nenda kokote kufuata uelekeo wa upepo.

Sasa unaweza kurudisha akili zako mfukoni na mambo mengine yaendelee!!
 
Hakunaga mzalendo muoga.
 
Mkuu mimi sio legal expert ila Katiba mbovu haiwezi kuzaa sheria nzuri/bora
 
Mikataba inaweza kuingiwa kwa namna mbili.
1. Written
2. Oral
Hiyo sio mikataba ya aina mbili ni namna mbili unavyoweza ingia mikataba. Oral agreements japo inatambulika kisheria lakin sio njia nzuri. Kwanini? A anaweza ongelea bahari, B akatafsiri ziwa. Mahakamani inakuwa ngumu ku verify ni nini hasa mlikubaliana so busara ni kuingia written agreement.

Difference between ya bilateral and unilateral agreements.
Bilateral agreement A anatoa apple, B anatoa pear. Kuna promise of of exchange za pande mbili. A akija na apple lake B ukisema huna pear anaweza kukushitaki.

Unileteral agreement ‘A’ anatoa ahadi kwa ‘B’ ukiosha gari ntakulipa tsh 50000. A na B hawana mkataba, mpaka B atakapoosha. Awezi kwenda kumshitaki B asipotaka kuosha gari.
 
Ukiacha kutetea DP world tutakuunga mkono
Mkuu JakiDubai, kuna watu wanaandika jf ili waungwe mkono?, utaniunga mkono ili iweje?.
Anyway karibu, hili ni moja ya mabandiko yangu kuunga mkono IGA ya DPW na Bandari zetu, angalia tuu tarehe ya bandiko hili ili ulinganishe na wengine, na ikitokea una uwezo wa kusoma contents, soma contents uone jinsi ninavyoisupport DPW na Bandari zetu!.

Karibu

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…