Wajue vizuri kuhusu wale jamaa wabishi wa Aziv Battalion, ambao wamemtia unyonge Putin pia Warusi wenzetu wa pale Tandale

Wajue vizuri kuhusu wale jamaa wabishi wa Aziv Battalion, ambao wamemtia unyonge Putin pia Warusi wenzetu wa pale Tandale

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Habari ukisubiria kikao cha Kamati kuu CHADEMA tupitie hapa

Nilisema nitakuja kuwaelezea vizuri kuhusu wale jamaa wabishi wa Aziv Battalion, ambao mpaka leo wamemtia unyonge Putin pia warusi wenzetu wa pale Tandika kaburi 1.

Putin alisema lengo lake la kuivamia Ukraine ni kui demilitarize na kuondoa neo-nazi ndani ya Ukraine. Baadaye akajikita zaidi kwenye madai ya kuondoa manazi.

Je, ni kweli ndani ya Serikali ya Ukraine kuna Neo-Nazi?

Twende taratibu. Kabla ya September, 2014 palikuwepo na kundi lenye itikadi za Neo-Nazi, na walijitambulisha hivyo na wakijiita neo-Nazi Social National Assembly (SNA) group

Kundi hili liliweka lilianzishwa huko maeneo ya East Ukrain hasa Mariupol na kusambaa East yote. Putin na Oligarch wenzake mdiyo vinara wa kulichukia kundi hili. Hata sababu kubwa waliyoitumia kuivamia Ukraine ni kuwa wanaenda kuwaondoa Neo Nazi ndani ya Ukraine. Ilikuwaje? Endelea kufuatilia.

Kundi hili lilikuwa na misimamo mikali katika ku support motives zao. Kati ya idea zao ni white supremacy, racism nationalism, kupinga ushoga, etc.
Kubwa ya walichokua wakikisimamia ni Nationalism (National Idea).

Hawa jamaa kilichopelekea kuundwa kwao ni chokochoko za Russia kule mashariki mwa Ukraine. Ninapoongelea mashariki au kusini mwa Ukrain, hapo utambue ni majimbo ya Jirani na Russia ambayo yana watu waongeao kirusi kwa wingi, ambao Russia anawaona ni raia wake na huwatumia sana kwenye agenda zake.

Uongozi wa Ukraine ulikuwa unabadilika kwa kufuata either upepo wa West au wa Russia kulingana ma serikali iliyochaguliwa. Hivyo itokeapo aliye madarskani anafuata upepo wa Russia, basi yale maeneo ya mashariki hata ulinzi hulegezwa na Russia kuendelea kutengeneza mamruki ambao huwaingiza kule kama wakaazi, huku wengine wakiwa ni wakaazi wa kule ila wenye asili ya Russia.

Kundi hilo lilikuwa ni la watu wa kujitolea tu, likawa likisumbuana sana na wale Russian separist wanaotaka kujitenga. Hawa walikuwa hawataki habari za kujitenga, kwao siku zote Ukraine ni moja.

Mwaka 2014, uasi wa kutaka kujitenga ukawa umepamba moto mashariki mwa Ukraine, hasa baada ya mwezi February 2014, Crimea kufanikiwa ya kuwa annexed na Russia.

Mapigano yakapamba moto hasa. Mwaka huohuo (mwezi May, 2014) kundi hilo, yaani neo-Nazi Social National Assembly (SNA) group* likaungana na kundi lingine la ultra-nationalist Patriot of Ukraine gang, na kutengeneza kundi lililoitwa Azov Battalion, ambapo ideoligies zao zilibaki vilevile, maana zilifanana (Makundi yote mawili yalianzishwa na mtu mmoja, kundi moja lilianzishwa mwska 2005, lingine mwaka 2008).

Kundi hili lilikuwa linaundwa na wana mgambo ambao walikuwa hawalipwi chochote kile. Vurugu na mapigano vikaendelea huko Donetsk na hasa Mariupol. Kumbuka Russia alikua ameshwtangaza kuwaunga mkono separist na akawa akiwapelekea silaha na wanajeshi ili kuwasaidia kwenye mapambano yao.

Mapambano yaliendelea hadi Jeshi la Ukrsine likaanza kuzidiwa, na walipoona raia wanazidi kubeba madhara ya viti ndipo Jeshi na Polisi vijaamua kurudi nyuma na kuondoka. Donetsk ikawa imeanguka, bendera za Ukraine zikashushwa.

Hapo mdipo Azov Battalion (Azov Regement) wakaenda mstari wa mbele kupambana na majeshi ya Russia na waasi. Mapambano yalikuwa ni makubwa lakini kundi hili la mgambo wa kujitolea halikujali kitu, lilirndelea kupsmbsna hadi Russia ma Separist wakakimbia na kuiacha miji. Mariupol ikawa imekombolewa, wakapandisha bendera ya Ukraine.

Ndipo ilipofika November, 2014, serikali ya Ukraine ikaamua kulitambua rasmi na kukiingiza kwenye Jeshi lake wakiitwa Azov Battalion kama walivyojiita na kuwa moja ya vikosi vyake na kikawa na Majukumu yake huko Mariupol.

Maana waliona hii ndiyo tiba ta Russia ma kwa kuwa wanaiogopa basi ndiyo sindano ya kuwachomea.

Tangu hapo Putin akapata nguvu ya kulalamika kuwa kuna neo nazi kwenye serikali ya Ukraine. Wakawa wanapeleka askari wa Russia na wale Wagner kufanya mashambulizi lakini walikutana na upinzani mkali wa Azov battalion.

Katika vita hii ya Ukraine, pale Donetsk na Mariupol, sehemu kubwa ya wapuganaji ambao Russia ilikabiliana nao ni hawa Azov battalion, ni sababu ya kikosi hiki Russia iliamua kutumia makimbora mbali kuchakaza majengo kabla ya kupeleka askari wake, ni sabsbu ya kikosi hiki ambacho sskari wske wengi huwa ni vokunteer ilipelejea Putin kutoa amri ya kuimarishwa kwa ulinzi pale kiwandani na kuhakikishu hata inzi hatoki eneo lile. Hiyo yote ni sababu ya tabia na uwezo wa kikosi cha Azov.

Hao ndiyo Azov Battalion, wanaume walioiharibu Victory Day ya Putin na kumpelekea awe mnyonge kwenye siku aliyoipa umuhimu hadi dunia ikatega sikio kusikia atakacho sema, badala yake akaishia kulialia kuwa NATO wanataka kuivamia Russia.

Bado wapo kiwandani, huku wengine wakiendeleza mapambano kwenye maeneo mengine Donetsky na Luhansky.

Russia amekomaa kuwa hawa ni nazi, wakati the Nazi part ya hawa ilishakufa walipokuwa absorbed jeshini, tena by the time wanakuwa absirbed only 12 percent nduyo walikuwa na hizo ideologies.

5ED30680-FE37-4102-9DCE-CBC0A2F71193.jpeg


Britanicca
 
The power hand is changed so is the support of many of our camared; wherever you are get ready, the game is over!
 
Hao Azov Regiment wana mkono mrefu sana wa CIA convert operations, na Mosad. Hawaondoki hao hadi Russia akimbie. Na ndiyo eneo NATO wameli target kuweka missiles zao once Ukraine ikishaingia. Na operations zingine za kwenda kuisambatisha Russia.
 
Oyaaa [emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23] Ulaya wameshatoa nje kikwazo cha kusafirisha mafuta miongoni mwa vikwazo walivyowawekea Urusi

[emoji116][emoji116][emoji116]

[emoji91][emoji91][emoji91]The ban on the transport of Russian oil is no longer included in the 6th package of sanctions against the Russian Federation - the German agency DPA[emoji91][emoji91][emoji91]
 
Hao Azov Regiment wana mkono mrefu sana wa CIA convert operations, na Mosad. Hawaondoki hao hadi Russia akimbie. Na ndiyo eneo NATO wameli target kuweka missiles zao once Ukraine ikishaingia. Na operations zingine za kwenda kuisambatisha Russia.
Ngoja Russia na yy akasuport vikundi vya kigaidi Mexico na nchi za wauza ngada ndio atajua hajui
 
Weee kaka sindano zako mbona Kama zina dawa ile ya crystapen......alisikika Pro Russian na kobazi zake huko Tandika Kaburi moja na wenzie kutoka Buza na vingunguti
 
Back
Top Bottom