Wajue Wabunge watano waongoza kuchangia bungeni

Peter Dafi

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
392
Reaction score
272
Dodoma. Tangu kuanza kwa Bunge Maalumu la Katiba, Februari 18 mwaka huu, wajumbe watano wanaonekana kuwa ndio wachangiaji wakuu katika mjadala wa Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo.
Bunge hilo la Katiba limekuwa likijadili Rasimu ya kanuni za Bunge kwa takriban wiki moja sasa na mjadala huo bado hilo haujamalizika kutokana na mivutano miongoni mwa wajumbe kuhusu baadhi ya vifungu vya kanuni hizo.

Pamoja na Bunge hilo kuwa na wajumbe 629, wanaochangia kila mara ni Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, Mbunge wa Nzega (CCM), Hamisi Kigangwalla, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika (Chadema) na Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiel Oluoch.

Mbali na kuchangia, wakati mwingine wajumbe hao wamekuwa wakinyoosha mikono au kusimama kwa lengo la kuchangia, lakini wanakosa nafasi.
Mfano mzuri ilikuwa ni jana wakati wa mjadala kuhusu Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo, wakati Ole Sendeka na Oluoch waliposimama na kuchangia.

Katika mjadala wa juzi, wajumbe hao wawili kila mmoja alichangia mara tatu na mara nyingi walipochangia hoja zao ziliungwa mkono na wajumbe wengi.

Kigwangalla naye hayuko nyuma kwani katika mjadala wa juzi alipewa nafasi mara mbili kuchangia na wiki iliyopita huchangia mara mbili kwa siku isipokuwa siku moja tu ambayo alichangia mara moja.
Mjumbe mwingine ni Mnyika ambaye katika mjadala wa juzi alichangia mara mbili kuhusu mkanganyiko juu ya kuchagua aina ya upigaji wa kura.

Naye Serukamba amekuwa mchangiaji wa karibu kila siku na Ijumaa iliyopita alichangia kuhusu kifungu cha 37 na 38 cha Rasimu ya Kanuni hizo.

Sasa imekuwa jambo la kawaida kwa wajumbe hao kuchangia katika Bunge hilo.

Chanzo:- Mwananchi
 
Kwa kutuletea hapa JF taarifa hii wewe mleta mada pendekeza basi waongezewe posho.
 
Kwa Kigwangala nadhani si sawa! Hivi ameshamfikia profesa Remmy kweli, je? Dk William
 
PANDU, MAHALU LISU SIMBACHAWENE MDEE
MWL OLOCHU UMMY MWALIMU MNYIKA
OLESENDEKA VICENT MBOWE MACHALIII
LIPUMBA wengine tuwataje mtzamo wangu wengi
hawajali wako kimaslahi zaidi ilimradi kiingie mfn
kipindi cha posho wote wanafungua midomo
naamini wengi ukiwaulizw juu ya rasimu hawajui
kitu hawasomi kinachoendelea
 
hili bunge ni machi km ya world cup kwa LISSU..lissu ana mchango mkubwa sana na ana umuhimu sana kwani anachambua vyema na ana nia njema sana.Hata anaposhambuliwa reaction yake ipo veye fair, hata wtau anaowapendekeza huwa ni watu wenye kuaminika kiasi kikubwa bila tegemea chama. Yaani haya ndio maeneo yake
 
Maccm hata yakichangia ni pointless tu....
 
Toweni ushabiki wa Simba na Yanga hapa. Badala ya kuwalisha watu Habari zilizoshiba hoja za hao waliotajwa ili tujue mantiki nyie mnakuja na hoja dhaifu eti fulani kachangia mara ngapi?!
Busara ilikuwa ni kuonesha uchambuzi wa hoja za kila mjumbe ili watu wawajue hawa jamaa vizuri! Unaweza kukuta wanachangia mara nyingi lakini hawapo upande wa wananchi!
 
Katika bunge hili la katiba nina imani kubwa na hawa wafuatao, john mnyika, tundu lissu, lipumba, jussa, mbowe,mbatia, sitta, bulaya, mdee, sakaya, kigwangallah, lugora, filikunjombe na sendeka kidogo. Prof. Safari na mtatiro, nje ya hapo ni wapiga dili!
 
PANDU, MAHALU LISU SIMBACHAWENE MDEE
MWL OLOCHU UMMY MWALIMU MNYIKA
OLESENDEKA VICENT MBOWE MACHALIII
LIPUMBA wengine tuwataje mtzamo wangu wengi
hawajali wako kimaslahi zaidi ilimradi kiingie mfn
kipindi cha posho wote wanafungua midomo
naamini wengi ukiwaulizw juu ya rasimu hawajui
kitu hawasomi kinachoendelea

Huyu Oluoch anafikiri fikiri ki-CWT zaidi, ana-argue hata mambo asiyoyajua vizuri hadi anaboa. Si angetulia ajifunze kwanza?
 
Mtu anaweza kuwa kiherehere wa kuongea lakini anachoongea ni pumba tupu
 
Kwa thred hii ni wazi kuwa machagadema yanazidi kufa
 
Kwanini unaendelea kuandika ujinga kila siku? Jifunze kwa wanaccm wenzako wanavyojenga hoja humu mtandaoni na sio kuandika tu kama unajamba!
 
Katika bunge hili la katiba nina imani kubwa na hawa wafuatao, john mnyika, tundu lissu, lipumba, jussa, mbowe,mbatia, sitta, bulaya, mdee, sakaya, kigwangallah, lugora, filikunjombe na sendeka kidogo. Prof. Safari na mtatiro, nje ya hapo ni wapiga dili!
Nakuunga mkono mkuu,mtu kama Lowassa,Kingunge wanapiga miayo kusign posho..ma ccm ni majanga.
 
Dodoma. Tangu kuanza kwa Bunge Maalumu la Katiba, Februari 18 mwaka huu, wajumbe watano wanaonekana kuwa ndio wachangiaji wakuu katika mjadala wa Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo.
Bunge hilo la Katiba limekuwa likijadili Rasimu ya kanuni za Bunge kwa takriban wiki moja sasa na mjadala huo bado hilo haujamalizika kutokana na mivutano miongoni mwa wajumbe kuhusu baadhi ya vifungu vya kanuni hizo.

Pamoja na Bunge hilo kuwa na wajumbe 629, wanaochangia kila mara ni Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, Mbunge wa Nzega (CCM), Hamisi Kigangwalla, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika (Chadema) na Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiel Oluoch.

Mbali na kuchangia, wakati mwingine wajumbe hao wamekuwa wakinyoosha mikono au kusimama kwa lengo la kuchangia, lakini wanakosa nafasi.
Mfano mzuri ilikuwa ni jana wakati wa mjadala kuhusu Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo, wakati Ole Sendeka na Oluoch waliposimama na kuchangia.

Katika mjadala wa juzi, wajumbe hao wawili kila mmoja alichangia mara tatu na mara nyingi walipochangia hoja zao ziliungwa mkono na wajumbe wengi.

Kigwangalla naye hayuko nyuma kwani katika mjadala wa juzi alipewa nafasi mara mbili kuchangia na wiki iliyopita huchangia mara mbili kwa siku isipokuwa siku moja tu ambayo alichangia mara moja.
Mjumbe mwingine ni Mnyika ambaye katika mjadala wa juzi alichangia mara mbili kuhusu mkanganyiko juu ya kuchagua aina ya upigaji wa kura.

Naye Serukamba amekuwa mchangiaji wa karibu kila siku na Ijumaa iliyopita alichangia kuhusu kifungu cha 37 na 38 cha Rasimu ya Kanuni hizo.

Sasa imekuwa jambo la kawaida kwa wajumbe hao kuchangia katika Bunge hilo.

Chanzo:- Mwananchi
Huyo sijui Oluch juzi aliniacha hoi eti akimaliza kuchangia tuu mjada ufungwe wakale chakula sababu vyakula ni vya shida Dodoma.Ili kuwa wapo kifungu cha 32 mida ilikuwa kama saa mbili kasoro usiku.
 
Back
Top Bottom