Wajue wanao takiwa kuwa na vitambulisho vya Ujasiriamali

Wajue wanao takiwa kuwa na vitambulisho vya Ujasiriamali

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
#AMA KWELI KODI YA KICHWA YA MIAKA ILE IMERUDI, HAPA JF 99.9% ya wanabody tumo humu na vinatuhusu.

MKUU WA MKOA WA IRINGA ATOA VIGEZO VIPYA VYA WANAOTAKIWA KUPEWA VITAMBULISHO VYA UJASILIAMALI

1. Vibarua wa viwandani wasio na mikataba maalum.
2. Wafanyakazi wote wanaofanya kazi kwa wenye maduka/stoo za jumla.
3. Wabeba mizigo wote kwenye stendi zetu.
4. Wafanyakazi kwa wamama/baba ntilie.
5. Wachuuzi kwenye mialo yote.
6. Vibarua wote wa viwanda/mashine za kusaga unga au kukamua mafuta ya Alizeti.
7. Wafanyakazi wote walio kwenye saloon za aina zote.
8. Wale wote wanaopeleka kuuza chai kwenye viwanda vya chai toka mashamba binafsi.
9. Wafugaji biashara wote wa Ng'ombe na kuku.
10. Vibarua kwenye garage zote.
11. Wachomeleaji (welder) wote.
12. Vibarua wote kwenye karakana za Uselemala.
13. Vibarua wote kwenye vijiwe vya nyama choma/chips.
14. Wapiga debe wote kwenye stend za Iringa.
15. Wanachama walio kwenye vikundi vyote vilivyopewa Mikopo.
16. Vibarua wote walio kwenye Migodi yetu.
17. Wanachama wote wa Saccos za Iringa.
18. Vibarua wote kwenye vibanda vya simu.
19. Wafanyakazi wote kwenye Supermarket
20. Wafanyakazi wa vituo vya Mafuta.
21. Vibarua wote katika Mashamba ya miti.
22. Wanaochoma mahindi barabarani, ya kutafuna.
23. Wafanyakazi wa guest wote.
24.Wafanyakazi wa restaurant wote.
25. Wafanyakazi wote wa baa.
26. Waliowezeshwa na Mfuko wa Tasafu na waliopiga hatua kwa msaada huo.
27. Wanaolima na kuuza kibiashara bustani za mboga.
28. Waganga wote wa Tiba za jadi.
29. Wanachama wote wa Vikundi vya vikoba.
30. Vilabu vyote vya pombe za kienyeji.
31. Madereva wote wa daladala, bodaboda, mabasi, Hiace.
32. Makondactor wote wasio na Mikataba rasmi.
33. Wajasiliamali wote kandokando mwa barabara.
34. Wafanyakazi wote katika Butcher za nyama/samaki.
35. Wafanyakazi wote wa carwash.
36. Waandishi wa habari wote.
37. Wanaofyatua tofali za biashara wote.
38. Walio kwenye sector ya Utalii wote.
39. Vibarua kwa wakandarasi wote na mafundi wote wa nyumba.
40. Wafugaji wa nyuki wote.
41. MCs wote na wapiga picha.
42. Madalali wote wa nguzo, nyumba, mashamba, mazao nk.
43. Wakusanya mazao wote.
44. Wanaokopi/rekodi nyimbo Vibarazani mwa maduka.
 
Huyo atakuwa amevuta bangi ya Njombe sio bure.
Kaona vimewadodea anaamua kutafuta makundi yasiyohusika.

Nchi hii inaongozwa na vichaa wengi sana wa kuteuliwa kumzidi aliyewateua.
 
Hadi sisi washereheshaji wa shughuli jamanii khaa🙆‍♀️🙆‍♀️

Ila nimejikuta nacheka tuu namba 28,29 na 30😄😄😄😄uuuuhhhh
 
Ila huo moto wa motoni na jehanamu
unavochochewa hauwezi kuwaacha salama hasa wote walio kipindi hiki, maana kwa style hii inaonyesha mwisho wao sio mzuri.
 
Yes dear!
Naona nami niko kwenye list wakati pato langu kwa mwezi ndo hiyo 20,000/= sasa sijui nikiitoa nitaishi vipi?[emoji848]
Wote tupo kwenye orodha...hakika wasakatonge wa nchi hii tupo mbioni kutoweka kabisa kwenye ramani ya nchi
 
"Ili unyolewe saloon lazima uwe na kitambulisho".

Huku ndiko tunapoelekea
 
Ujasiriamali una maana pana sana na lengo la raisi wetu mpendwa ni kuwaokoa wajasiriamali na adha waliyokuwa wanapata kukimbizwa kila kona na kunyang'anywa bidhaa zao.Hapo kwenye list angeongeza na manamba wa kwenye migodi na madalali wa mitandaoni pia
 
Hivi vitambulisho si vya wJasiriamali mbona naona na wafanyakazi wanatakiw kuwa navyo
 
Back
Top Bottom