Wajue wasanii 30 waliopotea katika musiki huku wakiwa na mashabiki wengi

Nilipokuwa bongo nilimuuliza msanii mmoja alipo bob haisa ...jamaa alinijibu kuwa bob haisa amekuwa chizi kabisa wa kuokota makopo ...ilinisikitisha sana kwa kweli
 
kuna chuma cha kuitwa FRED SAGANDA!mtu hatari sana kimuziki!....au mtu wakuitwa JUMA KAKERE!huyo mtu mzima najua ngoma zake mbili ila ni mikosi!..........halafu kuna fundi mwingine wakuitwa NURUELLY!ukimsikiliza huyo ndo utajua kuna watu wanajua siyo hawa watoto kina ben pol sijui belle 9
 
Nilipokuwa bongo nilimuuliza msanii mmoja alipo bob haisa ...jamaa alinijibu kuwa bob haisa amekuwa chizi kabisa wa kuokota makopo ...ilinisikitisha sana kwa kweli
je ni kwelii?au wabongo wameshamtengeneza?mana wabongo waone ivi ivi si umesikia ya GEITA CHATA mtu aliyekufa mwaka jana na kuthibitishwa hospitalini na kuzikwa kaonekana na sasa anakula ugali home?chezea WATZ wewe!
 
Juma Mohamed Mchopanga alitoka na kibao chake cha Famous na kilibamba na still kinabamba ktk anga za Hiphop hapa kitaa...
naomba umtoe hapo

mkuu kitaa gani hicho Famous bado inabamba? hii ni habari mpya kwangu ..
 
kuna mtu anaitwa Roho7 kwa watu wa Hiphop alinusa tu alafu akasepa...kwenye kuimba nna mmiss dada anaitwa Stara nilimpenda kwa kweli na wale Chuchu Sound band walitisha sana.
 
Mi ninayemsikitikia ni Q jay nilijua atashine mda mrefu lakini ndo hivyo
dogo kawa mlokole he is a very commited born again christian.usitegemee kabisa kumsikia tena kwenye bongofleva.
 
Bob rudala je???emmanuel nkulila??
hahaha.huyo nkulila miaka ya 90 cc wengine ndo alikuwa role mode wetu.nakumbuka zile interwiew alizo kuwa anafanyiwa na kina mike mhagama na sunday shomari pale radio one.
 
Namkumbuka sana SQUEEZER na lile sauti lake....lakini mwisho wa yote aliishia kula mmea kule msewe na mwenzake OCG....
 
Enika na Baridi kama hii..inanibamba mpaka leo
 
kuna mtu anaitwa Roho7 kwa watu wa Hiphop alinusa tu alafu akasepa...kwenye kuimba nna mmiss dada anaitwa Stara nilimpenda kwa kweli na wale Chuchu Sound band walitisha sana.

roho saba ni mtu kweli ambaya hata ukisikia flow yake ni ya kipekee sana tofauti na wanahip hop wengi kina sijui ONE,DARASA ambao flow zinafanana!sijui kapotelea wapi,angekaza stress zingewajaa wengi....anakuambia hip hop ni urithi alioachiwa na brother BIG na PAC!
 
wapi MZUNGU KICHAA?,
Berry black & berry white?
Makamua?
K-sal? (kilio cha yatima)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…