Wajue watu katili zaidi Duniani

Wajue watu katili zaidi Duniani

hii miamba ndio ilitakiwa ishushwe iongoze tanzania kwa wakati mmoja itunyooshe
Maskini, sio kosa lako ni kitendo cha mababu zetu kuruhusu kutawaliwa na wakoloni ndio imeleta kizazi cha aina hii,

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Africa.
 
Maskini, sio kosa lako ni kitendo cha mababu zetu kuruhusu kutawaliwa na wakoloni ndio imeleta kizazi cha aina hii,

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Africa.
Kizazi kipi hiko ?
 
Mmh huyu khomenin alikua hatari mkuu maana aliua yeyote yule aliyetaka kuifanya iran iwe nchi ya kidemokrasia
Mohammad bin Salman kamuua Khashoggi, Israel inaua watu West Bank na Gaza strip. Saudi Arabia inaua watu Yemen, Bush na Blair waliivamia Irak kuondoa silaha za nyuklia ambazo hazikuwepo na kuua watu mpaka leo bado wapo. Libya walimuu Ghaddafi tokea 2011 lakini mpaka sasa hakuna amani wala hakuna serikali. Jeshi ka Uturuki liko uko, Israel ishapeleka silaha, US wana upande wao, Egypt wana upande wao, Italy wana ya kwao, vurugu tupu kama chandimu.

Wote hao waliohusika hakuna anayeitwa gaidi wala muuaji. Ila mpaka leo Ghaddafi anaonekana adui na Bush ni shujaa.
 
mkuu "poor brain" moja ya sababu inayotufanya tusiendelee kama taifa ni ukosefu wa viongozi wa kaliba hii.viongozi wengi ni wafuata mkumbo,kumbuka tukio la mzee wetu wa loliondo mwanzoni tu wizara ya afya ilitahadharisha wananchi wakaanza kulalamika mitaani na mitandaoni ikiwemo humu jf kwamba babu aachwe ila serikali imwandalie mazingira.Hapo serikali ikakosa msimamo
Magufuli anapigania mikataba ya madini itunufaishe watu wanalalamika huku wakimwita kila jina baya na kumwombea mabaya
NAONGEZA SAUTI EEE MWENYEZI MUNGU TURUDISHIE HAO WABABE DUNIANI ILA SAFARI HII WASHUKIE TANZANIA,waungane na huyu tulienae WATUNYOOSHE
 
Yas kifo ndo mbabe wa wote kwa kweli, japo najiulizaga hv inakuaje mtu kuwa na roho ya kikatili kiasi kile. Kwa sasa wapo kama hawa ?
Wengi Sana Kama watu wanawasomesha namba wenzao,wanateka wenzao,wanawabambika wenzao,wanawalaza wenzao ndani miaka 7 eti upelelezi haujakamilika si ndo walewale uzao mmoja.Roho mbaya Mara nyingi utokana hasa Kama mtoto alipatikana kwa madawa ya waganga kule unapewa kiumbe nusu binadamu nusu shetani Kimwili ni mtu kiroho ni shetani.
 
mkuu "poor brain" moja ya sababu inayotufanya tusiendelee kama taifa ni ukosefu wa viongozi wa kaliba hii.viongozi wengi ni wafuata mkumbo,kumbuka tukio la mzee wetu wa loliondo mwanzoni tu wizara ya afya ilitahadharisha wananchi wakaanza kulalamika mitaani na mitandaoni ikiwemo humu jf kwamba babu aachwe ila serikali imwandalie mazingira.Hapo serikali ikakosa msimamo
Magufuli anapigania mikataba ya madini itunufaishe watu wanalalamika huku wakimwita kila jina baya na kumwombea mabaya
NAONGEZA SAUTI EEE MWENYEZI MUNGU TURUDISHIE HAO WABABE DUNIANI ILA SAFARI HII WASHUKIE TANZANIA,waungane na huyu tulienae WATUNYOOSHE
Kuukimbiza tu upepo tangu umeanza kunyooshwa we pasi.Hayo ni mawazo ya uncivilized society.Umewahi ona wapi mwanadamu aliwahifaulu kunyoosha mwanadamu mwenzake
 
Iko wazi usikitamani kiti Cha enzi muulize zito bia kumsahau sumae alikitaka kiti akaambiwa sumu haionjwi hii Kali ya Karne [emoji23][emoji1787][emoji2960]
kwa maana hiyo huo sasa si ni udikteta ndani ya chama mpaka kuuwana mkuu.
watu wa haki za binadamu wako wapi na kukemea uminywaji wa demokrasia ndani ya hiki chama?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohammad bin Salman kamuua Khashoggi, Israel inaua watu West Bank na Gaza strip. Saudi Arabia inaua watu Yemen, Bush na Blair waliivamia Irak kuondoa silaha za nyuklia ambazo hazikuwepo na kuua watu mpaka leo bado wapo. Libya walimuu Ghaddafi tokea 2011 lakini mpaka sasa hakuna amani wala hakuna serikali. Jeshi ka Uturuki liko uko, Israel ishapeleka silaha, US wana upande wao, Egypt wana upande wao, Italy wana ya kwao, vurugu tupu kama chandimu.

Wote hao waliohusika hakuna anayeitwa gaidi wala muuaji. Ila mpaka leo Ghaddafi anaonekana adui na Bush ni shujaa.
ajabu!
 
Habari wakuu
Kwa uchache nataka niwape historia fupi ya watu ambao ni katili na bado historia zao zinakumbukwa mpaka leo.

Dunia imewahi kukaliwa na watu mbali mbali. Wapo wanaozungumzwa kwa maadili yao mema na sifa zilizotukuka kuna kuna kundi linazungumzwa kwa uongozi wao mwema na pia kuna kundi linazungumzwa katika mtazamo hasi

Sasa turudi katika mada yetu husika hawa watu wafuatao walifanya karibia kila jambo la kuogopesha kwa namna walivyojisikia

01__JOSEPH STALIN

Alikua kiongozi wa chama cha kikomunist kuanzia mwaka 1922 mpaka mwaka 1953 alipo fariki dunia. Chini ya utawala wa stalin taifa la ukraine lilipitia katika adha kubwa sana ya njaa. Ila mbali na tatizo hilo pia katika utawala wake watu wengi walinyongwa kama matokeo ya sheria alizounda kwa ajili ya watu wengi walinyongwa kama matokeo ya sheria alizounda kwa ajili ya watu walioonekana na mawazo kinzani na yake

Mbali na watu wengi kufa na njaa kutokana na mfumo wake mbovu wa utawala ila pia katika enzi zile aliweza kunyonga watu zaidi ya mil60. Ni mtu aliyeogopesha kuanzia kauli mpaka matendo yake pia alifanya mauaji bila hata kujali haki za raia wake. Kiongozi huyu alibaki kuwa muovu na katili mpaka siku zao za mwisho

02__VLAD TEPES

Alikua mtoto wa mfalme wallachia wa romania kutoka mwaka 1448 mpaka mwaka 1476 Vlad anajulikana kama nguli na mkufunzi wa adhabu za kikatili duniani.

Miongoni mwa mateso makali aliyowai kuyatoa kwa wote walioonekana kumkosea ni kama yafuatayo:
Msumali wa kichwa, ukatajia wa viganja, kupofoa macho, kuwaunguza katika tanuri la moto wakosefu wake, kukata pua na masikio kukata sehemu za siri kwa wanaume hawa ni kwa wale waliokumbwa na makosa yanayohusiana na masuala ya kuchukua wake za watu. Pia alikua na kawaida ya kuwapika katika moto mkali watu waliokuwa na makosa mengine.

Katika vitabu vinavyoelezea utawala wao hakuna binaadamu wa kawaida anayeweza kuvisoma na kufurahishwa navyo. Alikua akifanya kila jambo la kikatili kwa binaadamu . watu walibanikwa , walichinjwa, na kupikwa bila hofu mwaka 1960 watu zaidi ya mil 1 walihukumiwa kuchomwa na visu katika enzi za utawala wake.

03__RUHOLLAH KHOMEIN

Kwa waarabu na wafuasi wa dini ya kiislamu hasa wale wa misimamo mikali hawawezi kumjumuisha kama binaadamu katili.

Huyu alikua kiongozi wa kidini katika taifa la iran kuanzia mwaka 1979 mpaka mwaka 1989 alikua kiongozi aliyekua mstali wa mbele kutoa adhabu na amri zinazo tafsiriwa kuwa ni za kikatili.

Wazinifu, wezi pamoja na wote waovu walipata habari yao katika taifa hilo la kiislamu. Halia hiyi ilizua hofu na uwoga kwa raia wa nchi za magharibi kwenda katika taifa hilo maana hakukua na bar wala uvaaji wa suruali hadharani kwa mwanamke na katika taifa hilo mwanaume wa kweli ni yule aliyekua akifuga ndivu.

Mwaka 1988 alitoa amri ya kuuwawa kwa wafungwa wa kijeshi waliokua wanapigana zidi ya serikali ya kiislamu. Aliua watu takribani 30,000 waliotaka kulifanya taifa hilo kuwa la kidemokrasia kwa kuamini kuwa kila dini ina haki ya kuongoza iran

Ilipofika june 4 mwaka 1989 baada ya kusumbuliwa na kutoka ndani kwa ndani kwa mda mrefu hatimaye kiongozi huyo alifariki dunia na kuacha simanzi katika taifa zima la iran huku mataifa ya magharibi hususani marekani, ufaransa na uingereza wakipendezwa sana na habari ya kifo chake..

04__ADOLPH HITLER

unamkumbukahuyu ? Katili aliyekua na kipaji hasa cha kuongoza kutoka katika familia masikini iliyomnyima elimu bora na maisha ya anasa mpaka kuwa mtu mzima

Adolph hittler alichaguliwa kuwa chancelor mwaka 1933 na kua kiongozi mwenye mamlaka makubwa zaidi ujerumani fuhrer mwaka 1934 mpaka mwaka 1945 inaposemwa alikufa

Mwishoni mwa vita ya pili ya dunia mteso kwa maadui zake na manyanyaso vilikua ni vitu vilivyopewa kipaumbele sana katika utawala wake. Ila tukio kubwa ni lile la kuwatesa na kuwauwa waisrael takribani milioni 6

April 30 mwaka 1945 baada ya kuona vikosi vyake vinazidiwa nguvu na majeshi ya adui, inasemekana adolph hitler aliamua kujiua kwa kujipiga risasi na mwili wake kutumbukia katika pipa la tindikali na mwili wake kuteketea kabisa

Anajulikana kwa jina la ivan IV pia alijulikana kwa jina la ivan the terrible. Alikua ni wakala mzuri wa kuvunja haki za binaadamu kutoka mwaka 1533 mpaka 1547. Ndiye alikua kiongozi wa kwanza wa urusi kuchukua haki za mfalme..

Niishie hapo kwa leo, kama kuna la kuongezea,,,,,

Mkuu nadhani umesahau kumtaja mjomba wake FaizaFoxy, yule Prince muuwaji wa Saudi Arabia aitwaye Mohammed bin Salman bin Abdulaziz Al Saud. Faiza anajuwa sifa zake zaidi ila hawezi kuja hapa kusema atamtetea tu na kusema anasingiziwa.
 
Back
Top Bottom