Wajue watu katili zaidi Duniani

Wajue watu katili zaidi Duniani

Habari wakuu,

Kwa uchache nataka niwape historia fupi ya watu ambao ni katili na bado historia zao zinakumbukwa mpaka leo.

Dunia imewahi kukaliwa na watu mbali mbali. Wapo wanaozungumzwa kwa maadili yao mema na sifa zilizotukuka kuna kuna kundi linazungumzwa kwa uongozi wao mwema na pia kuna kundi linazungumzwa katika mtazamo hasi

Sasa turudi katika mada yetu husika hawa watu wafuatao walifanya karibia kila jambo la kuogopesha kwa namna walivyojisikia.

01. JOSEPH STALIN
Alikua kiongozi wa chama cha kikomunist kuanzia mwaka 1922 mpaka mwaka 1953 alipo fariki dunia. Chini ya utawala wa Stalin taifa la Ukraine lilipitia katika adha kubwa sana ya njaa. Ila mbali na tatizo hilo pia katika utawala wake watu wengi walinyongwa kama matokeo ya sheria alizounda kwa ajili ya watu wengi walinyongwa kama matokeo ya sheria alizounda kwa ajili ya watu walioonekana na mawazo kinzani na yake.

Mbali na watu wengi kufa na njaa kutokana na mfumo wake mbovu wa utawala ila pia katika enzi zile aliweza kunyonga watu zaidi ya milion 60. Ni mtu aliyeogopesha kuanzia kauli mpaka matendo yake pia alifanya mauaji bila hata kujali haki za raia wake. Kiongozi huyu alibaki kuwa muovu na katili mpaka siku zao za mwisho

02. VLAD TEPES
Alikua mtoto wa mfalme Wallachia wa Romania kutoka mwaka 1448 mpaka mwaka 1476 Vlad anajulikana kama nguli na mkufunzi wa adhabu za kikatili duniani.

Miongoni mwa mateso makali aliyowai kuyatoa kwa wote walioonekana kumkosea ni kama yafuatayo:

Msumali wa kichwa, ukatajia wa viganja, kupofoa macho, kuwaunguza katika tanuri la moto wakosefu wake, kukata pua na masikio kukata sehemu za siri kwa wanaume hawa ni kwa wale waliokumbwa na makosa yanayohusiana na masuala ya kuchukua wake za watu. Pia alikua na kawaida ya kuwapika katika moto mkali watu waliokuwa na makosa mengine.

Katika vitabu vinavyoelezea utawala wao hakuna binaadamu wa kawaida anayeweza kuvisoma na kufurahishwa navyo. Alikua akifanya kila jambo la kikatili kwa binaadamu, watu walibanikwa, walichinjwa, na kupikwa bila hofu mwaka 1960 watu zaidi ya milion 1 walihukumiwa kuchomwa na visu katika enzi za utawala wake.

03. RUHOLLAH KHOMEIN
Kwa waarabu na wafuasi wa dini ya kiislamu hasa wale wa misimamo mikali hawawezi kumjumuisha kama binaadamu katili.

Huyu alikua kiongozi wa kidini katika taifa la Iran kuanzia mwaka 1979 mpaka mwaka 1989 alikua kiongozi aliyekua mstali wa mbele kutoa adhabu na amri zinazo tafsiriwa kuwa ni za kikatili.

Wazinifu, wezi pamoja na wote waovu walipata habari yao katika taifa hilo la kiislamu. Hali hiyo ilizua hofu na uwoga kwa raia wa nchi za magharibi kwenda katika taifa hilo maana hakukua na bar wala uvaaji wa suruali hadharani kwa mwanamke na katika taifa hilo mwanaume wa kweli ni yule aliyekua akifuga ndevu.

Mwaka 1988 alitoa amri ya kuuwawa kwa wafungwa wa kijeshi waliokua wanapigana dhidi ya serikali ya kiislamu. Aliua watu takribani 30,000 waliotaka kulifanya taifa hilo kuwa la kidemokrasia kwa kuamini kuwa kila dini ina haki ya kuongoza Iran

Ilipofika june 4 mwaka 1989 baada ya kusumbuliwa na kutoka ndani kwa ndani kwa muda mrefu hatimaye kiongozi huyo alifariki dunia na kuacha simanzi katika taifa zima la Iran huku mataifa ya magharibi hususani Marekani, Ufaransa na Uingereza wakipendezwa sana na habari ya kifo chake.

04. ADOLPH HITLER
Unamkumbuka huyu? Katili aliyekua na kipaji hasa cha kuongoza kutoka katika familia masikini iliyomnyima elimu bora na maisha ya anasa mpaka kuwa mtu mzima.

Adolph Hittler alichaguliwa kuwa chancelor mwaka 1933 na kua kiongozi mwenye mamlaka makubwa zaidi Ujerumani fuhrer mwaka 1934 mpaka mwaka 1945 inaposemwa alikufa.

Mwishoni mwa vita ya pili ya dunia mateso kwa maadui zake na manyanyaso vilikua ni vitu vilivyopewa kipaumbele sana katika utawala wake. Ila tukio kubwa ni lile la kuwatesa na kuwauwa waisrael takribani milioni 6.

April 30 mwaka 1945 baada ya kuona vikosi vyake vinazidiwa nguvu na majeshi ya adui, inasemekana Adolph Hitler aliamua kujiua kwa kujipiga risasi na mwili wake kutumbukia katika pipa la tindikali na mwili wake kuteketea kabisa.

Anajulikana kwa jina la Ivan IV pia alijulikana kwa jina la Ivan the terrible. Alikua ni wakala mzuri wa kuvunja haki za binaadamu kutoka mwaka 1533 mpaka 1547. Ndiye alikua kiongozi wa kwanza wa urusi kuchukua haki za mfalme.

Niishie hapo kwa leo, kama kuna la kuongezea.
Cecil Rhodes...falsafa zake ndiye zilimtia moyo hitler
 
Back
Top Bottom