Mkuu Kiranga, kushindwa kwa wabunge wa BMK kufanya kile walichotakiwa kufanya kunachagizwa na ukweli kwamba hao watu (wananchi) ambao wanatakiwa kufanyiwa hicho amabacho hakifanywi, hawahusiki moja kwa moja kuwaweka pale bungeni. Kwa hiyo, hawawajibiki kwao (wananchi) kwa namna yoyote ile.
Nimeshaligusia hili hapo juu. You have a valid point. Kwamba the further removed are they from their appointing mandate, the more diluted their sense of responsibility will be. I can go deeper into information theory and show how the nodes between the source of information and the recipient corrodes efficiency in the system. Huwezi kuwa unatoa copy ya copy ya copy with default settings halafu utegemee quality i improve.
I am not disputing that.
What I am disputing is the reductivist overgeneralization kwamba hawa watu hawawajibiki kwa wananchi kwa sababu aliyewateua ni rais, na wakichaguliwa na wananchi ndiyo tutapata fidelity of responsibility. Huyo rais anawajibika kwa nani? Hiyo katiba ni ya nani? Mbona tuna wabunge wa bunge la jamhuri wamechaguliwa na wananchi na hawana hiyo fidelity of responsibility?
In a serendipitously counterintuitive way, ukishaanza kwa kusema wabunge hawawajibiki kwa wananchi unawanyima wananchi nafasi ya kuwawajibisha. Unawapa legitimacy ya kusema "I serve at the pleasure of the president" kama utaondoa caveat nyingine ya kusema "the president serves at the pleasure of the president", at least in principle. And thus, they, by induction, serve at the pleasure of the people.
Mambo mengi wanayofanya ni yale ambayo ama yatamfurahisha yule aliyewateua au kikundi (chama) wanachotoka. Nafasi ya wananchi katika utunzi wa katiba hii, haitambuliki-ijapokuwa maoni waliyotoa ndiyo yaliyozaa hiyo rasimu wanayoijadili. Laiti kama wabunge hawa wangechaguliwa na wananchi, hata nafsi zingekuwa zinawasuta pale ambapo wanakwenda kinyume na maoni ya wenye katiba (wananchi).
There is a fallacy in this argument. And that fallacy is that kuchaguliwa na wananchi ni litmus test ya responsibility. Ingekuwa hivyo, bunge letu la siku zote lisingekuwa na indiscipline.
Kama nilivyoandika mwanzo hapo, suala la rais kuwa na mamlaka makubwa sana katika kuteua hawa wabunge ni la hatari. As a matter of fact mimi nimeanza kulisema hili suala la rais kuwa na madaraka makubwa hata kabla hii habari ya wabunge wa bunge la katiba. Nyerere mwenyewe aliyefaidika na hili alilisema kama jambo ambalo si zuri sana, alisema kama angetaka kuwa dikteta mbaya sana angeweza, ndani ya sheria. Leo hii rais hakatazwi kujimegea kipande chochote cha Tanzania na kuamua kufanya lolote analolitaka (kamkatia mshikaji wake Hashim Thabit kiwanja Obay bila maelezo, nani atamuuliza wakati katiba imempa mamlaka? Rais anaweza kuumba ofisi yoyote bila rhyme or reason, akampa mjomba wake asiye na kazi, ujuzi wala usomi, na huwezi kufanya lolote.
Tunategemea tu kwamba rais awe benevolent and self limiting with a lot of natural modesty. Siku tukipata kichaa aliyeficha makucha yake mpaka aupate urais tutajuta.
Kwa hiyo, mimi nitakuwa wa kwanza kupinga uhalali wa rais kuteua wabunge wa bunge la katiba. Especially kama rais huyo huyo ndiye mwenyekiti wa CCM. Vipi siku interests za CCM na interests za taifa zitakapogongana? Rais atateua watu kwa kigezo cha kutetea interests za nchi au interests za CCM? Wengine wanaweza kusema hiki ndicho kinatokea sasa.
Kwa hiyo, nikisema kwamba principle ya wabunge kuwa responsible kwa wananchi inabaki pale pale hata kama wabunge wameteuliwa na rais, simaanishi kutetea habari ya rais kuteua wabunge, namaanisha kwamba hata kama tunahitaji kumpunguzia rais madaraka na wabunge hawa wachaguliwe na wananchi - something that may prove impractical for a constitutional body like this in the middle of election seasons and all the other questions revolving around the hoopla of representation of religious bodies etc etc
Hii ni sawa kabisa na mfano wako uliotoa kuhusu baba na mtoto. Ili mtoto ajione kwamba anawajibika kwa baba, ni sharti huyo baba awe amemzaa mtoto husika. Maana yake ni kwamba, ukaribu wao wa kidugu, utamfanya mtoto ajisikie vibaya pale anapomuona baba yake akiteseka wakati anao uwezo wa kumsaidia.
Tukirudi kwenye mfano huo - nearing the territory of stretching an analogy here-, mtoto kuwajibika kumtunza baba, hakumzuii kutaka kumtunza babu aliyemzaa baba pia. Lakini pia, kama ni wajibu wa mtoto kumtunza baba, na imefikia wakati mpaka mjukuu inambidi azidishe kumtunza babu, inabidi tujiulize baba mbona hajamtunza babu?
Kwa maana nyingine, kilichotakiwa kutokea in principle hapa ni a chain of delegation. In principle, wananchi wamemchagua rais wakampa kazi ya kuangalia interests zao, rais akawateua wabunge wamsaidie kuangalia interests za wananchi. Basi kama kuna wabunge hawaangalii interests za wananchi, utakuwa na haki ya kuhoji si tu uzuri wa huu mfumo wa wananchi kum delegate rais awafanyie hii kazi (labda wabunge wanaweza kuwa na responsibility kwa wananchi zaidi kama watachaguliwa na wananchi moja kwa moja - natumai utakubali kodi itakayozidishwa kwako kama mwananchi ili kupata haki hii-) kwa hiyo concern yako ni genuine. Lakini inabidi pia tumuhoji rais kwa nini kateua wabunge ambao hawafanyi kazi zao, za kuwa deputies wa deputy wa wananchi?
The same case applies to BMK. Wabunge wa BMK hawaoni umuhimu wa kujali matakwa ya wananchi, kwa kuwa wananchi hawajahusika kuwachagua kuingia bungeni. Ndio 7bu wanajitahidi kulinda maslahi ya chama (kwa lengo la kumfurahisha mwenyeketi wa chama chao aliyewateua) kuliko maslahi ya wananchi ambao wametengwa mbali kabisa na katiba hii.
Ungekuwa na a stronger argument katika hili kama bunge letu la jamhuri ya muungano lingekuwa na tofauti kubwa sana katika kujali maslahi ya wananchi.
This is not to say nina support rais kuteua wabunge wa bunge la katiba.
It is just saying kwamba unaweza kupata gharama za uchaguzi, ukachagua wabunge wa baraza la katiba, karibu wote wakawa kina Dr. Maji Marefu, wataalamu wa sheria na mengine yanayohusika katika katiba moja kwa moja wasiwemo, ukaingia gharama za mamilioni ya dola, bila kupata responsibility unayoitaka.
Tanzania tuna utamaduni wa kutokuwajibishana na accountability kama alivyosema Amani Karume. Kuanzia kwenye familia baba hakosei. Wangapi washamshuhudia baba akiiomba samahani familia kwa kuikosea?
Mpaka hapo tutakapobadilisha utamaduni, huko mbele tunachuzana tu.Watu wakichaguliwa na wananchi au wakiteuliwa na rais hawatakuwa na tofauti kubwa sana kama hakutakuwa na la msingi litakalobadilika katika utamaduni wetu.
Waingereza wanasema "you can't teach an old dog new tricks". Mijitu imekulia katika clientelism for decades (CCM na upinzani), huwezi kusema itabadilika leo kwa sababu imechaguliwa na wananchi.
Ni kama kusema eti nywele za mtu zitaacha kuwa kipilipili siku zote eti kwa sababu kaweka relaxer mara moja!