kichongeochuma
JF-Expert Member
- Jan 21, 2024
- 1,669
- 2,864
Wajumbe najua wengi mpo humu na mnasoma haya na mnaziona harakati na vikao vya siri na vya wazi mnavyo endelea navyo huko mafichoni, sasa kama mtajichanganya shauri yenu na heshima ya chama chenu mliyo ijenga miaka yote itapotea kabisa ndiyo mtakuwa mnakiua kama vilivyo kufa vyama vingine.
Mkumbuke kuna watu wameuawa kwa ajili ya kutetea misimamo na imani ya hicho chama chenu, kuna waliolemazwa pia kwa ajili ya kusimamia misimamo ya hicho chama dhid ya udhalim wa serikali sasa kukubali rushwa na pesa za hongo ni kukinajisi sana chama hicho na hasa kwa namna kilivyo jijenga na kilivyo aminiwa huko duniani.