Wajumbe Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu (RAAWU) wamkataa mwenyekiti wao

Wajumbe Mkutano Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu (RAAWU) wamkataa mwenyekiti wao

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Kuna Mkutano Mkuu wa Baraza la Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Ufundi Stadi, Ushauri, Habari na Utafiti ambao unafanyika katika Hoteli ya Edema Manispaa ya Morogoro.

Lakini katika mkutano huo ambao umeanza majira ya saa mbili asubuhi leo tarehe 23 Machi 2023 baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu wamekuwa na malalamiko juu ya Mwenyekiti wao wa chama hicho Taifa, JANE MIANJI kwa tuhuma ya kuvunja katiba yao ya chama.

Kwa mujibu wa baadhi ya wajumbe wa mkutano huo niliozungumza nao wametoa hoja zao ambazo ni

-Je, Kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi RAAWU kuwa Kiongozi wa Chama cha siasa, Katiba imevunjwa?

-Katiba ya RAAWU ya mwaka 2009 - Ibara ya 15.7(b) - imesema Kiongozi wa Chama hatakuwa Kiongozi wa Chama cha siasa bali anaweza kuwa Mwanachama wa Chama cha siasa.

-Je, Sifa za Mgombea wa nafasi ya Uongozi wa RAAWU zinaruhusu kuwa Kiongozi wa Chama cha siasa

-Kanuni za Katiba ya RAAWU za mwaka 2005 - Kifungu cha 18.0 imeeleza Sifa za Mwanachama anayeweza kuwa Mwenyekiti wa Chama na imeweka wazi Kiongozi wa nafasi ya kisiasa hawezi kuwa hata Mgombea.

-Je, Miiko ya RAAWU inazuia Kiongozi wake kuwa Kiongozi wa Chama cha siasa?

-Kanuni za Katiba ya RAAWU za mwaka 2005 - Kifungu cha 22.2 - Kimeeleza pia Miiko ya Viongozi wa Chama kuwa hawatakiwi kuwa Kiongozi wa Chama cha siasa.

-Je, Mjumbe ni Kiongozi? au Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM na JUMUIYA zake ni nani?

-Katiba ya CCM ya mwaka 1977 ibara ya 16 imeeleza vyema Kiongozi ni Mwanachama yeyote mwenye dhamana ndani ya CCM aliyechaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa Katiba.

-Je, UWT inatambuliwa na Katiba ya CCM au ina uhusiano na CCM?

-Katiba ya CCM ya mwaka 1977 ibara ya 124 imeeleza wazi uhusiano wa UWT na CCM

-Je, Katiba ya UWT inaundwa kwa kuzingatia Katiba ya CCM na UWT ipo ili kuongoza Utekelezaji wa shughuli za CCM?

-Katiba ya CCM ya mwaka 1977 sehemu ya mwisho, Nyongeza B imeainisha list ya Katiba zinazoundwa kwa ajili ya Utekelezaji wa Katiba ya CCM ikiwepo UWT.

-Je Baraza kuu linayo Mamlaka ya kumsimamisha Kiongozi wa RAAWU

Katika Ibara ya 15.8 (a) na (b) inatoa Mamlaka kwa Baraza Kuu ya kumsimamisha Kiongozi aliyevunja Katiba au Miongozo ya Chama. Na imeeleza Baraza kuu likimsimamisha uamuzi utaanza mara moja na Kiongozi aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu atasubiri Maamuzi ya Mkutano Mkuu.

Baada ya Hoja hizo wajumbe wanasubiri hatma ya suala hilo katika mkutano wao utakao endelea leo na kesho.

Lakini pia inaonekana wajumbe wengi wanapingana na Mwenyekiti wao wakishinikiza aachie nafasi hiyo kwa kuvunja katina.
 
Bora wao wamethubutu!CWT imejaa mapandikizi ya Ccm Kila Kona.Wamekuwa butu hata maamuzi ya kutetea maslahi ya walimu hawawezi kuchukua.Wakikutana ni kudumisha fikra za mwenyekiti tu[emoji45]
 
Back
Top Bottom