Wajumbe: Tunamtaka Samwel Sitta

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Wajumbe wengi wa Bunge la Katiba wamesema kuwa wanamtaka Samwel Sitta kama Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge hilo. Wakizungumza nami kwa nyakati tofauti hapa Dodoma,Wajumbe hao waliojipachika jina la WAJUMBE HURU (WAHU) wamesema kuwa katika kuchagua kiongzi wao,hakuna chama wala mtu atakayewayumbisha.

WAHU walifanya vikao vyao mbalimbali jana usiku na leo asubuhi katika maandalizi ya kumchagua Samwel Sitta kama Mwenyekiti wao juma lijalo. WAHU inaundwa na Wajumbe ambao ni Wabunge,Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Wajumbe wateuliwa na Rais.

'Sisi tunamtaka Sitta. Hakuna zaidi.Hata jina lake lisipoletwa Bungeni,tutampigia kura za wingi na ikiwezekana zote. Huu si wakati wa kuchaguliwa na kuongoozwa kwa kila kitu. Sisi ni Wajumbe huru.Itambulike hivyo' alisema mmoja wa WAHU. 'Wao watuletee yeyote,sisi tutamchagua Sitta. Tunajua hapa mpo mtakaopeleka habari.Pelekeni na mseme kuwa tunamtaka Sitta kama Mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Kila mtanzania ajue hivyo' aliongeza mwana-WAHU wakati wa kikao chao.

Je, itawezekana WAHU kuibuka washindi katika hili? Tusubiri na kujionea

Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodooma)
 
Mbele ya jembe Samwel Sitta,Tanganyika yetu lazima irudi!
 
WAHU.. nao. mhhh

tusubiri jumatatu nani amtashinda kati ya kura ya wazi na kura ya siri..? na sijui watumia kigezo gani kuamua..? maana kama watatumia kura je watapiga kwa uwazi au kwa siri kuamua kura ya uwazi au ya siri... hahaha
 
WAHU inawanachama takriban wangapi ?, Yaani kwenye huo mkutano wao walihudhuria wajumbe wangapi
 
Sitta ni mnafiki kama wewe MZEE TUPATUPA
 
In Sitta i trust,This is the most honest politician i have ever known.Sitta,You deserve to lead the Parliament into getting a better constitution,Only You,Remember!!??With you in the chairnmanship seat my beloved Tanganyika will come back!!
 
Mzee wewe huwa nakuaminia katika mabandiko yako. Swali ni je, uliozungumza nao ni kutoka vyama vyote vya siasa au ni upande mmoja wa wanaotaka kura za wazi?
 
Nani zaidi ya Sitta jamani pale bungeni? Sioni kichwa cha kuliongoza Bunge la Katiba zaidi ya Mzee Samuel John SITTA. Mzee ana sifa zote. Anakubalika na wabunge wengi wa CCM na wajumbe 'wote' 201 walioteuliwa na rais. Watanzania tunataka Sitta aongoze CA. CCM msituangushe tena kwa kuendekeza mabifu ya kitoto kama safari ile mlipomuweka 'kimeo' Makinda!
 
WAHU inawanachama takriban wangapi ?, Yaani kwenye huo mkutano wao walihudhuria wajumbe wangapi
Kwa mujibu wa nyaraka wanazozimiliki,WAHU ina wanachama wasiopungua 300

Mzee Tupatupa

 
Bila ushabiki wa kimtandao wa kichama; Sitta ndio ataweza midahalo ya katiba mule ndani. Kile kiti kinataka mtu madhubuti ambaye hana upendeleo wa kijinga.. Hebu tumpe nafasi kwa mara nyingine atusaidie katika hili zoezi nyeti la uundwaji wa katiba ya nchi hii.. Anaweza akawa na mapungufu mengine kama mwanadamu halisi, lakini kwa kutazama the big picture, jamaa yuko vizuri kwenye kuongoza vikao..
 
Sheria hii ya Mabadiliko ya Katiba hairuhusu Mwenyekiti achaguliwe kutoka nje ya Wajumbe wa Bunge hili la Katiba? Huku nje vipo vichwa vizuri tu ambavyo havijatafunwa na siasa za vyama na makundi ya Urais na visasi kama Issa Shivji.

Samwel Sitta hajatulia na hatabiriki kabisa.
 
Mzee wewe huwa nakuaminia katika mabandiko yako. Swali ni je, uliozungumza nao ni kutoka vyama vyote vya siasa au ni upande mmoja wa wanaotaka kura za wazi?
Kamanda Royals,WAHU ina Wajumbe toka vyama vyote na Taasisi zote hapa Dodoma Bungeni.Sasa wamefika 300

Mzee Tupatupa
 
Last edited by a moderator:
Kwa mujibu wa nyaraka wanazozimiliki,WAHU ina wanachama wasiopungua 300

Mzee Tupatupa


Okay Good...., Lakini isije ikawa hio WAHU ndio ikabadilika na kuanza kuchagulia na kuamulia maamuzi watu (na sio individual decisions) yaani yale tuliyoyakataa CCM ya kuwapangia watu maamuzi yakaamia WAHU
 
Sita ndiye anakwenda kuwa mwenyekiti hilo alina mjadala hata ccm hapo wamenyanyua mikono
Chenge akijaribu kugombea habari yake kwisha ccm watalia kilio cha mbwa mwitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…