Wajumbe: Tunamtaka Samwel Sitta

Wajumbe: Tunamtaka Samwel Sitta

Mzee Tupa Tupa uko vizuri kwa kutuletea News za kutoka Dom kwenye Bunge la Katiba Japo unaonekana wewe u Gamba Sugu lenye sumu kali.
 
Wajumbe wengi wa Bunge la Katiba wamesema kuwa wanamtaka Samwel Sitta kama Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge hilo. Wakizungumza nami kwa nyakati tofauti hapa Dodoma,Wajumbe hao waliojipachika jina la WAJUMBE HURU (WAHU) wamesema kuwa katika kuchagua kiongzi wao,hakuna chama wala mtu atakayewayumbisha.

WAHU walifanya vikao vyao mbalimbali jana usiku na leo asubuhi katika maandalizi ya kumchagua Samwel Sitta kama Mwenyekiti wao juma lijalo. WAHU inaundwa na Wajumbe ambao ni Wabunge,Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Wajumbe wateuliwa na Rais.

'Sisi tunamtaka Sitta. Hakuna zaidi.Hata jina lake lisipoletwa Bungeni,tutampigia kura za wingi na ikiwezekana zote. Huu si wakati wa kuchaguliwa na kuongoozwa kwa kila kitu. Sisi ni Wajumbe huru.Itambulike hivyo' alisema mmoja wa WAHU. 'Wao watuletee yeyote,sisi tutamchagua Sitta. Tunajua hapa mpo mtakaopeleka habari.Pelekeni na mseme kuwa tunamtaka Sitta kama Mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Kila mtanzania ajue hivyo' aliongeza mwana-WAHU wakati wa kikao chao.

Je, itawezekana WAHU kuibuka washindi katika hili? Tusubiri na kujionea

Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodooma)

Haya mkuu acha hayo WEHU wajipange tuona mtanange wiki ijayo .
 
Kamanda Royals,WAHU ina Wajumbe toka vyama vyote na Taasisi zote hapa Dodoma Bungeni.Sasa wamefika 300

Mzee Tupatupa
Mzee Tupatupa.
Ikiwa wajumbe watajenga misimamo kama hii, na jana kuna au juzi kulikiwa na bandiko la akina "tunataka katiba ya wananchi" ikiwa Sita atapita, na ikiwa wale wanaokomalia "kura zisizo na nguo" wakishindwa si huo utakuwa ndio mwanzo wa kuzaliwa taifa jipya lenye nguvu na mshikamano mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Sitta , chama kitamwambia sasa huu ni wakati wa Mwanamke .....Asha atakatiza ........
 
Hii imekaa vizuri sana. Apewe Mh. Sitta lakini pia ajue hiki ni kipimo kizuri kwake kama kweli anafaa au hatufai kama ataingia kwenye kile kinyang'anyiro cha kuelekea Magogoni. Akifanya vema, itampa heshima kubwa na kumjengea jina, ila akiendesha Bunge hili kwa ushabiki wa kichama, ajue ndio imekula kwake jumla!!!!
 
Sitta ni zaidi ya wanasiasa wengi wa ccm huwa anawatingisha hata wakubwa zake
 
Samwel 6 ni Makini kuliko Chenge kwa mbaliiiii.
 
Wajumbe wengi wa Bunge la Katiba wamesema kuwa wanamtaka Samwel Sitta kama Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge hilo. Wakizungumza nami kwa nyakati tofauti hapa Dodoma,Wajumbe hao waliojipachika jina la WAJUMBE HURU (WAHU) wamesema kuwa katika kuchagua kiongzi wao,hakuna chama wala mtu atakayewayumbisha.

WAHU walifanya vikao vyao mbalimbali jana usiku na leo asubuhi katika maandalizi ya kumchagua Samwel Sitta kama Mwenyekiti wao juma lijalo. WAHU inaundwa na Wajumbe ambao ni Wabunge,Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Wajumbe wateuliwa na Rais.

'Sisi tunamtaka Sitta. Hakuna zaidi.Hata jina lake lisipoletwa Bungeni,tutampigia kura za wingi na ikiwezekana zote. Huu si wakati wa kuchaguliwa na kuongoozwa kwa kila kitu. Sisi ni Wajumbe huru.Itambulike hivyo' alisema mmoja wa WAHU. 'Wao watuletee yeyote,sisi tutamchagua Sitta. Tunajua hapa mpo mtakaopeleka habari.Pelekeni na mseme kuwa tunamtaka Sitta kama Mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Kila mtanzania ajue hivyo' aliongeza mwana-WAHU wakati wa kikao chao.

Je, itawezekana WAHU kuibuka washindi katika hili? Tusubiri na kujionea

Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodooma)

Tupa tupa wambie sisi tunataka tanganyika yetu
 
Mbona nilisoma mahali humu kwamba Sitta ni muumini wa SERIKALI MBILI wakati Chenge ni wa SERIKALI TATU?

Je, ni kweli?
 
Sita ndiye anakwenda kuwa mwenyekiti hilo alina mjadala hata ccm hapo wamenyanyua mikono
Chenge akijaribu kugombea habari yake kwisha ccm watalia kilio cha mbwa mwitu.
Lusinde Livingstone amependekezwa M/kiti
 
Ah this is not fair.... ina maana Mhe Getrude Rwakatare amesahaulika?? Sikubaliani na hili, she is simply the best, kipenzi changu mama Rwakatare watu wanakubania sana usijali lakini endelea kulisongesha
 
Sheria hii ya Mabadiliko ya Katiba hairuhusu Mwenyekiti achaguliwe kutoka nje ya Wajumbe wa Bunge hili la Katiba? Huku nje vipo vichwa vizuri tu ambavyo havijatafunwa na siasa za vyama na makundi ya Urais na visasi kama Issa Shivji.

Samwel Sitta hajatulia na hatabiriki kabisa.

Issa Shivji wa sasa, kopo kabisa, wamekwisha kumchakachua, siyo yule wa zamani! Shivji wa sasa anayemponda jembe Warioba, hatufai katu, apotelee kwa mbali!
 
Back
Top Bottom