Wajumbe: Tunamtaka Samwel Sitta


Hapo kwenye Red ndio msimamo nilioupenda, maana CCM kwa kujifanya wanajua kuepusha shari wangeweza kuwatosa wote, yani Chenge na Sitta ili tu kumkomoa Mzee Six.......sasa kwa huo msimamo wa hao WAHU, naiona bendera ya Tanganyika ikipepea Mlima Kilimanjaro.........
 

Huyu 6 damu ya Chama cha Mapinduzi imo ndani ya mishipa yake, hawezi kuwa mtu mzuri katika nafasi hiyo, hatokuwa na tofauti yeyote na yule bibi Kiroboto makinda., akisimama mpinzani kujenga hoja atamlazimisha akae kitako kwa nguvu au ataita askari wa bunge atolewe nje., 6 hafaiii.,
 
Hivi ukitaka kugombea uenyekiti wa bunge la katiba lazima upitie kwenye vyama? Kama ni hivo basi tuna safari ndefu watanzania!
 
wanaweza kumpa Asha , ila nina wasi wasi hana proven record ya kusimamia mijadala ya bunge na kuwa partial, sasa hakiharibu na bunge la katiba ni once in 50 yrs?
 
Mbele ya jembe Samwel Sitta,Tanganyika yetu lazima irudi!

hahahhahaha, sahau Tanganyika mbele ya wana CCM. Sitta mwenyewe haitaki Tanganyika umesahau siku alisema serikali tatu ni mzigo mkubwa kwa wananchi? asijue kuwa serikali mbili siyo mzigo bali ni kisu kooni mwa Watanganyika. Ningekuwepo huko kwenye bunge ningesimamia serikali tatu na ningesema tu tuwe na rais mmoja wa Jamhuri. Tanganyika iongozwe na waziri mkuu, na Zanzibar iongozwe na Waziri mkuu. Rais mmoja Mawaziri wakuu wawili. Kwisha kazi. Hakuna gharama ya marais watatu japo kwa sasa bado gharama ipo pale pale kwa kuwa kuna Rais wa Muungano, Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Muungano. Ni wangapo hao? Kule zanziber ndo kali zaidi kwani kuna makamu wawili wa Rais, wa kwanza ni wa Cuf na wa pili ni wa CCM. Hivyo havionwi na wanasiasa.
 
Msimamo wa sitta ni serikali tatu, rais mmoja. Kwa mtazamo huu, atakuwa angalau fair kwa pande zote.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Msimamo wa sitta ni serikali tatu, rais mmoja. Kwa mtazamo huu, atakuwa angalau fair kwa pande zote.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Kwa kumbukumbu zangu sijawahi kumsikia huyo 6 akiunga mkono serikali tatu hadhalan labda mafichoni!
 
Issa Shivji wa sasa, kopo kabisa, wamekwisha kumchakachua, siyo yule wa zamani! Shivji wa sasa anayemponda jembe Warioba, hatufai katu, apotelee kwa mbali!

Haswaa nakuona GT pale unapogongana mawazo na mimi, hilo zee shivji nowdayz bure kabisa
 
Labda JK aingilie kati, bila hivyo SITTA atajengewa mikwala mpaka watu tutabaki midomo wazi, kumbuka jinsi mama Makinda alivyo kuja kuteuliwa nafikiri na yeye alishangaa alipo pendekezwa - yote hayo zilikuwa ni mbinu za kumu-contain Mzee Sitta, wahusika wakuu wa sakata hilo bado wapo - we unafikiri safari hii hawawezi kuwa na mbinu mdalada ya kurudia mchezo huo huo wa kumukwamisha, sisi watu wa ajabu sana - hawajali mstabali wa Taifa hili wanajali maslahi yao tu sio Taifa letu, mambo mengi wanayo sema ni michezo ya kuigiza, na hili JK aliwahi kutoa onyo lakini watu wengine vichwa ngumu wanamu-ignore tu, at the end of the day tuta end up bila katiba mpya au marekebisho yoyote kutokana na malumbano ya kitoto tu - kumbe wanacho taka katika hii ni katiba hii endelee ili Rais wa mwaka 2015 hawe dikteita kama Stalin - ndio!

Hata Kambarage aliwahi kusema katiba iliyopo ikimkuta Rais ambaye ana dalili za kunyanyasa watu by default, katiba hii inaweza kumfanya kuwa Super/Mega Dictator - thank God JK hayuko hivyo, watanzania wenzangu tuwe wakweli mambo yanatisha sana, hivi zama hizi Watanzania wengi wame elevuka kwa kiwago cha hali ya juu sana - kwa nini watu wachache tu wenye ajenda zao zisizo eleweka wapendelee kuburuza the entire Nation kwenye dire straits - wala hilo hawalioni, hawe endani na wakati hata kidogo na wengi wao si wakweli - watu wanaitwa kuhojiwa seriously hili Taifa letu/chama chao kiwe na amani, wakitoka huko baadhi yao wanadanganya watu eti walikwenda kunywa chai na kutoa ushauri as if chama chao akina mkono mrefu wa kungamua mbinu zao za chinichini ambazo zinaweza kabisa kuhatarisha amani ndani ya chama chao na Taifa letu kiujumla, hilo hawalioni mimi hawa nawaogopa sana kwenye chama chetu kuliko kitu kingine, nashukuru NEC kuwaweka where they belong na kueleza ukweli wa mambo na siyo kuzuga watu.
 
Kura ni siri ya MTU jaman so iwe siri na sitta kuwa mwenyekiti is impossible kwa thz time ......
 
Kama anazo sifa wampe tu kwani tatizo liko wapi kama anaweza?
 
Samwel John Sitta bhaasiii,
chaguo sahihi
 
Mbele ya jembe Samwel Sitta,Tanganyika yetu lazima irudi!

Hana lolote naye ---- tu aheshimu maoni ya wananchi wamchague wajute na hivi anataka urais hawezi tena kwenda against na sera yao anaogopa watamtema kama uspika
 
Mbele ya jembe Samwel Sitta,Tanganyika yetu lazima irudi!
Six poa lakini na yeye anautaka urais wa jamhuri. Mnadhani atakwenda kinyume na sera ya chama chake? Wanaopenda serikali mbili wasiwe shaka na six kwani bila ya shaka atatumia busara na hekima kufanya wajumbe waone mfumo wa mbili ndio salama kwa umoja wa jamhuri yetu tukufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…