Wajumbe tupeane "connections"

Wajumbe tupeane "connections"

Others

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2013
Posts
1,189
Reaction score
2,765
Habari za muda huu 'Wajumbe'.

Heshima yenu nawapa...

Nimekaa na kufikiria sana, nikagundua karibia kila mtu anahitaji mtu mwingine kwa ajili/sababu flani flani ili kuwezeshana kufika mahala fulani.

Maisha ni kutafuta na kutegemeana. Hivyo basi, hata uwe katika hali nzuri sana 'Title', hali ya 'Uchumi wa Kati' au hata katika hii hali yetu tulio wengi ya 'Pangu pakavu, tia mchuzi'. Bado utahitaji mtu wa kukusaidia au wewe kumsaidia au rafiki wa kuongea nae na wakati mwingine hata Best fulani wa 'Mchongo', Friend with benefits, Mtu wa kunywa nae. Aidha Mpenzi au pia upo Mkoa flani au unasafiri Mathalani Mkoani au Mijini humo ukiulizia jukwaani humu hutokosa au lazima utampata tu wa kushare nae good or bad times.

Tushirikiane hasa katika Kipindi hichi kigumu cha 'Mpando wa Mafuta', 'Mfumuko wa Bei' na 'Mapambano ya Kimaisha'. Tushikamane na tushikane mikono Bandugu. 🤝

Humu duniani pekeyako pekeyako utafika kwa kuchelewa na ukiwa umechoka sana. Funguka, tufungukiane tupeane hayo Makoneksheni.

Naomba kuwasilisha 'Bandugu zangu Ba Mutu Ba Bungeni, Bajumbe!'

Nokia-Connecting-People-1.jpg
 
Ndugu yangu wewe unataka connection gani hasa kama nimbeba zege upate connection ya wabeba zege wenzio, kama nidalali upate connection za madalali wenzio
 
enzi za magufuri liliibuka kundi flani lililokuwa na roho mbaya lilikuwa na kamsemo kake "pambana na hali yako"....lakini kwa huyu mama wa kizenji anaejitahidi kuwafuta machozi watumishi wa serikali pamoja na wengineo...nakuapia tegemea kupata bonge la connection kabla ya huu mwaka haujapinduka...
 
Na mimi nazamia katika hiyo Baraka Mkuu.
 
Ndugu yangu wewe unataka connection gani hasa kama nimbeba zege upate connection ya wabeba zege wenzio, kama nidalali upate connection za madalali wenzio
Kawaida Connection haiangalii wewe ni nani au unaweza kufanya nini... Zaidi inaangalia uhitaji wa mtoa connection and not exactly specific of a receiver.
 
enzi za magufuri liliibuka kundi flani lililokuwa na roho mbaya lilikuwa na kamsemo kake "pambana na hali yako"....lakini kwa huyu mama wa kizenji anaejitahidi kuwafuta machozi watumishi wa serikali pamoja na wengineo...nakuapia tegemea kupata bonge la connection kabla ya huu mwaka haujapinduka...
AMINA KUBWA SANA MTUMISHI.🙏🏽
 
Back
Top Bottom