Wajumbe tusaidiane mwenye connection ya kazi au internship ya ualimu wa English na Kiswahili

Wajumbe tusaidiane mwenye connection ya kazi au internship ya ualimu wa English na Kiswahili

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau..!!

Mambo yamekuwa magumu maana wife anatafuta nafasi ya internship au kazi ya kufundisha masomo ya lugha kwa DsM.

Mwenye connection ya kibabe tuyajenge ,maana mjini hapa kama hauna connection hata kwenye msiba unaweza usile.

Nawaombeni wadau tusaidiane kwenye hili jamani,maana anatia huruma amekuwa kama mlinzi wa geti nikiondoka asubuhi namuacha nikirudi namkuta.
 
Kwanini usimfungulie shule hizi za chekechea?
 
Nimecheka kama mazuri,eti bila connection unaweza usile msibani[emoji23]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Usicheke mambo yapo ,juzi bi mkubwa kaenda kwenye msiba uswahilini fulani huko hakula watu wakamkung'utisha mikono maana kilipikwa kitu cha ubwabwa ww umeona wapi ubwabwa msiba wa uswahilini hapo hautii mkono km haumjui mtu.
 
Hilo nalo wazo ila kufundishq watoto ni kipaji baba .I will take your advice nitaanza kumtafutia eneo la kukodi .
Kama una mtaji wa kukodi au kujenga ka hall kadogo kama darasa hivi,..ndani ya mwaka mmoja tu atakuwa mbali mno.
 
Kama una mtaji wa kukodi au kujenga ka hall kadogo kama darasa hivi,..ndani ya mwaka mmoja tu atakuwa mbali mno.
Wazo zuri ila mabanda mazuri ni yale ya vibanda umiza,ngoja nianze msako wa kuyasaka ambayo hayatumiki asubuhi🤔🤔🤔🤔🤔
 
Kama una mtaji wa kukodi au kujenga ka hall kadogo kama darasa hivi,..ndani ya mwaka mmoja tu atakuwa mbali mno.
Easy said..

nina rafiki alifungua kaishia wanafunzi watatu na anatakiwa kurenew mkataba
 
Easy said..

nina rafiki alifungua kaishia wanafunzi watatu na anatakiwa kurenew mkataba

Maisha ni kujaribu,biashara pia zina mambo mengi haupaswi kuanza biashara kienyeji au kimazoea labda kama ukoo wenu hakuna wazee😂😂😂😂
 
Maisha ni kujaribu,biashara pia zina mambo mengi haupaswi kuanza biashara kienyeji au kimazoea labda kama ukoo wenu hakuna wazee

Maisha ni kujaribu,biashara pia zina mambo mengi haupaswi kuanza biashara kienyeji au kimazoea labda kama ukoo wenu hakuna wazee😂😂😂😂
kama wazee wanakusaidia kupata wateja na kushawishi mzazi kuandikisha mtoto shule mpya ni Sawa,
 
Back
Top Bottom