Wajumbe wa bodi zote sensitive nchini ni wazee, wana maarifa lakini wanakosa utandawazi; nini kifanyike wasiendelee kuwa watia sahihi?

Wajumbe wa bodi zote sensitive nchini ni wazee, wana maarifa lakini wanakosa utandawazi; nini kifanyike wasiendelee kuwa watia sahihi?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kila siku ukisikia wajumbe wa bodi wameteuliwa utasikia huyu kustaafu kule na yule kustaafu huku.

Wanaosimamia mipango ya nchi wanapoteuliwa wote unabaini walishastaafu.

Lakini unapokwenda kwenye mashirika binafsi yanayoganya vizuri katika private sector Duniani utabaini wenye mamlaka kamili ni vijana kati ya miaka 20 hadi 45.

Je, Tanzania tunaamini wazee watatutoa hapa tulipo? Tumeziacha wapi fikra za akina Mwalimu Nyerere zilizochukua vijana kama Salimu Ahmmed Salimu kuwa viongozi Afrika?

Ni lini tumekuwa disappointed na vijana?Kwanini wanaotumbuliwa kwa utendaji mbovu au wanaonyomwa kura wawe wajumbe wa bodi? Tumekosa vijana wakuwapa kazi? Tumeshindwa hata kufanya hata mgawanyo basi tuwe na succession plan kwamba bodi yenye wajumbe saba
1. Wazee above 60 wawe wawil kwa mgawanyo wa jinsia
2. Wazee between 50 and below 60 awepo mmoja
3. Wazee between 40 to 50 awepo mmoja
4. Vijana between 20 to 40 wawepo watatu

Kwa mgawanyo huu utagundua vijana wengi zaidi watapata muda wa kujifunza wanapoelekea kuchukua madaraka makubwa.

Lakini mfumo wa sasa wakujaza wazee kwenye bodi nyeti kama ya TANESCO, Nishati na mashirika sensitive utagundua hakuna new ideas zinazozaliwa. Lakini pia utagundua tunaweka watu ambao walishachoka kusoma badala yake wanawaza kusomewa na kusaini.

Tufanye reform kwenye nafasi hizi tutumie vijana bila kuwaacha wazee kwa kuzingatia ukweli kwamba vijana wanayo mengi ya kujifunza kwetu wazee
 
Uko sahihi succession plan hamna kwenye bodi wamejaza vizee vikongwe vitupu vinasinzia tu kwenye vikao vya bodi vikisubiri posho tu
 
Back
Top Bottom