Wajumbe wa CHADEMA muumbueni Mbowe utakapotaka kuwanunua

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Hakuna namna Mbowe anaweza kumshinda Mh.Lissu zaidi ya kununua wajumbe na kuiba kura. Wajumbe wengi wameonyesha kutokubali Mbowe kujimilikisha chama.

Kama huyu mtu amekosa aibu kabisa basi na sisi tusimuonee aibu kwa vyovyote. Tumuanike popote bila aibu anapotaka kununua mjumbe yeye mwenyewe au mawakala wake. Hakuna siri katika uchaguzi, iwe ukitaka kununuliwa wewe au mjumbe mwenzio toa taarifa kwa umma.

Hakuna haja ya kusubiri uchaguzi uishe, bali wakati ni sasa.
 
Au wachukue hizo hela, ajiaminishe atashinda then wamchinje na kwenye sanduku la kura.
 
😝Akili zenu ni finyu sana yani Lisu na akina dr slaa na maria sarungi wamshinde Mbowe
 
Muda utaongea kati ya wanaharakati wapiga kelele wa Twitter na watu wanaofanya siasa seriously
Siasa ya kung'ang'ania Uwenyekiti kwa zaidi ya miaka 20 au unaongelea siasa gani?
 
Muda utaongea kati ya wanaharakati wapiga kelele wa Twitter na watu wanaofanya siasa seriously
Mbowe amefanya siasa seriously kwa miaka 20 iliyopita lakini kwa sasa amefikia ukomo wa kufanya siasa za ushindani anatakiwa awe mshauri tu awaachie wengine waende front. Maridhiano na Samia yamempunguza sana nguvu ya kupambana na CCM hii iliyojaa ulaghai.
 
Hio ni hoja dhaifu,kama uwezo upo anaweza endelea
Mfuateni lisu atakapoamia Act,akagombane na Zito tena πŸ˜€
 
Hio ni hoja dhaifu,kama uwezo upo anaweza endelea
Mfuateni lisu atakapoamia Act,akagombane na Zito tena πŸ˜€
Chawa wa Sultan mnajitoa ufahamu sana. Kama huoni kuwa uwezo wa Mbowe kupambana na CCM umepungua basi ukapimwe akili,hata kilichotokea kwenye uchafuzi wa serikali za mitaa huoni sasa nitabishana na wewe wa nini.
 
πŸ™†Kwa hio nyie mnajifungia ndani na wake zenu,mnategemea mbowe au lisu ndio wapambane na ccm?😝😝

Mmejaa humu kazi kuandika andika tu na kuwalaumu wakiwaita kuandamana hamtaki kutokea kabisa,kama ni rahisi nenda field kapambane wewe uone moto πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…