wajumbe wa tume ya katiba mpya wajitengenezea ulaji mwingine.

Logatho Mwolokujova

Senior Member
Joined
Apr 27, 2013
Posts
116
Reaction score
18
Kwanin wameamua kuja na pendekezo la serikali tatu ilihal wananch hawakuambiwa kama muundo utakuwa hv? wanataka waendelee kuandika rasimu na katiba ya Tanganyika na zanzibar! Serikali tatu ni mzigo sana. kwa mfano wabunge sehemu ninayokaa mimi watakuwa watatu. wawili wa muungano na mmoja wa Tanganyika. Dawa ni serikali moja.
 
Wazenji wakikusikia watakuuua. Ila inauma kwa wazenji kutaka muundo huu wa serikali mbili iendelee ati hii ni sera ya CCM!!!!
 
Haya ni maoni ya wananchi sio ya tume. Usiwalaumu! Wengi wa wananchi walisema kuwa wanataka serikali tatu.
 
Serikali tatu ni mzigo kwa watanganyika ..wazanzibar hawana kitu zaid ya harua na tende...Tufanye maamuzi magumu Tuachane nao kwanza wanatunyonya sana serikali yao wanaendeshea fedha za watanganyika
 
Mkuu tanganyika haipo,irejesheni kwanza tujue mbichi na mbivu.
 
Ili tusimeguke vipande vipande, ni vema tukawa na nchi moja (JMT) yenye katiba moja (Katiba ya JMT) inayojumuisha vipengele vya serikali zote ndani ya JMT.

Serikali za JMT hazitakuwa tatu, zitakuwa nyingi zaidi. Lakini kubwa ni tatu. Tusipojitengenezea katiba moja inayoongoza serikali zote, basi tutakuwa tumejiwekea misingi ya kufarakana.

Viongozi wa serikali za Tanganyika, Zanzibar na za JMT itafaa waape kuilinda katiba ya JMT (ambayo ndani yake tayari kuna katiba ya serikali ya Tanganyika au Zanzibar). Kusiwe na kiongozi ya Tanganyika au Zanzibar ambaye hataapa kuilinda katiba ya JMT.

Ni wazi basi ili tudumu, itabidi sasa tuwe na katiba mpya moja ambayo itakuwa na vipengele mbadala vya katiba ya sasa ya JMT na katiba ya sasa ya Serikali ya Zanzibar, na katiba mpya ya Serikali ya Tanganyika.

Hili wazo kwamba katiba ya sasa ya Serikali ya Zanzibar itabaki ni wazo lisilowezekana. Lazima kuwe na katiba mypa ya Serikali ya Zanzibar itakayoendana na katiba mpya ya JMT.

Yote haya yatawezekana na kufanyika vizuri kama tutatambua ukweli kwamba itabidi Kamati ya Katiba (ya Warioba) itayarishe Katiba ya JMT yenye vipengele vya katiba mpya za Serikali za Zanzibar na Tanganyika. Na ndio maana hiyo kamati ina wajumbe wa kutosha kutoka sehemu zote za JMT.

Ili muungano wetu udumu, itabidi tuwe nchi moja yenye katiba moja yenye vipengele vya serikali tatu. Tutaongozwa na katiba moja na sio katiba tatu.

Nchi moja, sheria mama moja.
 
Hii nchi raia wake mmejitengenezea utamaduni wa kulalamika tu kila jambo. Ni utamaduni wa wazee na watoto wasioridhika. Unaposema kuwa watu hawakutaka serikali tatu umetumia vigezo gani? Kama ulifanya research, ulitumia parameters zipi na sample size ya population yako ni ipi? No wonder hii nchi inaongozwa kwa matukio tu kwasababu the majority of citizens are mediocre minds!
 
Kwanin wameamua kuja na pendekezo la serikali tatu ilihal wananch hawakuambiwa kama muundo utakuwa hv? wanataka waendelee kuandika rasimu na katiba ya Tanganyika na zanzibar! Serikali tatu ni mzigo sana. kwa mfano wabunge sehemu ninayokaa mimi watakuwa watatu. wawili wa muungano na mmoja wa Tanganyika. Dawa ni serikali moja.
Ulitaka wafanyaje wakati mmewalizimisha watu waje na katiba mpya bila ya kutaka kujua itatue matatizo gani na kero gani za sasa, wasn't the whole thing pathetic from the outset.

Kiasi Miss Shonza awaite wale waliotuaribia kupata balance and checks na kutaka katiba mpya without a clear improvement on the existing problems ni kasaccos tu cha watu wachache (sio maneno yangu hayo bali ya yule dada wa mipasho some where on this forum on some thread they exist) the whole demand of a new constitution was pathetic.

Isipokuwa raisi ana nguvu nyingi sana and that is a problem na watu wengi wanaoteuliwa wanahitaji kuchaguliwa au nyadhifa zingine ni za kufutwa tu (kama wakuu wa mikoa).

Wengine wakaanza na hadithi za majimbo nakukoroga mambo how idiotic.
 
Naunga Mkono kwa asilimia zote wazo la Serikali Tatu kwa sababu kwa Mazingira ya sasa huwezi pendekeza uanzishwaji wa Serikali Moja ukaungwa mkono na hata asilimia Moja ya Wazanzibari.Vilevile Wazo la kuvunja Muungano haliwezi kuungwa Mkono na viongozi wengi hadharani.Kwa maana hiyo,Wazo la kuanzishwa kwa Serikali tatu ni njia sahihi katika uelekeo wa kutatua Kero za Muda Mrefu za Muungano.
 
Tunaweza kubadili maeneo mengi lkn hl l serikari tatu hapana. Mm naunga mkono serikali 2
 
What will be ZNZ's matters, what will be Tanganyika's Matters and what is the purpose of the Central gov? In your opinion; and what problems would they solve on both parties?
 
Ndugu,Umeuliza Maswali ya Msingi sana.Kwa kifupi Mimi ni Muumini wa Serikali Moja tu yenye Mamlaka yote bila kuwa na Mambo yanayofanywa na Zanzibar peke yao au Tanganyika peke yao.Kwa kuwa, hili haliwezi kukubaliwa na Asilimia Kubwa ya Wazanzibari wakiongozwa na Maalim Seif,Na kwa kuwa, Muundo wa sasa wa Muungano unaonekana kuwanyonya zaidi Watanganyika,Sipendi Muundo wa sasa wa Serikali Mbili uendelee.Pendekezo langu ni kwamba,Kila Upande uwe na Mamlaka yake kamili bila Muungano.SASA BASI,Kwa kuwa,hakuna mwenye Ubavu Serikalini wa kupendekeza Muungano uvunjike,ndio nikafika Hitimisho kwamba Uanzishwaji wa Serikali tatu ndio njia pekee iliyobaki ya kutupeleka kwenye kuvunja Muungano.
 
Kwanin wameamua kuja na pendekezo la serikali tatu ilihal wananch hawakuambiwa kama muundo utakuwa hv? wanataka waendelee kuandika rasimu na katiba ya Tanganyika na zanzibar! Serikali tatu ni mzigo sana. kwa mfano wabunge sehemu ninayokaa mimi watakuwa watatu. wawili wa muungano na mmoja wa Tanganyika. Dawa ni serikali moja.
Wananchi wangeambiwaje kuwa mfumo utakuwa serikali tatu kabla ya tume kukusanya maoni ya wananchi na wadau wote kujua aina ya muungano wanaoutaka? au Ulitaka tume ikae tu na ku dictate??Na incase ya kuundwa kwa katiba ya Tanganyika tume ya warioba hawawezi kutumika maana tume yao ina sura ya muungano, sasa unataka kusema wazanzibar watakuja kusaidia kuandika katiba ya Tanganyika au Watanganyika wataenda kuunda katiba ya Zanzibar lazima iundwe Tume nyingine! Usipende tuu kutupa lawama bila kujiridhisha na hizo tuhuma!!Hilo la serikali moja ni wazo lako ungeliwasilisha kwenye tume, ila wengi wametaka serikali tatu!
 
Tunaweza kubadili maeneo mengi lkn hl l serikari tatu hapana. Mm naunga mkono serikali 2

sawa ila walio wengi wametaka serikali tatu ndio maana Rasimu imependekeza hilo!!
 
Ili tusimeguke vipande vipande, ni vema tukawa na nchi moja (JMT) yenye katiba moja (Katiba ya JMT) inayojumuisha vipengele vya serikali zote ndani ya JMT.

Serikali za JMT hazitakuwa tatu, zitakuwa nyingi zaidi. Lakini kubwa ni tatu. Tusipojitengenezea katiba moja inayoongoza serikali zote, basi tutakuwa tumejiwekea misingi ya kufarakana.

Viongozi wa serikali za Tanganyika, Zanzibar na za JMT itafaa waape kuilinda katiba ya JMT (ambayo ndani yake tayari kuna katiba ya serikali ya Tanganyika au Zanzibar). Kusiwe na kiongozi ya Tanganyika au Zanzibar ambaye hataapa kuilinda katiba ya JMT.

Ni wazi basi ili tudumu, itabidi sasa tuwe na katiba mpya moja ambayo itakuwa na vipengele mbadala vya katiba ya sasa ya JMT na katiba ya sasa ya Serikali ya Zanzibar, na katiba mpya ya Serikali ya Tanganyika.

Hili wazo kwamba katiba ya sasa ya Serikali ya Zanzibar itabaki ni wazo lisilowezekana. Lazima kuwe na katiba mypa ya Serikali ya Zanzibar itakayoendana na katiba mpya ya JMT.

Yote haya yatawezekana na kufanyika vizuri kama tutatambua ukweli kwamba itabidi Kamati ya Katiba (ya Warioba) itayarishe Katiba ya JMT yenye vipengele vya katiba mpya za Serikali za Zanzibar na Tanganyika. Na ndio maana hiyo kamati ina wajumbe wa kutosha kutoka sehemu zote za JMT.

Ili muungano wetu udumu, itabidi tuwe nchi moja yenye katiba moja yenye vipengele vya serikali tatu. Tutaongozwa na katiba moja na sio katiba tatu.

Nchi moja, sheria mama moja.

Mkuu unavyosema serikali za tanganyika na Zanzibar ndan ya JMT utashindwa kutenganisha hzo dola mbili ndogo ndan ya JMT. M naona wazo lako jipya ni kwamba viongoz wa Tanganyika na Zanziba nao waape kuilinda katiba ya JMT. Bado ni mzigo sana kuwa serikali Tatu. Dawa nzuri ya kulinda Muungano ni kuwa na serikali moja tu Zanzibar kuwe na majimbo au mikoa.
 
Hii nchi raia wake mmejitengenezea utamaduni wa kulalamika tu kila jambo. Ni utamaduni wa wazee na watoto wasioridhika. Unaposema kuwa watu hawakutaka serikali tatu umetumia vigezo gani? Kama ulifanya research, ulitumia parameters zipi na sample size ya population yako ni ipi? No wonder hii nchi inaongozwa kwa matukio tu kwasababu the majority of citizens are mediocre minds!

M nafikiri asiyejua kulalamika kichwa chake hakifikiri. Tunachokisema hapa ni maoni kama wewe usivyo na maoni ya mtindo upi ungelinda muungano zaidi. Swala kusema yalikuwa maoni ya wananchi kuwa na serikali tatu mbona hawajatupa takwimu sahihi ni watu wa ngapi wamesema wanataka serikali tatu, mbili, Moja au tuvunje? M nafikiri ilikuwa inatakiwa tupate kura za maoni ya je tuwe na serikali ngapi ila tusivunje muungano kama hadidu za rejea walizokuwa nazo.
 
Naunga Mkono kwa asilimia zote wazo la Serikali Tatu kwa sababu kwa Mazingira ya sasa huwezi pendekeza uanzishwaji wa Serikali Moja ukaungwa mkono na hata asilimia Moja ya Wazanzibari.Vilevile Wazo la kuvunja Muungano haliwezi kuungwa Mkono na viongozi wengi hadharani.Kwa maana hiyo,Wazo la kuanzishwa kwa Serikali tatu ni njia sahihi katika uelekeo wa kutatua Kero za Muda Mrefu za Muungano.

je unaamin kwamba Talaka ni mwanzo wa kuachana? m siamin kama hakuna wazanzibari wanaotaka serikali moja. wapo wengi tu.
 
Ndugu,Umeuliza Maswali ya Msingi sana.Kwa kifupi Mimi ni Muumini wa Serikali Moja tu yenye Mamlaka yote bila kuwa na Mambo yanayofanywa na Zanzibar peke yao au Tanganyika peke yao.Kwa kuwa, hili haliwezi kukubaliwa na Asilimia Kubwa ya Wazanzibari wakiongozwa na Maalim Seif,Na kwa kuwa, Muundo wa sasa wa Muungano unaonekana kuwanyonya zaidi Watanganyika,Sipendi Muundo wa sasa wa Serikali Mbili uendelee.Pendekezo langu ni kwamba,Kila Upande uwe na Mamlaka yake kamili bila Muungano.SASA BASI,Kwa kuwa,hakuna mwenye Ubavu Serikalini wa kupendekeza Muungano uvunjike,ndio nikafika Hitimisho kwamba Uanzishwaji wa Serikali tatu ndio njia pekee iliyobaki ya kutupeleka kwenye kuvunja Muungano.

Kumbe unaamin serikali tatu ni njia ya kuvunja Muungano. M naamin Hata kama wazanzibar hawatapenda serikali moja kelele zao zitakuwa za muda tu.
 
Back
Top Bottom