Logatho Mwolokujova
Senior Member
- Apr 27, 2013
- 116
- 18
Mkuu tanganyika haipo,irejesheni kwanza tujue mbichi na mbivu.Serikali tatu ni mzigo kwa watanganyika ..wazanzibar hawana kitu zaid ya harua na tende...Tufanye maamuzi magumu Tuachane nao kwanza wanatunyonya sana serikali yao wanaendeshea fedha za watanganyika
Ulitaka wafanyaje wakati mmewalizimisha watu waje na katiba mpya bila ya kutaka kujua itatue matatizo gani na kero gani za sasa, wasn't the whole thing pathetic from the outset.Kwanin wameamua kuja na pendekezo la serikali tatu ilihal wananch hawakuambiwa kama muundo utakuwa hv? wanataka waendelee kuandika rasimu na katiba ya Tanganyika na zanzibar! Serikali tatu ni mzigo sana. kwa mfano wabunge sehemu ninayokaa mimi watakuwa watatu. wawili wa muungano na mmoja wa Tanganyika. Dawa ni serikali moja.
What will be ZNZ's matters, what will be Tanganyika's Matters and what is the purpose of the Central gov? In your opinion; and what problems would they solve on both parties?Naunga Mkono kwa asilimia zote wazo la Serikali Tatu kwa sababu kwa Mazingira ya sasa huwezi pendekeza uanzishwaji wa Serikali Moja ukaungwa mkono na hata asilimia Moja ya Wazanzibari.Vilevile Wazo la kuvunja Muungano haliwezi kuungwa Mkono na viongozi wengi hadharani.Kwa maana hiyo,Wazo la kuanzishwa kwa Serikali tatu ni njia sahihi katika uelekeo wa kutatua Kero za Muda Mrefu za Muungano.
Ndugu,Umeuliza Maswali ya Msingi sana.Kwa kifupi Mimi ni Muumini wa Serikali Moja tu yenye Mamlaka yote bila kuwa na Mambo yanayofanywa na Zanzibar peke yao au Tanganyika peke yao.Kwa kuwa, hili haliwezi kukubaliwa na Asilimia Kubwa ya Wazanzibari wakiongozwa na Maalim Seif,Na kwa kuwa, Muundo wa sasa wa Muungano unaonekana kuwanyonya zaidi Watanganyika,Sipendi Muundo wa sasa wa Serikali Mbili uendelee.Pendekezo langu ni kwamba,Kila Upande uwe na Mamlaka yake kamili bila Muungano.SASA BASI,Kwa kuwa,hakuna mwenye Ubavu Serikalini wa kupendekeza Muungano uvunjike,ndio nikafika Hitimisho kwamba Uanzishwaji wa Serikali tatu ndio njia pekee iliyobaki ya kutupeleka kwenye kuvunja Muungano.What will be ZNZ's matters, what will be Tanganyika's Matters and what is the purpose of the Central gov? In your opinion; and what problems would they solve on both parties?
Wananchi wangeambiwaje kuwa mfumo utakuwa serikali tatu kabla ya tume kukusanya maoni ya wananchi na wadau wote kujua aina ya muungano wanaoutaka? au Ulitaka tume ikae tu na ku dictate??Na incase ya kuundwa kwa katiba ya Tanganyika tume ya warioba hawawezi kutumika maana tume yao ina sura ya muungano, sasa unataka kusema wazanzibar watakuja kusaidia kuandika katiba ya Tanganyika au Watanganyika wataenda kuunda katiba ya Zanzibar lazima iundwe Tume nyingine! Usipende tuu kutupa lawama bila kujiridhisha na hizo tuhuma!!Hilo la serikali moja ni wazo lako ungeliwasilisha kwenye tume, ila wengi wametaka serikali tatu!Kwanin wameamua kuja na pendekezo la serikali tatu ilihal wananch hawakuambiwa kama muundo utakuwa hv? wanataka waendelee kuandika rasimu na katiba ya Tanganyika na zanzibar! Serikali tatu ni mzigo sana. kwa mfano wabunge sehemu ninayokaa mimi watakuwa watatu. wawili wa muungano na mmoja wa Tanganyika. Dawa ni serikali moja.
Tunaweza kubadili maeneo mengi lkn hl l serikari tatu hapana. Mm naunga mkono serikali 2
Ili tusimeguke vipande vipande, ni vema tukawa na nchi moja (JMT) yenye katiba moja (Katiba ya JMT) inayojumuisha vipengele vya serikali zote ndani ya JMT.
Serikali za JMT hazitakuwa tatu, zitakuwa nyingi zaidi. Lakini kubwa ni tatu. Tusipojitengenezea katiba moja inayoongoza serikali zote, basi tutakuwa tumejiwekea misingi ya kufarakana.
Viongozi wa serikali za Tanganyika, Zanzibar na za JMT itafaa waape kuilinda katiba ya JMT (ambayo ndani yake tayari kuna katiba ya serikali ya Tanganyika au Zanzibar). Kusiwe na kiongozi ya Tanganyika au Zanzibar ambaye hataapa kuilinda katiba ya JMT.
Ni wazi basi ili tudumu, itabidi sasa tuwe na katiba mpya moja ambayo itakuwa na vipengele mbadala vya katiba ya sasa ya JMT na katiba ya sasa ya Serikali ya Zanzibar, na katiba mpya ya Serikali ya Tanganyika.
Hili wazo kwamba katiba ya sasa ya Serikali ya Zanzibar itabaki ni wazo lisilowezekana. Lazima kuwe na katiba mypa ya Serikali ya Zanzibar itakayoendana na katiba mpya ya JMT.
Yote haya yatawezekana na kufanyika vizuri kama tutatambua ukweli kwamba itabidi Kamati ya Katiba (ya Warioba) itayarishe Katiba ya JMT yenye vipengele vya katiba mpya za Serikali za Zanzibar na Tanganyika. Na ndio maana hiyo kamati ina wajumbe wa kutosha kutoka sehemu zote za JMT.
Ili muungano wetu udumu, itabidi tuwe nchi moja yenye katiba moja yenye vipengele vya serikali tatu. Tutaongozwa na katiba moja na sio katiba tatu.
Nchi moja, sheria mama moja.
Hii nchi raia wake mmejitengenezea utamaduni wa kulalamika tu kila jambo. Ni utamaduni wa wazee na watoto wasioridhika. Unaposema kuwa watu hawakutaka serikali tatu umetumia vigezo gani? Kama ulifanya research, ulitumia parameters zipi na sample size ya population yako ni ipi? No wonder hii nchi inaongozwa kwa matukio tu kwasababu the majority of citizens are mediocre minds!
Naunga Mkono kwa asilimia zote wazo la Serikali Tatu kwa sababu kwa Mazingira ya sasa huwezi pendekeza uanzishwaji wa Serikali Moja ukaungwa mkono na hata asilimia Moja ya Wazanzibari.Vilevile Wazo la kuvunja Muungano haliwezi kuungwa Mkono na viongozi wengi hadharani.Kwa maana hiyo,Wazo la kuanzishwa kwa Serikali tatu ni njia sahihi katika uelekeo wa kutatua Kero za Muda Mrefu za Muungano.
Ndugu,Umeuliza Maswali ya Msingi sana.Kwa kifupi Mimi ni Muumini wa Serikali Moja tu yenye Mamlaka yote bila kuwa na Mambo yanayofanywa na Zanzibar peke yao au Tanganyika peke yao.Kwa kuwa, hili haliwezi kukubaliwa na Asilimia Kubwa ya Wazanzibari wakiongozwa na Maalim Seif,Na kwa kuwa, Muundo wa sasa wa Muungano unaonekana kuwanyonya zaidi Watanganyika,Sipendi Muundo wa sasa wa Serikali Mbili uendelee.Pendekezo langu ni kwamba,Kila Upande uwe na Mamlaka yake kamili bila Muungano.SASA BASI,Kwa kuwa,hakuna mwenye Ubavu Serikalini wa kupendekeza Muungano uvunjike,ndio nikafika Hitimisho kwamba Uanzishwaji wa Serikali tatu ndio njia pekee iliyobaki ya kutupeleka kwenye kuvunja Muungano.