wajumbe wa tume ya katiba mpya wajitengenezea ulaji mwingine.


Hilo la wengi wamesema ni sawa maamuzi ya spika Bungeni kusema wengi wamesema ndio wakati si kweli. kwanin usiwekwe utaratibu wa kupiga kura?
 
Hilo la wengi wamesema ni sawa maamuzi ya spika Bungeni kusema wengi wamesema ndio wakati si kweli. kwanin usiwekwe utaratibu wa kupiga kura?

Jamani tunapochambua hii rasimu tuchambue tukiujua tunachoongea, awali maoni ya wananchi ndio yamewekwa kwenye rasimu, kama umemsikia warioba vizuri alisema wananchi wengi walipendekeza serikali tatu ndio maana imewekwa kwenye rasimu, kama unauelewa mtiririko mzima wa kupata Katiba mpya kura ya maoni itapigwa mwishoni kabisa kuidhinisha draft ya mwisho ya rasimu kuwa katiba, sasa wewe unataka kura ipigwe wapi au lini??soma rasimu na elewa mtiririko mzima wa kuipata katiba,,,
 
We are right on our split path as a united republic of tanzania.i wonder who will be a loser and who will be a winner is any anyone guess!
 
je unaamin kwamba Talaka ni mwanzo wa kuachana? m siamin kama hakuna wazanzibari wanaotaka serikali moja. wapo wengi tu.

Siamini kwa mzanzibar halisi kutaka serekali moja labda huyo ni mzanzibara au muhafidhina wa kimaslahi
 
sawa ila walio wengi wametaka serikali tatu ndio maana Rasimu imependekeza hilo!!

kwa nini tusiwe na majimbo mawili lets say jimbo la Tanganyika na jimbo la zanzibar na yote yakaongozwa na magavana?na wote wakaapa kwa katiba ta muungano.au tukawa tunachagua rais na makamu wake wawili wa zanzibar na tanganyika ambao kila mmoja jukumu lake kuu itakuwa ni kusimamia mambo yasiyo ya muungano kwa upande wake na wote wakawajibika kwa kwa rais ambaye atakuwa wa muungano.
 

Kura ninayomaanisha ni ya kuwa na serikali ngapi? sio kuipigia kura katiba mpya. hlo lije baada ya kujua wangapi wanataka serikali ngapi.
 
Suluhisho ni kuachana na muungano sababu hata tukiwa na serikali tatu bado hatutaweza kuondokana na manung'uniko toka pande husika, kama kuungana tutakutana kwenye East Africa community, but for benefits of both side lets separate.
 
hao binadamu wachoyo visiwani watakusikia lakini wewe? dawa ni kuachana nao tu!
 
Kumbuka wananchi wengi hawahijui katiba ya sasa kwahiyo hata utoaji wa maoni na maoni yao ni copy and paste toka kwa wanasiasa just kukidhi matakwa ya kisiasa bila kuzingatia vigezo na hali halisi.
 
Hilo la wengi wamesema ni sawa maamuzi ya spika Bungeni kusema wengi wamesema ndio wakati si kweli. kwanin usiwekwe utaratibu wa kupiga kura?

Huwezi kujua kama mwenzako anauwezo wa kuhesabu sauti, huenda katiba mpya ikapigiwa kura ya ndiyoooo!! na kutumia uwezo wa bi kiroboto kuzihesabu sauti hizo!
 
Muda wa kura za maoni bado, ngoja mabaraza ya katiba ya kata yamalize wajibu wake ndo wake ndo lije bunge la katiba then tupige kura. Haraka ya nini, kwani wamesema hiyo rasimu ndo katiba yenyewe? Bado una nafasi ya kukataa au kuikubali ila tukubali tu kuwa the winner takes all!!!!
 
Mimi nadhani mawazo ya kuwa na serikali moja au mbili au tatu yote ni sawa. Kikubwa zaidi ni
1. Kuzingatia ufumbuzi wa yanaitwa matatizo ya Muungano.
2. Ukubwa wa Serikali ya Muungano, Tanganyika na ile ya Zanzibar. Hadi hivi sasa katika Rasimu hii ya katiba kuwa na mawaziri 15 na manaibu wake (ni dhahili Manaibu Waziri nao ni 15), Wabunge 75 bado ni Serikali kubwa ilihali wakishughulikia mambo 7 tu! Wengi walivyosikia idadi hii wamepongeza sana wakifikiri au wakitafsiri kwa kulinganisha na idadi ya viongozi hao hao katika Serikali ilipo madarakani (JMT), kumbe si kweli!

Watu wengi wameanza kulalamikia Serikali tatu kwamba ni mzigo hilo wala halina ubishi vinginevyo idadi ya Mawaziri manaibu waziri na Wabunge katika Muungano wapungue na wale watakao pendekezwa katika Katiba za Serikali za Tanganyika na Zanzibar nao wawe kidogo sana kiasi kwamba Idadi ya viongozi hawa kutoka serikali shirikishi na ile ya Muungano iwe chini ya idadi tuliyonayo katika Muungano. Vinginevyo ni MAUMIVU!!!!!!
 
Kura ninayomaanisha ni ya kuwa na serikali ngapi? sio kuipigia kura katiba mpya. hlo lije baada ya kujua wangapi wanataka serikali ngapi.

ilishapigiwa sasa kelele kuwa iitishwe kura ya maoni kuhusu muungano lakini serikali hii ya ccm ilivyo na ukaidi ilikataa katakata!!
 

Lakini ni kawaida kabisa kwa serikali ya muungano kuwa na dola ndogo nyingi ndani yake. Angalia mfano wa Ujerumani au wa Marekani. Serikali ya JMT ndiyo itakuwa serikali kuu. Chini yake kutakuwa na serikali za Tanganyika na Zanzibar.

Serikali za Zanzibar na Tanganyika zitakuwa kama zilivyo serikali za Florida na California katika serikali ya Marekani.

Cha msingi kabisa basi ni swala la Watanzania wameimbia nini Tume ya Katiba. Kama wametaka serikali tatu, basi hilo linawezekana, na sio demokrasia kufanya vinginevyo. Zitakuwa serikali tatu, lakini hazitalingana. Serikali ya JMT itakuwa ndiyo serikali kuu, na viongozi wote wataapa kulinda katiba yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…