Ndiyo maana vyombo vya habari vya waarabu vinadharauliwa! Eti wajumve kutoka mataifa 180, huo ni uwongo mkubwa.
Taarifa kutoka UN, wajumve waliotoka walikuwa kutoka mataifa 150. Taarifa hiyo imesema kuwa wengi wa waliokhwemo humu ukumbini kabla ya Natenyahu na baadaye kutoka nje, walikuwa ni maafisa wa chini wawakilishi wa mataifa yao. Maafisa wakuu wawakilishi wa mataifa mengi hawakuwemo humu ukumbini, hata kabla ya Netenyahu kuingia ukumbini.
Mwisho wa yote ni dhihirisho namna wawakilishi wengi wa nchi za kiarabu na kiislam walivyo na upeo mdogo. Hivi kutoka nje ya ukumbi, halafu ukiwa nje unafuatilia hotuba hiyo hiyo uliyoikimbia, hiyo ni akili au ujinga? Hivi kutoka ukumbini, kunabadilisha vipi hali ya Gaza? Hii ni sawa na kumwambia Netanyahu aendelee na mpango wake.
Wangekuwa na weledi, wangebakia ili baada ya hotuba yake, nao waandae hotuba za kumjibu. Na pia kuangalia mahali pa kuingilia ili kuokoa maisha ya wapalestina. Mathalani kwenye hotuba ya Netanyahu amesema kuwa Hamas wanyang'anywe silaha, mateka wote waachiwe kwa mpigo, Serikali ya kiraia yenye utayari wa kuwa na mahusiano ya amani na Israel iundwe. Hapo ndipo palikuwa pa kuanzia, wangeboresha, na kukomesha vita. Huo ujinga walipufanya, wa kutoka nje, hauna msaada wowote kwa wapalestina wasio na hatia.