Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
MAKUMBUSHO YAWAKA BAADA YA MUHARAMI CHUMA KUTANGAZWA MSHINDI – WAJUMBE WAPINGA, WATAKA UCHAGUZI URUDIWE
Hali ya sintofahamu Iliibuka katika Kata ya Makumbusho, Wilaya ya Kinondoni, baada ya kutangazwa kwa Muharami Rajabu Chuma kuwa mshindi wa kura za maoni za udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika mchakato wa uchaguzi wa ndani unaoendelea kote nchini.
Chuma, ambaye pia ni diwani anayemaliza muda wake, ameibuka mshindi wa kura hizo, lakini tangazo hilo limeibua hisia kali kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa matawi, wajumbe na wafuasi wa wagombea wengine, wakilalamikia kile wanachokiita “wizi wa kura” na kuhoji uhalali wa mchakato mzima.
"Wapigia Kura sawa sawa, kwanini boksi moja halionekani? Na kwanini katika boksi moja zimekutwa Kura 20 za Mgombea mmoja? Wao ndio viongozi wa Kata hii kwanini wanataka kuwa wachonganishi?"