Wajuzi naomba kueleweshwa TRA Imewezaje kuwa mwekezaji wa timu ya mpira ya Tabora united ?

Wajuzi naomba kueleweshwa TRA Imewezaje kuwa mwekezaji wa timu ya mpira ya Tabora united ?

Tajiri wa kinyankole

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,977
Reaction score
4,912
Kwangu mimi nachofahamu mamlaka ya mapato tanzania (TRA) kazi yake kubwa ni ukusanyaji wa kodi ambazo kodi hizo hupelekwa kwenye miradi ya maendeleo na kulipa watumishi katika taasisi mbalimbali

Fedha hizo za uwekezaji kwenye mpira zimetoka wapi siyo kwamba ni njia ya utakatishaji fedha!
Au ni jina tu limetumika katika kubadilisha timu ya mpira ?

Binafsi mimi sijaelewa kabisa kuhusiana na hili naombeni wenye maarifa mapana wanidadavulie swala hili ambalo kwangu mimi bado naona lina ukakasi.
 
Nadhani inawezekana sababu mbona majeshi kama JKT na Police wana timu
 
Nadhani inawezekana sababu mbona majeshi kama JKT na Police wana timu
Hizo pesa zilizonunua team kwanini zisingepwlekwa kwenye miradi ya maendeleo kama kwenye miundombinu ya barabara,afya, elimu, n.k hizo fedha zilizokusanywa na wananchi naamini kwamba zingeenda kuboresha kwenye afya , maji n.k. na siyo kwenda kununua team.
 
💯
 
Kuna team kadhaa kila siku zinakuja jangwani kujifunza mambo kadhaa.

URA Sports Club ni team iliyo chini ya mamlaka ya mapato Uganda na ni moja ya team ya muda mrefu kwenye league pale Uganda.

Je, unajua au hujui uenda TRA walienda kupata uzoefu kule?.
 
Wameamua kupunguza nuksi za ufisadi mkiwauliza pesa zinaenda wp watawaambia wanafadhili timu...
 
Back
Top Bottom