Mkuu mbona simple sana!
Hiyo ndio maana ya "MAIGIZO" yaani "UNAIGIZA" hakuna kinachotakiwa kuwa kweli yote ni kuigiza tu hakuna kupigana kweli ngumi za uso.
Hiyo ya watu kujua kupigana kweli ilikuwa enzi hizo sana tena kwa kwenye movie zenye budget ndogo.
Lakini siku hizi ni muigizaji anaingia gym kufanya mazoezi ya kujenga mwili na misuli (wengine hujifunza kabisa aina za mapigano kama kong fu na judo au krav maga kama nyongeza au kufanya mwili uwe sharp pekee) baada ya hapo director na write tayari wanakuwa na scene ya mapigano itakavyokuwa vichwani mwao inaitwa fight choreography, alafu kunakuwa na watu special kabisa ambao ni wapiganaji officials kabisa wao kazi yao wanaapply maagizo ya director na write yaani fight choreography na kusaidia actors wapigane vipi mbele ya camera. hakuna kupigana ngumi kweli lakini au kama itahitajika hivyo basi watatumia watu wanaita stunt doubles hawa ni watu maalum ambao huajiriwa kwa ajili ya kufanya mambo ya hatari tu kwenye movies ikiwemo mapigano.
Au wataruka yote hayo na kwenye scenes za mapigano watachukua tu stunt doubles wanaofanan na actors wenyewe lakini ambao ni wapiganaji professional then watarecord scenes za mapigano alafu wataedit sura ya actor na stunt double alafu tayari movie imekamilika.
Kwenye movies kubwa watu hawaangalii nani anajua kupigana bali wanaangalia uwezo wao wa kuigiza yaani acting skills na elimu yako ya maswala ya sanaa bila kusahau umaarufu wa jina, hayo mengine ni nyongeza tu.
Muigizaji bora anayejua anachokifanya atacheza scene yoyote kwa ufasaha na uhalisia hasa akipata director bora na mzoefu anayejua maana movie choreography na movie cinematography.
Muone brad pitt kwenye fury.
Leonardo dicaprio kwenye inception.
Keanu reeves kwenye John Wick, humu keanu alifanya mazoezi ya shooting lakini jamaa sio fighter ni mtu mmoja cool sana lakini zile fight choreography zinamfanya awe professional assassin mnyama asiyekamatika.
matt damon kwenye Jason Bourne.
Tom Cruise, huyu mzee angalia movie zake zote hasa mission impossible na jack reacher na yeye hatumii stunt doubles bali anafanya mwenye kiume maigizo yote hata kuruka nje ya ghorofa na ndege na kuning'inia nje ya ndege huyu mzee ni legend.
Colin Firth kwenye Kingsman the secret service, hii movie ina scene moja ya hatari sana pale kanisani acha kabisa na yote ni sababu ya director na ule upangaji wa fight choreography, director na amefanya unyama sana kwenye ile scene respect.
Chris evans kwenye captain america, humu wanatumia computer yaani vfs na green screen.
Bob Odenkirk kwenye nobody.
Daniel craig kwenye james bond hasa no time to die na yule bidada mrembo Ana de Armas anachapa mkono sasa jiulize yule dada mrembo namna ile na usoft wote ule anawezaje hata kurusha ngumi mpaka mtu aisikie acha kuanguaka.
Alafu bado kidogo niisahau The Equalizer kazi ya mzee mzima mr Denzel Washington.
Mzee nikiendelea kuandika hapa naona sitamaliza sababu movie nilizoangalia ni mamia au maelfu mpaka sasa ila kiufupi kwenye main cinema industry au niseme hollywood kitu kinachoamua Movie iwe vipi ni Budget ya movie yaani pesa za kutosha na baada ya hapo kinachofuata ni Writer na Director bora anayejua anachokifanya ukipata hivyo vitatu movie itakuwa vyovyote vile inavyotakiwa.
Limitation ni Imagination pekee, nimeandika rough sana lakini nadhani inaeleweka.
Over and out.