Wajuzi wa gari aina ya Premio naombeni ufafanuzi

Lorenzo1

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2017
Posts
530
Reaction score
641
Habari Wakuu,

Leo nimekuja hapa na ishu moja. Katika harakati zangu za kujichanga nategemea kupata kahela kidogo kama 9 - 10 m hivi.

Sasa nimeona sio mbaya kama nikawa na kausafiri kangu kakuzugiaa. Katika kucheki gari nikatokea kuipenda sana Toyota Premio. Kucheki bei nikaona zinacheza 13+ mpaka 14 kwingne mpaka 15.

Sasa nataka nichukue iliyokwisha tumika hapa bongo lakini kwa mtu au dealer anayeaminika.

Nimekuja hapa Mnisaidie mambo mawili. Kwanza kwa yeyote mwenye uelewa wa hii gari ya premio, shida zake na changamoto zake kwa ujumla. Pili kama kuna mtu yeyote au dealer wa kuaminika ambaye nitaweza kumtumia nivute iyo gari lakini ikiwa used Maana bajeti kwa sasa sina.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.


Premio
 
Hapo kwa Dealer anayeaminika sijakuelwa, ila Premio ni sedan nzuri ,haina kipengele chochote tena chukua ya 1.5k cc nimeitumia huu mwaka wa pili haijawahi kusumbua tofauti na kumwaga oil na kubadilisha filter, cha msingi uwe mtunzaji vifaa vyake kama taa zake bei yake imechangamka kidogo.
 
Hii gari nimeitumia miaka 3 mpk kuja kuiuza na niliiuza kwa sababu binafsi tu na si kwamba gari ilikuwa na shida...gari haijawah nisumbua kwa miaka yoye 3..ni service tu basi
 
Kiukweli mimi ndo gari ninayotumia kwa sasa kwa miaka mitatu sasa sijawahi kuona shida yoyote tofauti kumwaga oil au filter na hata spare zake zinapatikana kwa urahisi. 1790cc
 
Hii chombo haina mawaa hata ukipata ya 1.8 sio mbaya bado fuel consumption iko chini sana na perfomance yake sio ya kuibeza sana.
 
Asante sana kwa ushauri kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…