Wajuzi wa magari mnisaidie

Mkuu, hiko kinaitwa Smart Fortwo Passion 2nd generation hiyo ya 2009 nadhani. Engine cc 1000 piston 3 (engine ni ya Mitsubishi).

Kuna maza mmoja alikua nako, kila siku kakawa na shida kaliwajua mafundi kama 30 hivi hapa mjini. Sahivi kapo kwao amenunua tu IST.
 
Asante kwa taarifa, so inaonekana ni kigari flan korofi au
 
Na vipi hukubahatika kujua Bei yake kwa hapa bongo na wap vinapatikana
 
Utembelee huto tugari twa mtoto? Kuwa serious mkuu ukiona gari ina studs 4 kushuka chini jua ni gari ya kiwango cha chini. Hicho ni mfano halisi wa bebiwoka with 3 studs!

Gari za maana zinaanzia 5 studs mpaka 6 hapo.[emoji3][emoji3][emoji3]
Bora kuchapa lapa kuliko hii toy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…