Wajuzi wa magari nisaidieni, ninunue gari aina gani na rangi ipi. Nina milioni 12

Wajuzi wa magari nisaidieni, ninunue gari aina gani na rangi ipi. Nina milioni 12

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2018
Posts
448
Reaction score
409
Wapendwa Nina milioni 12, ila nashindwa kufanya maamuzi, ninunue aina ipi ya gari na rangi ipi nzuri, wenye uzoefu mnaojua ambalo halili mafuta na siyo la kuchoka haraka.

Asanteni.
 
Chukua hii

2453595_images2039.jpg
 
Nadhani ni muhimu kufahamu unahitaji kulitumia kwa shughuli gani?

Kwenda kazini, ibadani, biashara au unalihitaji kwa sababu za kisaikolojia (kupandisha hadhi, kutaka utambulike, nk), kutunza pesa au shughuli nyingine yoyote.

Pia zingatia mazingira ya kule litakakotumika. Ubora/ubovu wa barabara.

Kumbuka kuzingatia matumizi ya nishati na bei ya vipuri.

Hapa namaanisha uwezo wako wa kumudu kununua mafuta, kufanya matengenezo, "service" na kununua vipuri.
Karibu kwenye chama.
 
Kaka kama mfukowako umetoboka wewe baki kwenye IST ama Vitz RS Old model.waache wababe na mindinga yao ya 12 valve 6 cylinder full time full tank cc 400.
 
RUNX, ALLEX, PREMIO, ETC. Kwa bajeti yako zitakufaa Ila nasikitika zote zinakula mafuta.
 
Back
Top Bottom