Hiyo pesa ni nyingi sana, tafuta fundi wa laki 8, alafu tafuta dogo yoyote wa civil eng mpe laki 2, mwambie akusaidie tu kumshauri fundi wakati wa ujenzi wa msingi
Mimi ni mtaalamu sana kwenye hizo kazi, wapo mafundi watakuambia Hadi mil 3 kujenga tu msingi, achana nao.
Usilipe zaidi ya mil 1, ukilipa zaidi ya mil 1 umepigwa.
Tunachoangalia sio fundi anayejenga, bali wewe unayemsimamia. Unaweza kupata fundi mzuri Ila Kama hana msimamizi mzuri anaharibu na unaweza kupata fundi wa kawaida Ila ukamsimamia vizuri basi kazi inatoka bora Sana.
Ukienda kwenye mradi wowote wanaojenga ni mafundi mchundo tu wa kawaida, ila issue ni wasimamizi.